Skip to main content

Posts

Showing posts from May 17, 2015

Ni kweli wa Ughaibuni wajuaji....

Ndio na Hapana.....hello, jambo kabisa? Wengi sio wajuaji (wanajua sana)ila nadhani ni wazuri kwenye kufananisha..... ukifananisha system ya UK na Tza kwa mfano hakika uta-sound mjuaji(kumbe ni bongolala tu). Kingine kinachofanya udhani kuwa wa Ughaibuni wanajifanya wajuaji ni uhuru wa kusema, kwamba kila mtu ana Maoni yake kuhusu kila kitu kinachotokea au anachokisoma na pengine kushuhudia. Uhuru huo (ahsante nyingi kwa Gugo) unafanya baadhi yetu kuweka maoni yetu  kwenye issue yeyote ambayo tunahisi inatugusa. Nikianza kukupa (maoni yangu) mbinu za kukusanya Kodi (nita-base zaidi na system ya UK ambayo naijua lakini wewe huijui) na kuitumia Kodi hiyo kwenye kuboresha Maisha ya Watanzania waishio maisha Duni hakika utaniona nina Akili kweli na ninafaa kuwa Waziri. Kumbe katika hali halisi mie ni m-bovu wa Hisabati na Masuala ya Kiuchumi siyajui lakini ni mzuri kwenye kujieleza so nikipata "material" naweza kuyaelezea kwa urahisi na kueleweka bila kutumia "stat

Kwanini Weusi sana huenda na Wazungu?

Herooo heri ya J'3! Unakumbuka ile vita ya Weusi na Weusi wenye rangi ng'avu(wewe unawaita Weupe) niliyoigusia hapa mawiki kibao yaliyopita?....haiwezi kuisha hasa kwa nchi hizi za mbele. Kufunga ndoa na mtu Mweupe zaidi yako ni kupoteza muda, Baadhi ya wanadamu (Weusi) wanaamini kuwa unless mwenza wako ni Mzungu.....uhusiano wenu hautodumu. Mmmh come to think of it.....Weupe(Wazungu) wengi(niwaonao) wakiamua kuoa au kuolewa huenda Darker. Umewahi kuona Wazungu wangapi wanafunga ndoa na Waafrika ambao ni a bit lighter/fair. Halafu ukifanya Uchunguzi wako binafsi ambao sio rasmi (obviously)kwenye Sosho Media utagundua au utaona walio na Wazungu kama wenza wao ni weusi sana(deep dark). Lakini pia Ndoa au Mahusiano hufikia mwisho kwasababu nyingine nyingi na Rangi sio moja ya sababu hizo. Hivi ujawahi kujiuliza kwanini wanaume wa Kizungu hujibebea wadada Weusi warembo kweli (model like kiumbo) tofauti na Wanaume Weusi ambao hujikusanyia wamama_____well hurudi home na