Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kuzaa

Mpenzi akuone uKizaa vs uKinya.....

Kuna mambo mengine bana ni too personal. Binafsi bora  Asali wa Moyo anione nikizaa(done twice) kuliko anione nikiwa Nashundi. Hii ni Topic ambayo hufanya baadhi ya watu wadhani kuwa hawapendwi vya kutosha. Kwamba kama unapenda mwenzio basi usione aibu Kupumua au Kutoa Haja Kubwa mbele yake. Kama nilivyosema hapo awali kuwa Mie binafsi naamini kuwa Kupumua au kutoa Haja Kubwa ni tendo la "usiri" na ni "personal"......kwasababu tu unaniingilia Kimwili na kuniona Mtupu kila siku, haina maana una "Haki ya Msingi" kuniona nikinya au kusikia nikijamba au hata kuvuta harufu ya Ushuzi wangu nikiwa Macho na nina fahamu zangu kamili(kujamba wakati umelala haihesabiki). Miaka yote niliyoishi na Mume wangu sijawahi Kujamba mbele yake....achilia mbali kujisaidia Haja kubwa akiwa anaoga au anafanya jambo Bafuni. Inawezekana na Makuzi/Malezi ambayo labda Kisaikolojia yamefanya nishindwe kufanya tendo la Kujamba mbele ya watu. Kwetu tulifunzwa kuwa ukitaka ...

Kupoteza Nywele baada ya Kujifungua Update (Bidhaa)....

Natumaini Post hii itakukuta ukiwa Mzima wa afya. Kama nilivyoahidi, leo nitakuelezea utaratibu wangu uliosababisha nywele(Relaxed) zangu kurudia Afya yake baada ya kuzipoteza na kupata "upara" wa muda. Jikoni kuna mwanga asilia, sihifadhi Bidhaa hizi Jikoni....hihihi! Ukiachilia mbali kuongeza aina ya Mboga iitwayo Kale kwenye Mlo wangu wa kila siku na kula Mayai 2-3 kila asubuhi. Bidhaa hizi zimechangia kwa kiasi kikubwa kuzuia Nywele zangu kuendelea kung'oka/anguka baada ya Kujifungua. Utaratibu wangu Rahisi. Kila Siku: Napaka Cantu Shea Butter kila siku asubuhi na Jioni na baada ya kupaka Cantu huwa na-"seal" na Mafuta asilia ya Sweet Almond. Kila Wiki: Huosha na Deep Condition Nywele zangu mara Moja (kila Ijumaa/JumaMosi) na huwa natumia Cream of Nature shampoo. Baada ya hapo nafanya deep condition kwa kutumia Vitale Mayonaise ambayo huwa nachanganya na Hello hydration (haipo pichani) na aina 2 za Mafuta asilia ambayo ...

Tumezaliwa ili tuzae....

....ndio Asali wa Moyo anaamini hivyo, which is Sad really.....but hey mepata topic! Wazazi wako walipoamua kuanza familia nadhani ilikuwa ni maana ya Ndoa, kwamba mtafanya Tendo hilo ili kuzaliana. Nia na dhumuni la Tendo la Ngono ni kuzaliana, kama hutaki kuzaa basi tumia Kinga (usiolewe/usioe) si ndio?!! Kwasisi wa kileo ambao tunabaki Shule kwa muda mrefu, Muda wa kufanya Tendo kwa "haki" (kuzaliana) huwa  sio muhimu, lakini pia sio wote tunaweza kuvumilia mpaka muda ufike...hivyo tunaanza Ngono kabla ya Ndoa nakujikinga "Kizungu" Dhidi ya "kuzaliana". Wazazi kutuzaa sisi ilikuwa uamuzi wao, haikuwa lazima na hakuna aliewalazimisha, sasa kwasababu tu nilizaliwa haina maana na mimi ni lazima nizae. Suala la kuzaa sio rahisi (kwa mwanamke ambae ndio anaezaa)kama ambavyo wengi wanafikiria. Mwili wa Mwanamke ni wa ajabu in a good way, Ukiachilia mbali Athari na Mabadiliko makuu(mengine yanahatarisha uhai) kwa Mwanamke kwa ndani baad...

Kukosoa na Kumcheka mtu ni "interest" yako?

Nakuona! Wengi huamini kuwa ukiwa na tabia ya kukosoa au kucheka watu wengine basi wewe utakuwa na Matatizo kwenye Maisha yako, maisha yakoo hayana furaha na yamejawa na Huzuni na hivyo kukosoa na kucheka watu ndio njia pekee ya kujipatia "furaha". Nakubali kwa kiasi fulani, kwa baadhi kuwa Hasi kwenye kila kitu  ni tatizo na linaathiri maisha yao ya kila siku. wengine huamua kuwa Hasi kama sehemu ya kupata "attetion" au "Trafic" na "Views" popote walipo kwenye Sosho Midia. Kwa wale wa Ughaibuni, Maisha mitaa hii yanaweza kuwa ya Upweke sana na hivyo kumfanya mtu kutumia muda wake mwingi kwenye kutafuta "furaha" kwa kuwa Negative towards watu wengine. Upweke wa huku unatokana na utofauti wa Kitamaduni, Utaratibu wa kazi za "shift",  Majira ya Mwaka(Kiza kuingia mapema) vilevile kutumia muda mwingi kusafiri to na from work....by the time unafika nyumbani upo hoi, tayari ni Giza hivyo  hakuna muda wa kutoka au kukarib...