Skip to main content

Posts

Showing posts from November 29, 2015

Single Mum/Loner Parent, Mzazi Mmoja=no Help

Hi! Sitojifanya mjuaji kwenye hili, tangu sijawahi kuwa "single mother" iwe kwa kutaka (wale wanaoamua kushika Mimba bila kuwa na hitaji la mwanaume husika) au kwa bahati mbaya, kwamba kutofautiana kwenu kumefanya mmoja wenu abaki na mtoto/Watoto(hapa siwazungumzii Wajane au wale waliobakwa, hii ni issue nyingine). Ninaowagusia hapa ni wale ambao kuwa "single mother" ni Mtindo wa Maisha,Sifa, chanzo cha kuonekana Imara/Unaweza! Wengi hapa ni wale Wasichana waliokulia miaka ya 90s na wale wa early 2000s. Ule msukumo wa kutaka kujitegemea ukikuwa na "impact" kubwa kwetu kiasi cha kuhisi hatuhitaji Wanaume ili kuwa na Familia. Tuliamini kuwa tunaweza kufanya yetu kama Wanawake na tunaweza kufanya ya Wanaume pia, "ikiwa mwanaume anaweza hata mimi naweza" sort of Imani....hakika hakuna afanyacho Mwanaume ambachoo sisi hatuwezi kufanya, lakini kuna mambo ambayo hatuwezi kuyafanya kama Wanawake kwenye malezi ya Mtoto au watoto(h

Kukosoa na Kumcheka mtu ni "interest" yako?

Nakuona! Wengi huamini kuwa ukiwa na tabia ya kukosoa au kucheka watu wengine basi wewe utakuwa na Matatizo kwenye Maisha yako, maisha yakoo hayana furaha na yamejawa na Huzuni na hivyo kukosoa na kucheka watu ndio njia pekee ya kujipatia "furaha". Nakubali kwa kiasi fulani, kwa baadhi kuwa Hasi kwenye kila kitu  ni tatizo na linaathiri maisha yao ya kila siku. wengine huamua kuwa Hasi kama sehemu ya kupata "attetion" au "Trafic" na "Views" popote walipo kwenye Sosho Midia. Kwa wale wa Ughaibuni, Maisha mitaa hii yanaweza kuwa ya Upweke sana na hivyo kumfanya mtu kutumia muda wake mwingi kwenye kutafuta "furaha" kwa kuwa Negative towards watu wengine. Upweke wa huku unatokana na utofauti wa Kitamaduni, Utaratibu wa kazi za "shift",  Majira ya Mwaka(Kiza kuingia mapema) vilevile kutumia muda mwingi kusafiri to na from work....by the time unafika nyumbani upo hoi, tayari ni Giza hivyo  hakuna muda wa kutoka au kukarib