Herooo heri ya J'3!
Unakumbuka ile vita ya Weusi na Weusi wenye rangi ng'avu(wewe unawaita Weupe) niliyoigusia hapa mawiki kibao yaliyopita?....haiwezi kuisha hasa kwa nchi hizi za mbele.
Kufunga ndoa na mtu Mweupe zaidi yako ni kupoteza muda, Baadhi ya wanadamu (Weusi) wanaamini kuwa unless mwenza wako ni Mzungu.....uhusiano wenu hautodumu.
Mmmh come to think of it.....Weupe(Wazungu) wengi(niwaonao) wakiamua kuoa au kuolewa huenda Darker. Umewahi kuona Wazungu wangapi wanafunga ndoa na Waafrika ambao ni a bit lighter/fair.
Halafu ukifanya Uchunguzi wako binafsi ambao sio rasmi (obviously)kwenye Sosho Media utagundua au utaona walio na Wazungu kama wenza wao ni weusi sana(deep dark).
Lakini pia Ndoa au Mahusiano hufikia mwisho kwasababu nyingine nyingi na Rangi sio moja ya sababu hizo.
Hivi ujawahi kujiuliza kwanini wanaume wa Kizungu hujibebea wadada Weusi warembo kweli (model like kiumbo) tofauti na Wanaume Weusi ambao hujikusanyia wamama_____well hurudi home na watoto wao kila mwaka lakini Mkewe haji....kwanini?
Asali wa Moyo ana-share Picha zake na watoto bila mimi hihihihi wale wale....angalau mie sio Mzungu bana.
Babai.
Comments