Skip to main content

Posts

Showing posts from January 16, 2022

Hebu tuone Past life yako: Kutelekezwa/Achwa...

Umekuwa na mama yako kwa Miezi 9 mpaka 11 kama ulikuwa na bahati, wengine ni miezi 6 na wengine karibu Mwaka(Miezi 12). Ni mtu pekee unaemfahamu, na unahisi kuwa upo salama na unapendwa, sababu Mtu huyu sio tu amehatarisha maisha yake ili kukubeba na kukuleta Duniani. Mtu huyu ataendelea "kuteseka" sababu unataka ule x4 usiku wa manane, ataendelea kukupenda, kukulinda, kukufunza na kukujali.  Hayo yote hutokea kwa Miezi 3 ya mwanzo, baada ya hapo unamuona mtu huyo Nusu siku, kila unapoachwa unalia sana. Siku zinavyozidi kwenda ukaribu wako na mtu huyo unapungua na kilio chako kinapungua. Kitendo cha Mtu huyo ambae sasa unamtambua kama Mama(au Anty, Dada wa Kazi ndio Mama yako) kukutelekeza/kukuacha huwa kinaumiza sana. Sasa umekua na unajitegemea kwenye mambo mengi kama vile kucheza peke yako, kujivisha viatu/nguo nk. Lakini bado ni Mtoto na bado unamuhitaji Mama yako. Jana la leo Mama amekua nyumbani siku zima, unahisi furaha, upendo na kujaaliwa.....Mama anaamua kutaka kuto