Sasa kabla hatujaanza kumsimamnga Wifi kambadilisha Kaka yetu, tuangalie kwanza Wifi alikuwa nani kwao, na je uamuzi wa Wifi kupumzika ki-career baada ya Kuzaa ni kum-support Kaka yenu(Mumewe) ki-career au ni njia tu ya yeye kula Mahela ya Kaka yenu? Je ndugu zake waliokuwa wakimtegemea hawateseki kwa kukosa "kipato" kutoka kwa Dada/Mwana wao?
Kwenye era hii ya Sosho Midia inabidi uwe makini sana maana info ni za kumwaga(tofauti na 2007 nilipoanza kublog), ni kweli baadhi zinasaidia hasa zile za Medical kutoka kwenye Site za Shirika la Ugojwa husika au Shirika la Afya Duniani. Lakini linapokuja suala la Ndoa au mahusiano, ongeza umakini kwasababu Ndoa hazina Kanuni Moja na watu hatufanani hata kama tulikaa tumbo Moja Miezi 9 na kuzaliwa kupitia Njia mooja na siku Moja bado tutatofautiana kwa kiasi fulani.
Maisha magumu, kila mtu anatafuta views na clicks siku hizi, mara zote(kama Wanasiasa) watu huamua kuongea au kuandika mambo ambayo wanajua watu watakuja mbio kutaka kuona/jua. Labda ni kwavile ndio wanachopitia hivi sasa au wanajiandaa just incase ikitokea watakuwa wanajua namna ya kupambana.
Siku moja "nilitumiwa" Video ya Mwanamke(as you do) akiwaasa Wanawake kama yeye kutowabadilisha Waume zao na kukamata Pesa zao na hivyo Waume hao "kusahau" Familia zao. Nikaendelea kusikiliza nikiamini kuwa anawazungumzia Vimada in which nilianza kumuunga Mkono.
Baadae akasema "utakuta Umeolewa na Mwanaume ambae alikuwa anategemewa na familia yake, lakini baada ya muda unambadilisha Mumeo na kuitelekeza Familia yake. Familia yake inateseka kwa ajili yako. Familia uliyomkuta nayo, iliyomlea, tuache kuwabadili Waume zetu". mmmh!
Nikajisemea "huyu Dada lazma hajasoma (hana Elimu ya juu) au ameolewa akiwa hana Kazi wala Majukumu kwenye Familia yake(Wazazi na Ndugu zake). Kuna akina sie ambao tulikuwa tunategemewa pia na Familia zetu, mpaka baada ya Kuzaa na Waume zetu. Je kuna mtu anaenda kueneza "Neno" kuwa Waume zetu wasitubadilishe Wake zao?
Wazazi wetu (sisi Wake) hawakutumia Pesa zao kutusomesha na kutupa maadili mema ili tuje "kuzalishwa" a.k.a "haribiwa shape" na kuacha Career zetu kwa Muda ili tulee watoto ambao wanabeba Jina lenu la Ukoo. Hebu wekeni Heshima, ebo!
Sijawahi kusikia mtu yeyote akilalamika kuwa Wake tumebadilishwa na Waume zetu baada ya kufunga nao ndoa, sio kwamba "hawatubadilishi" la hasha! tunabadilishwa pia.....tena sio kubadilishwa hehehehe, tunaharibiwa Shape na isitoshe kupatwa na Maradhi ya ajabu ajabu for the rest of our lives.
Sidhani kuwa tunawabadilisha Waume zetu, bali Majukumu na Vipaumbele vinabadilika. Watoto na Mkewe wanakuwa muhimu zaidi kwake kuliko Ndugu zake. Ndugu zake wamekua/watakuwa na maisha yao bila yeye. Yeye hakuwaleta Ndugu zake Duniani bali Wazazi wenu, kama yeye alivyo Mzazi kwa Watoto wake.
Kuna wakati Maisha hubadilika(mtu unakua mtu Mzima), Familia yako inakuwa Wewe, Mkeo/Mumeo na Watoto wenu. Wale mliozaliwa pamoja kama Familia mnakuwa sio "Familia" tena, mnabaki kuwa Ndugu wa Damu. Upendo na uzito/umuhimu upo pale pale, mtasaidiana ktk shida na mtatembeleana lakini hauwezi kuwa Tegemeo lao Kiuchumi.
Sawa, huyo ni Kaka yenu ambae ni Mume wa Mtu mwingine(Wifi yenu), mnamjua Kaka yenu tangu utoto wake lakini Mkewe anamjua Kaka yenu katika Kiwango kingine tofauti na cha kipekee ambacho hata mfanye nini hamuwezi kumjua kihivyo(sizungumzii Ngono hapa), sio nyie tu Ndugu zake bali hata Baba na Mama yenu.
Nathamini muda wako hapa, shukrani kwa kunichagua Mie leo.
Noo see ye efter.
Comments