Skip to main content

Akisema "tafuta mwingine, mie siwezi/nimechoka"....


...hamaanishi kwamba ukatafute  kweli mwingine, anachomaanisha ni kuwa "nibembeleze na unihakikishie kuwa utanivumilia" mpaka nitakapo kaa sawa Kihomono au kupona(kama alikuwa anaumwa)....Za Miezi Miwili/Mitatu? hello, jambo jambo!!


Kwa kawaida Mume anapopatwa na tatizo kubwa litakalomfanya ashindwe kutekeleza Majukumu yake kama Baba na Mume, Mwanamke atavumilia na kumuuguza, kumpa Moyo na Matumaini. Lakini Mwanamke akijifungua(zaa) achilia mbali kuugua....katoa Uhai wa Mtu salama baada ya Miezi 9 kukaa na kulala kwa tabu.


Mara zote kipindi hiki huwa Kigumu sana japokuwa kasumba ya Jamii "kukuharakisha" upone haraka huficha ukweli kuwa Mwanamke anapojifungua hukabiliana na mambo mengi Kiafya(kimwili, kihisia na kiakili). Hali ambayo hufanya baadhi ya Wanaume kuamini kuwa Mimba na kuzaa ni "cha mtoto" tu, sio kazi(kama alivyo pizi ndani ya dakika zake 3 kwa utambu uliodumu kwa sekunde 90)....hakuna ugumu wowote, fyatueni tu.



Kwa kawaida(uzoefu wangu) Mwanamke anapona pale alipotokea Mtoto ndani ya Wiki 4, lakini wapo baadhi huendelea "kuumwa" mpaka Miezi 3 au Sita. Kipindi hiki huesabiwa kuwa ni kigumu kwa Mume, kwasababu atapata wapi Tendo la Ndoa ikiwa Mkewe bado "anaumwa" kwa muda mrefu hivyo.



Presha hii siku zote hutoka kwa Wanawake wenzetu huko nje, na ndani huwa Mume husika(hasa kama sio muelevu). Mumeo anaweza kulalamika kwasababu haelewi unachokabiliana nacho na hivyo mnaweza kugombana(zozana) kutokana na upungufu au "uchelewaji" wa kurudia hali yako ya kawaida.


Kwa hasira hapo mwanamke anaweza kusema kama unashindwa kuvumilia mpaka nitakapo pona basi nenda katafute Mtu mwingine, mie siwezi! Mara nyingi hapa Mwanaume wa kipuuzi atakaa kimya akijua kapewa ruhusa.


Lakini Mume mwema na mwelevu atajitahidi kujua kwa undani kinachomsumbua mkewe, ataomba radhi na kuahidi kuendelea kuvumilia. Atakuwa karibu na Mkewe na kutoa ushirikiano zaidi. Wakati mwingine ushirikiano na uelevu wa  masuala ya uzazi kwa Mwanamke husaidia kwa kiasi kikubwa uponaji wa Mkeo baada ya kujifungua.


Sasa anaposema, "tafuta mwingine, mie siwezi" humaanisha "nipe ushirikiano, nielewe, nivumilie na unihakikishie kuwa huendi popote mpaka akae sawa".

Yep! Wanawake (karibu wote) hata mie ambae ni straight foward no corner kuna wakati namaanisha kitu kingine kabisa tofauti  na ninachomwambia Asali wa Moyo.....hasa nikiwa na Hasira.



Pamoja na kusema hayo yoooote hapo juu bado kama Mke  unaweza kutumia Kazi ya Mikono, Mdomo, Mipaka ya Makalio au vilevile unaweza kuongeza ukaribu na Mumeo kwa namna nyingine. Ila kuwa makini kwasababu Nyege zikikupanda ni wazi utapata "maumivu" fulani hivi maeneo ya K, nje na ndani kutokana na Msukumo wa Damu....bila Msukumo wa Damu, hakuna Nyege. eeeeh Moyo Sukuma Damu na si vingine, hihihihihi Ditto knew that akakupotosha!!



Endelea kuwepo, Post ijayo tuangalie jinsi Mke anavyolaumiwa "kumbadili" Mume asiipende na kujali Ndugu zake kwenye Ndoa. Je ni kweli tunawabadili? vipi kuhusu sisi Wake ambao  labda tulikuwa tunategemewa na Ndugu zetu lakini tukaacha "Career" zetu na kuwazalia/kuwalelea watoto wao? Usikuse.

Shukrani kwa Ushirikiano.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao