Skip to main content

Posts

Showing posts with the label aibu

Wanaume hawajui kunung'unika/kukaa na Kinyongo....

....Sosho Midia si imewabadilisha? Hakika bado wapo hivyo ila namna wafanyavyo ni tofauti na walivyokuwa wakifanya kabla ya Sosho Midia(nionavyo mimi). Unakumbuka ulipokuwa mdogo(au ni mimi tu), Baba yako akisikia jambo kutoka kwa Mwanaume mwenzie halizungumzii ila anakwenda kwa huyo Mtu na kuzichapa/kumkung'uka Magumi? well Baba yangu alikuwa mtu Mwema na Mtu wa watu lakini alikuwa Ngumi Mkononi, anakutandika halafu yanaisha. sasa hii ndio "Wanaume hawakai na Kingongo" niijuayo mie. Niliendelea kuona hiyo  kwa Kaka zangu na rafiki zao pia na hivyo kuweka Sementi kwenye hilo. Siku hizi Waanaume, wanaanika mambo ya wenzao nje (mitandaoni)ikiwa wamekorofishana, kwamba mmoja akiudhiwa/kasirishwa na mwenzie basi Jamaa wa Shosho Midia wote watajua. Kwa sisi Wanawake ambao hufikiria baada ya action(sio kabla) na kisha kuomba msamaha baada ya kuharibu ni Kawaida(ilizoeleka hivyo), lakini sio kwa Wanaume. Sio kwamba  nasikitika kuwa Wanaume wamebadilika na wala s

Mpenzi akuone uKizaa vs uKinya.....

Kuna mambo mengine bana ni too personal. Binafsi bora  Asali wa Moyo anione nikizaa(done twice) kuliko anione nikiwa Nashundi. Hii ni Topic ambayo hufanya baadhi ya watu wadhani kuwa hawapendwi vya kutosha. Kwamba kama unapenda mwenzio basi usione aibu Kupumua au Kutoa Haja Kubwa mbele yake. Kama nilivyosema hapo awali kuwa Mie binafsi naamini kuwa Kupumua au kutoa Haja Kubwa ni tendo la "usiri" na ni "personal"......kwasababu tu unaniingilia Kimwili na kuniona Mtupu kila siku, haina maana una "Haki ya Msingi" kuniona nikinya au kusikia nikijamba au hata kuvuta harufu ya Ushuzi wangu nikiwa Macho na nina fahamu zangu kamili(kujamba wakati umelala haihesabiki). Miaka yote niliyoishi na Mume wangu sijawahi Kujamba mbele yake....achilia mbali kujisaidia Haja kubwa akiwa anaoga au anafanya jambo Bafuni. Inawezekana na Makuzi/Malezi ambayo labda Kisaikolojia yamefanya nishindwe kufanya tendo la Kujamba mbele ya watu. Kwetu tulifunzwa kuwa ukitaka &quo