Nakuona!
Wengi huamini kuwa ukiwa na tabia ya kukosoa au kucheka watu wengine basi wewe utakuwa na Matatizo kwenye Maisha yako, maisha yakoo hayana furaha na yamejawa na Huzuni na hivyo kukosoa na kucheka watu ndio njia pekee ya kujipatia "furaha".
Nakubali kwa kiasi fulani, kwa baadhi kuwa Hasi kwenye kila kitu ni tatizo na linaathiri maisha yao ya kila siku. wengine huamua kuwa Hasi kama sehemu ya kupata "attetion" au "Trafic" na "Views" popote walipo kwenye Sosho Midia.
Kwa wale wa Ughaibuni, Maisha mitaa hii yanaweza kuwa ya Upweke sana na hivyo kumfanya mtu kutumia muda wake mwingi kwenye kutafuta "furaha" kwa kuwa Negative towards watu wengine. Upweke wa huku unatokana na utofauti wa Kitamaduni, Utaratibu wa kazi za "shift", Majira ya Mwaka(Kiza kuingia mapema) vilevile kutumia muda mwingi kusafiri to na from work....by the time unafika nyumbani upo hoi, tayari ni Giza hivyo hakuna muda wa kutoka au kukaribisha watu kwako as kesho unatakiwa Kazini.
Nilipokuwa Teen nilijulikana kwa baadhi ya wanafunzi wenzangu kuwa "Dinah siku zote huwa na sababu ya kukosoa", nilikuwa na tabia ya kuchea watu, haijalishi mtu kafanya nini jema lazma nitapata/ona Kasoro na kukosoa....by doing that wenzangu walikuwa wanacheka balaa!
Sasa, Darasa letu lilikuwa juu (Ghorofani) na hivyo tulikuwa na tabia ya "kuwachora" Wanafunzi na Wageni waliokuwa wanakatiza maeneo ya Nje ya Gate ay ndani ya Gate. Wakati mwingine nilikuwa busy na mambo mengine, lakini bado wataniita ili nione kasoro ya watu au mtu na hivyo wao kupata Burudani.
Ilifikia mahali nikachukulia kuwa kucheka watu ni "interest" yangu, kiukweli napenda kucheka na huwa najicheka mwenyewe.....lakini kucheka watu haikuwa sahihi. Mwaka 2010 ndio nikaamua kubadilika. Ni baada ya kushika Mimba.....Mimba ikanibadilisha. Nikatambua kuwa unapokosoa mtu ama watu kama sehemu ya "burudani" ni wazi kuwa unatatizo, sikuwa na sababu ya kukosoa na kucheka watu.
Unapomkosoa mtu kila siku hata kwa yale mema au yale yasiyohitaji "maoni" yako huko kunakuwa sio kukosoa tena bali ni kumchukia mtu huyo. Kwanini umchukie mwenzio/wenzio? wamekukosea nini? Pamoja na tabia hiyo ya ajabu bado sikuwahi kucheka Walemavu, Wenye matatizo au Masikini zaidi yangu.
Era ya Sosho Media imewarahisishia wale watu ambao wapo kama nilivyokuwa mimi huko nyuma. Tofauti ni kuwa mimi nilikuwa nafanya hivyo bila kuwagusa wahusika moja kwa moja. So walikuwa hawajui nawakosoa kuhusu nini. Siku hizi mtu anakufuata live kwenye "profile" na kuanza kukukosoa.....anakuwa na utaratibu huo kila siku.
Mwaka 2013 niliugua PD(stori yake itakuja siku ingine)....baada ya kupona nikajifunza kuwa "Chanya" kwa Msaada wa Daktari. Hapa ndio nilipojifunza kuwa mambo mengi yanatokea kwenye Maisha ya mtu, huwa kuna sababu. Mpaka uijue sababu ya yeye kufanya alicho/anachokifanya ndio umkosoe. Kama hujui basi muache kama alivyo.
Kukosoa ni tofauti na Kujaji......bado najaji (siwezi kujizuia), pamoja na kuwa nitakujaji bado sitokucheka. Heeey, ahsante kwa kuichagua Blog hii. Tambua nathamini na kuheshimu muda wako hapa.
Babai.

Comments