Kuna mambo mengine bana ni too personal. Binafsi bora Asali wa Moyo anione nikizaa(done twice) kuliko anione nikiwa Nashundi.
Hii ni Topic ambayo hufanya baadhi ya watu wadhani kuwa hawapendwi vya kutosha. Kwamba kama unapenda mwenzio basi usione aibu Kupumua au Kutoa Haja Kubwa mbele yake.
Kama nilivyosema hapo awali kuwa Mie binafsi naamini kuwa Kupumua au kutoa Haja Kubwa ni tendo la "usiri" na ni "personal"......kwasababu tu unaniingilia Kimwili na kuniona Mtupu kila siku, haina maana una "Haki ya Msingi" kuniona nikinya au kusikia nikijamba au hata kuvuta harufu ya Ushuzi wangu nikiwa Macho na nina fahamu zangu kamili(kujamba wakati umelala haihesabiki).
Miaka yote niliyoishi na Mume wangu sijawahi Kujamba mbele yake....achilia mbali kujisaidia Haja kubwa akiwa anaoga au anafanya jambo Bafuni.
Inawezekana na Makuzi/Malezi ambayo labda Kisaikolojia yamefanya nishindwe kufanya tendo la Kujamba mbele ya watu. Kwetu tulifunzwa kuwa ukitaka "kupumua" toka nje au nenda chumbani/chooni na ubaki huko mpaka harufu iishe au fungua dirisha na jipepee. Hitaji la kujamba huwa haliji unless nipo peke yangu......hihihihi najua, Kipaji hiki.
Pamoja nakusema hivyo bado kuna wakati (kwa Wanawake)unaeza kujisaidia(kutokwa na Haja kubwa) wakati wa Kujifungua.....yeah hii haina kuTigOliwa, kuna Wanawake hawajawahi guswa Tigoni na bado ile siku ya siku(Kuzaa) wanaanza na Dinfi(Kinyesi) kwanza......tunaita "safisha njia".
Mama na Bibi yako na Somo yako aliekufunda kamwe hawawezi kukuambia hili(Hongera kwa kuichagua Blog hii sasa unajua).....wao husisitiza kula ushibe ili upate nguvu ya kusukuma pale Uchungu unapoanza hihihihihi ukila Mkimama umekwishaaaaa, lazma ushundi kabla Mtoto hajatoka.
Sisemi usile ila ni muhimu kuepuka vyakula vigumu au vya Wanga unapofikia Wiki ya 39. Kunywa sana Maji na kula Matunda(utaishia kukojoa) usiku kabla ya siku siku unayotarajia kujifungua.....vinginevyo jiachie tu.....kuleta kiumbe Duniani sio kazi ndogo na hata kama Mpenzi akiona unavyojikamua na Mavi kukutoka sio kwa Kunya bali kuzaa Mwanae si ndio!......haiesabiki!!
Sasa ikiwa na wewe unaamini kuwa Kujisaidia Haja kubwa ni vema Mwenza asijue aunkuona unavyojikamua, usijione wa ajabu au Mpweke. Mie pia naamini hivyo.
Kuna vitu vingine vinapaswabkutoonwa au shuhudiwa, haijalishi mnapendana lwa kiasi gani(kama ni mgonjwa sasa hivyo ni anaza kesi).
Naheshimu nankuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments