Thursday, 4 June 2015

Wanawake na Usenge!

Kwanini sisi wakimama ni wepesi sana kukubali hawa jamaa?.....Hi are you well?


Usinielewe vibaya! Siwachukii wanaojibadilisha kutoka Jinsia moja kwenda nyingine(I feel sorry kwa mume/mke na watoto though). Pia sina habari na Wanaume wanaopenda kujiremba au kuvaa nguo za kike.Hakika sijali nini mwanaume na mwanaume mwenzie au mwanamke na mwanamke mwezie wanafanya chumbani kwao(keep it there).
Lakini sitoacha kujiuliza au kuuliza ni nini hasa kinafanya wanawake kuwa wepesi kuwakubali hawa jamaa kwenye Jamii? Kwanini sisi ni wa kwanza kuwachukulia poa na hata kurafikiana nao?Ni ile "huruma nature" tulioumbwa nayo au ni kwasababu Wanaume wengi ni Waoga wakidhani hali hiyo(Usenge) inaambukiza so wanakuwa wagumu au wenye Chiki/hasira wakihofia "kubadilishwa"?


Pengine wanaogopa kuwadondokea Wasenge wa Kiume hihihihihi kama unaeza mtamani wa jinsia yako akiwa Mtupu na ukawimika wewe ni Msenge tu hata kama umeoa na unawatoto.....usiogope toka Kabatini.Back to the post: Binafsi (dada mkubwa) mwenye Wadogo wa Kiume. Hakika nilikuwa napata hasira nikifikiria vipi madogo wakiwa  Wasenge? Nitawachukia? Nitawaua?


Natambua hii ni hofu ya wazazi wengi(hasa wa kiume) na can break your heart lakini kutokana na Mazigira yalivyo sasa na urahisi wa kufikia au kipatabinfomations ni vema tubadilishe namna tunakuza wenetu.


Kamwe sitokufundisha  namna ya kumlea mwanao au kukuambia lea mwanao kama nileavyo wanangu......mwenyewe najifunza daily hapa.


Nina Kijana na Binti.....je huwa namfikiria Mwanangu wa kiume kwenda kwingine na hivyo kujitahidi kumlea kama MWANAMUME? Hapana!


Nawalea wanangu kama wanangu....kila moja anajijua kuwa yeye ni a Girl na mwingine ni a boy so i go with flow.


Babuu akilia-lia au kunung'unika simuambii "boys dont cry.....au dont cry like a girl" namwambia a 4yr old...grown nursery boy dont cry like a stay home baby. Hapendi kuitwa baby na hapendi kukaa nyumbani so that works.Unapoanza kum-feed mtoto kuwa Wavulana ni  Wakakamavu, Jasiri, hawalii au kuwa emotional ni wazi kuwa unamwambia mwanao wa kiume "usiwe kama msichana" au Wasichana ni Wadhaifu.Watu wenye tabia hii ni wanaume ambao hawathamini mwanamke na nadhani wanahofu kuu kuwa watoto wao watakuwa Wasenge.....wakidhani Usenge ni kuwa mwanamke.Usenge sio Uanamke.....kupenda kuvaa mavazi ya kike au kujiremba sio Uanamke....kuwa na Matiti sio Uanamke.....kuwa mbeya sio Uanamke.Mimi kama mwanamke najiamini na kukuambia kuwa Uanamke ni zaidi ya kuwa emotinal.....unamke ni zaidi ya kulia-lia na mengine ambayo Wanaume mnaita "tabia za kike"Nimechanganya topics didn't I? 2-in 1 Blog post si ndio. Asante kwa kuichagua blog hii.

Babai.

No comments: