Tuesday, 9 September 2014

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!!


Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana!

Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima.

Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu).

Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!!

Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu".

Kaongeza: "Vumilia tu mwanangu, ndio Ukubwa huo, Vaa Bra kusapoti Uzito".....anyway baada ya Wiki yakaanza kukauka na kurudi yalivyokuwa kabla sijazaa.

Sasa leo nimeamua kumuachisha Binti yangu, yaani hakuna ku-give in.....atalia, atarusha tantrums (maana ni kabingwa) walaaaa sijali.
Haya ni pale Mshauri anapoomba Ushauri....anyone?!!


Babai.
Mapendo tele kwako...

8 comments:

Unknown said...

Bado naendelea kukuheshimu kwa mada zako ambazo nilikuambia katika comment yangu ingine huko nyuma kuwa inanikumbusha 'mie' mwingine kimawazo yako na u'endawazimu' wako in writting. Hongera.

Mie pia alinyonya jamani, hadi miaka miwili. Na hakuwa na dalili za kuacha. Ila nikaanza kusikia aibu. Maana kilikuwa na mwili hicho sasa mtoto mkubwa hadi mnahojiana wakati ananyonya!!

Na hivi ni ka-much-know! Sasa mnaanza kabunge ka katiba wakati wa kunyonya. Of koz mi nilikuwa na enjoy maana ni mwanangu pekee ( sikuwa na mpango wa kuongeza baada ya kukawia -kwa kipimo cha binadamu, kuingia stage hiyo ya uzazi) lakini nikaona sasa too much. Mwisho aanze kwenda nursery akirudi mama nyonyo.
Hadi ananiuliza kabla hajanyonya kama nimeshalisafisha nyonyo na maji safi na sabuni! ( ka-much know hatari!)

Kuna jirani yetu fulani though, alimnyonyesha mwanaye hadi akiwa na miaka 7. Am not kidding. Ingawa nadhani mwishoni it was just for fun sio kuwa maziwa yalikuwa yanatoka. Sijui ndio kudekeza au ni aje, nakumbuka anatoka shule na kaptula ya bluu primary, mamake anamwambia niko huku njoo unyonye na kweli mvulana yule anadanda , miaka ile hakuna tuition wala nini..mkirudi mnakuta mama anasonga ugali so anadinya palepale mama kashika lile banio la ugali!

nakaonea huruma kabinti kako lakini kataweza tu kama huyu kipepe wangu aliweza though shurt kwa kumwambia kuwa ni machafu na sijayaosha na ofkoz na local excuses za kizamani kuwa nimeweka pilipili na kuwa kuna dinosaur au mdudu kwenye nyonyo.

Kazi njema Bidada

Dinah said...

Ahsante sana kwa Comment! Heshima back at ya! Mpaka leo tunaendelea vema, Kananyonya Usiku tu(kunipunguzia discomfort ya Ujazo). During the day hakanisogelei kabisa.....nahisi kushinda hehehe.

Unknown said...

M na mtoto wa miezi 18 lkn hataki kula kabisa na kibaya zaidi kilo hakaongezeki kabisa manes wamenishauli nikaachishe kunyonya Lkn naogopa coz nikadogo sana

Unknown said...

Me nimeachisha mtt lakin maziwa hayajajaa wala hayaumi mwanangu ana miaka miwili ni kawaida hua inatokea mwingine hapa maumiv ya maziwa au nitakua nimenasa

Unknown said...

Sasa akinyonya usiku tu siyatakua hayakauki hayo matiti

Unknown said...

Mimi nme muachisha ina enda week xaxa lkn nyonyo lime jaa na halina dalili ya kunywea..lina Norma xana..bint yuko na mwaka na miez 11 nme jitahid thou

Unknown said...

Je kama Mtoto ana miezi kumi Na NNE alafu mama akasafiri kwa siku kumi bila ya kumnyonyesha akirudi unaweza kuendelea kumnyosha Na je kutakuwa Na madhara gani akimnyonyesha?

Unknown said...

ukipata jibu naomba unijibu na mie nataka kujua