Skip to main content

Posts

Showing posts with the label wanaume

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao

Wanaume hawajui kunung'unika/kukaa na Kinyongo....

....Sosho Midia si imewabadilisha? Hakika bado wapo hivyo ila namna wafanyavyo ni tofauti na walivyokuwa wakifanya kabla ya Sosho Midia(nionavyo mimi). Unakumbuka ulipokuwa mdogo(au ni mimi tu), Baba yako akisikia jambo kutoka kwa Mwanaume mwenzie halizungumzii ila anakwenda kwa huyo Mtu na kuzichapa/kumkung'uka Magumi? well Baba yangu alikuwa mtu Mwema na Mtu wa watu lakini alikuwa Ngumi Mkononi, anakutandika halafu yanaisha. sasa hii ndio "Wanaume hawakai na Kingongo" niijuayo mie. Niliendelea kuona hiyo  kwa Kaka zangu na rafiki zao pia na hivyo kuweka Sementi kwenye hilo. Siku hizi Waanaume, wanaanika mambo ya wenzao nje (mitandaoni)ikiwa wamekorofishana, kwamba mmoja akiudhiwa/kasirishwa na mwenzie basi Jamaa wa Shosho Midia wote watajua. Kwa sisi Wanawake ambao hufikiria baada ya action(sio kabla) na kisha kuomba msamaha baada ya kuharibu ni Kawaida(ilizoeleka hivyo), lakini sio kwa Wanaume. Sio kwamba  nasikitika kuwa Wanaume wamebadilika na wala s

Usenge + Ubunifu wa Mavazi=Skinny Models

Unaamini katika Chunguzi za Kisayansi? Mie naamini zile za Kitibabu(ambazo ni Sayansi pia.....kabla hujanijaji, tambua kuwa kuna Sayansi za aina nyingi....Viumbe,Mimea,Siasa,Kemikali n.k). Natumaini wewe ni mzima kabisa. Kama ujuavyo suala la Waonyesha mavazi/Wanamitindo kuwa Size Sufuri ni pana na mpaka likaingizwa kwenye Siasa(likafeli). Lakini bado hawa wafanya biashara watumiao Miili yao kuonyesha mavazi(Models/Wanamitindo) wanaandamwa kutokana na wembamba wao. Baadhi ya watu "mtaani" wanadai kuwa Wabunifu wanachagua "unreal women" kwasababu wao(most of them) ni Mikorosho/Wasenge na hivyo nguo wanazobuni ni za kutosha Wavulana na sio Wanawake......Unabisha?, endelea kusoma sasa. Kiasilia Mwanaume anaevutiwa na kupendeza kwa mwanamke atazingatia Umbile la Mwanamke, kwamba juu Mdogo halafu chini mkubwa/pana(Peasi)  au Juu mkubwa , kati mdogo halafu chini mkubwa pia(namba nane)....tuliobaki ni WAVULANA hihihihihi. Sasa kwa Msenge ambae ni Mbu

Kuoga Usiku Vs Asubuhi/Mchana!

Haiyaaa! Kiangazi Kimeisha na Mvua ime-cotton fire, hii sio sababu ya wewe kuacha kuoga. Usafi wa Mwili ni muhimu kama vilivyo vitu vingine Maishani. Lakini je wewe unaoga mara ngapi kwa Siku? na je kuna ulazima wa kuoga zaidi ya mara moja kwa Siku? Wanawake tunapewa/peana PRESHA kuoga-oga  mara nyingi na tunaambiwa tusipooga tunatoa harufu kwa sababu ya Maumbile yetu, lakini wanasahau kuwa kunakosababisha harufu sio mwili as in Ngozi, bali kwapa na kunako(Nyeti) ambazo hata wanaume wanazo na zinatema harufu pia ikiwa hazitaoshwa. Sasa nikianzia mwisho, hakika kuna ulazima wa kuoga zaidi ya mara Moja kwa siku, Inategemea unafanya kazi gani na wapi, unatumia Usafiri gani(kubanana  kwenye daladala/train hakika unabeba wadudu) na bila kusahau hali ya hewa. Ikiwa unafanya kazi Hospitali(una deal na maambukizo), unaishi mahali penye joto sana au kazi yako inakufanya utoke jasho sana mpaka unanata basi wewe oga mara zote unazohitaji. Kitibabu tunapaswa kuoga angalau

Knowledge vs Ego....

Kwa maCeleb Ego hujionyesha wazi kwenye mahojiano ya moja kwa moja. Baadhi wanadhani kuwa ni wao tu ndio wanazo hizo Ego, nitakupa mfano na pengine kukusaidia(kama hujui) kuitambua kutoka kwa Mwenza wako. Kwa mimi na wewe Ego zetu hujitokeza zaidi pale tunapogombana. Ndoani/Mahusiano huwa tunagombana sana eti? Wakati mwingine ugomvi unakuwa hauna hata maana. Ujue kuna ile kugombana kwasababu mmoja wenu kafanya kosa kubwa kama vile umegundua kuwa amekuwa akipeleka Pesa mahali ambapo hupajui! Kwa mfano. Sio kwanini hakupokea simu?!! Na ikiwa mnawatoto basi mnaweza kugombana kwasababu mmoja wenu anahisi kuwa anaingiliwa kwenye kona yake ya malezi(wanaume) au mwingine(sisi wakimama) kuhisi kuwa watoto wanaonewa au mwenzio hatoi muda kuwaelewa watoto na badala yake anatanguliza kufoka (hasira) kwa watoto. Katika hali halisi kama mmoja wenu anawakilisha linalomkwaza kwa namna ya kawaida(kukereka bila hasira/kufoka) na mwingine kusikiliza hakutokuwa na ugomvi. Inaitwa MAWASILIANO/K

Wanawake na Usenge!

Kwanini sisi wakimama ni wepesi sana kukubali hawa jamaa?.....Hi are you well? Usinielewe vibaya! Siwachukii wanaojibadilisha kutoka Jinsia moja kwenda nyingine(I feel sorry kwa mume/mke na watoto though). Pia sina habari na Wanaume wanaopenda kujiremba au kuvaa nguo za kike. Hakika sijali nini mwanaume na mwanaume mwenzie au mwanamke na mwanamke mwezie wanafanya chumbani kwao(keep it there). Lakini sitoacha kujiuliza au kuuliza ni nini hasa kinafanya wanawake kuwa wepesi kuwakubali hawa jamaa kwenye Jamii? Kwanini sisi ni wa kwanza kuwachukulia poa na hata kurafikiana nao? Ni ile "huruma nature" tulioumbwa nayo au ni kwasababu Wanaume wengi ni Waoga wakidhani hali hiyo(Usenge) inaambukiza so wanakuwa wagumu au wenye Chiki/hasira wakihofia "kubadilishwa"? Pengine wanaogopa kuwadondokea Wasenge wa Kiume hihihihihi kama unaeza mtamani wa jinsia yako akiwa Mtupu na ukawimika wewe ni Msenge tu hata kama umeoa na unawatoto.....usiogope toka Kabatini. Back to the po

Kwanini Weusi sana huenda na Wazungu?

Herooo heri ya J'3! Unakumbuka ile vita ya Weusi na Weusi wenye rangi ng'avu(wewe unawaita Weupe) niliyoigusia hapa mawiki kibao yaliyopita?....haiwezi kuisha hasa kwa nchi hizi za mbele. Kufunga ndoa na mtu Mweupe zaidi yako ni kupoteza muda, Baadhi ya wanadamu (Weusi) wanaamini kuwa unless mwenza wako ni Mzungu.....uhusiano wenu hautodumu. Mmmh come to think of it.....Weupe(Wazungu) wengi(niwaonao) wakiamua kuoa au kuolewa huenda Darker. Umewahi kuona Wazungu wangapi wanafunga ndoa na Waafrika ambao ni a bit lighter/fair. Halafu ukifanya Uchunguzi wako binafsi ambao sio rasmi (obviously)kwenye Sosho Media utagundua au utaona walio na Wazungu kama wenza wao ni weusi sana(deep dark). Lakini pia Ndoa au Mahusiano hufikia mwisho kwasababu nyingine nyingi na Rangi sio moja ya sababu hizo. Hivi ujawahi kujiuliza kwanini wanaume wa Kizungu hujibebea wadada Weusi warembo kweli (model like kiumbo) tofauti na Wanaume Weusi ambao hujikusanyia wamama_____well hurudi home na

Mvaa Vimini na mzaa ovyo....

....nani hajiheshimu? Mambo vipi? Uchaguzi umepita....maisha yameanza upya Jana na Pound imeshuka thamani. Maana Ijumaa ilishuti mpaka kufikia 2,900Tsh(why am i telling you this? Never mind). Kuna wakati mtu unachoka kujielezea na kuelewesha baadhi ya watu kuwa Mavazi ya mtu sio tabia na mavazi mafupi sio kielelezo cha mtu kutokujiheshimu. Natambua kuna tofauti ya ufupi wa mavazi kulingana na umri japokuwa umri sio sababu ya mtu kubadilisha style yake ambayo anadhani kuwa inampendeza kulingana na shape yake au kulingana na kuonyesha kilicho "perfect" ili kuondoa attention kwenye kile akionacho kuwa ni "imperfect" (miguu vs sura) hiihihihihi mie. Sasa unapomuita mvaa nguo fupi kuwa ni Malaya, hajiheshimu au Changudoa(uchangudoa ni kazi japo siiungi mkono) na kumtukuza mvaa mavazi marefu na ya kujificha(eti heshima) lakini ana watoto 3+ kutoka wanaume watatu tofauti unakuwa bwegelao(bongwa la mabwege). Kabla hujachukia au kuponda vazi la mtu ambalo unadhan