Tuesday, 11 October 2016

How to kaza K baada ya Usiku...


...wa Tendo tayari kwa "cha" Asubuhi. Niligusia kuwa baadhi yetu(mie) huwa hatuogi baada ya Tendo Usiku, tunalala nayo ili kuachia "nature" ifanye yake(itoke yenyewe) pia  ili kutunza Utamu si eti! Maana ukikimbilia kuoga unasahau hata kama ulipata!Inategemea na Imani yako, pia inategemea unaichukuliaje Manii. Mie Binafsi Manii sio Uchafu ikiwa mwenye nayo ni Mume wangu. Ikiwa ni Mpita Njia kwamba hamna uhusiano ambao ni  "exclusive na serious" hakika Manii ni Uchafu na kamwe Usikubali yabaki Ukeni which means post hii haikuhusu hihihihi  natania usiondoke mwaya!Sijui kama unajua ila Ukikaa na Manii K-ini unakuwa hatarini kuwa "over relaxed" huko chini hivyo ikifika Asubuhi  hutofurahia Tendo kiviiiiiiiiile! Hata wakati wa kusaka Mimba hunashausiwa kukaa nayo kwa Dakika 5-15 ukiwa umejinua ili kuharakisha prosesi.


Pia ukikaribia kujifungua unashauriwa kucha Manii humo muda mrefu uwezavyo ili kukusaidia wakati wa kujifungua...kwamba Uke hautokuwa Sore sana as Misuli itaongezewa m-relax-isho na Manii.


Sasa tunafanya nini basi ili kurudisha Uke kwenye hali yake ya Kawaida kabla ya Tendo lililopita?

Kama wewe ni msubiri "nature" i-take place(Uume  kujitoa wenyewe Ukeni baada ya kulegea) basi mara tu baada ya kutoka (kama hujapitiwa na usingizi, kwani inategemea na Mkao) ngenda kajiswafi kwa kutumia Maji ya baridi...baada ya kujikausha, fanya kama unataka kuchuchumaa kisha inuka na bana Misuli ya Matako...rudia mara 15-30.Ukirudi Kitandani lala kama ulivyotoka, kwa maana mtupu....sijui Utupu unafanyaje kazi kwenye hili la kurudisha Uke katika hali yake ya kwaida ila trust me ni tofauti kabisa na ukilala na Chupi sijui Pajama. Inabidi wataalam walifanyie hili kazi/Uchunguzi.Najua unaweza kusema "sisi tuna watoto, siwezi kulala Uchi"...kwani kwenu hukupewa Khanga? hihihihi Mwanamke Ghanga Moja, wee baki hapo na U-black American wako sijui U-feminist....upo kwenye Ndoa  Bibi lala mtupu huku pembeni weka Khanga/Mtandio! Watoto wakija  jihifadhi. Nisikuchoshe, jaribu uongeze furaha ya Tendo la Asubuhi.Post ijayo tuone faida za Kufanya Mapenzi Asubuhi(najikomiti eeh)....Nathamini  na kuheshimu Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua blog hii.

Babai.

Monday, 10 October 2016

Mwenza Mshindani/Mpinzani...utamjuaje?Kuna baadhi ya watu wameumbwa/zaliwa kuwa Washindani na hivyo kwao ni kawaida(pia ni vizuri), mara nyingi huliweka hili wazi mwanzoni kabisa mwa Uhusiano. Wakati mwingine wewe mwenyewe unaweza tu kugundua kuwa Mpenzi wako ni Mshindani kwenye shughuli zake za Kibiashara/Kazi, Masomo, Utunzaji wa Pesa, namna anakutunza n.k. Lakini hutofikiria hata siku moja kuwa mkifunga Ndoa hatokubali wewe "umshinde" kwenye jambo lolote.Ukiachilia mbali mtu kuzaliwa hivyo(mshindani) pia Ushindani unaweza kusababishwa na Mazingira, Uzoefu au Malezi. Kwa wale ambao wamezaliwa wachache au wengi (Mtoto wa  Pili, Mtoto wa 3 au 5 kati ya watoto 8-10) au yule wa Pili kutoka Mwisho kati ya watoto zaidi ya 5(hii ni Uzoefu wangu binafsi mie sio Mtaalam).Pengine unaweza usigundue mpaka mtakapokuwa na Watoto, ambao huibia mambo mengi sana kati ya Wewe na Mwenza wako. Kumbuka Watoto huwarudisha nyote wawili kule mlikotokea(utotoni) na hivyo  kutaka kulea wanao kama ulivyolelewa wewe au tofauti na ulivyolelewa ili kuepuka Uzoefu Hasi ulionao Ukubwani....na hapa ndipo "Ushindani"  huibuka. 

 
Sasa utajuaje kama Mume/Mkeowako anakuchukulia wewe  kama Mpinzani/Mshindani wake badala ya Mwenza wake?

1-Ukimnunuliza Zawadi nzuri na Ghali, basi yeye atakununulia Ghali zaidi(Wanawake huwa tunafanya makusudi ili kupata the most expensive....au ni Mimi tu?)


2-Anakukosoa kwanza kabla/balada ya kuuliza kwanini umeamua kufanya jambo fulani. Bila shaka kama Wenza mnashirikiana kwenye kila jammbo lakini kumbuka kuna Mambo mengine hutokea ghafla na hivyo kuhitaji maamuzi ya haraka na hapo kwa hapo, huwezi kumngojea Mwenza aje/apokee/rudishe Simu.


3-Anatumia Maneno ya Umoja zaidi "Mimi", "Niki", "Mwanangu"  n.k....nitakupa Mifano:-
Anapowaonya Watoto..."Mimi Mzazi wako sipendi tabia mbaya badala ya Sisi Wazazi wako hatupendi tabia Mbaya".


"Hii Summer nikienda Likizo na sio Tukienda likizo. Nikimalizia ile Nyumba badala ya Tukimalizia ile Nyumba".

Mkizozana/pishana kuhusu kuadabisha Watoto hasa kama yeye ni Mfokeaji (kwamna anafoka tu hata kwa kosa la Mtoto ambalo linahitaji muongozo wake kama Mzazi)...."huyu ni Mwanangu nitamlea nitakavyo".


4-Ukikosa Nafasi fulani ya Juu Kikazi au Kielimu....haonyeshi kujali sana(anakuwa kama vile kafurahia bila kuonyesha, lakini kwa sababu ni Mwenza wako hakika utajua tu kuwa hajaumia kama ulivyoumia wewe.


5-Akigundua unafanya Jambo fulani vizuri basi hatokusaidia kamwe! ukiomba msaada atakuambia "sipendi kuingilia mambo yako" hihihihi ukweli ni kuwa hataki kufeli halafu wewe ufaulu.


6-Ukija na Wazo zuri la Kimaendeleo ama anakukatisha tamaa  na baadae yeye Kulifanya au anakwambia umwachie yeye afanye Uchunguzi  kwanza....hutopata majibu ya Uchunguzi kuhusu wazo lako bali atakupa Wazo lingine linalofanana na lako.


7-Kwenye Kufanya Mapenzi....unajijua upo Vizuri, lakini hata siku moja hatokusifia. Ila ukimsifia yeye anafurahia huyo halafu hakuambii kuwa kakufanyia hivyo kwa ajili yako....anasema "najua". Nikupe Mfano? napenda Mifano....:-

Sio kila siku unamfanya/mnafanyana vizuri, ila kuna zile siku  unajisikia  upo "Juu" na unataka kuwa "extra" unamuamulia na unauhakika kabisa kafurahia kutokana na Matokeo during na after Tendo....lakini hatokusifia ng'ooo! Ila yeye akikuamulia siku hiyo unampa sifa zake, anakujibu "i know am good" hehehehe. How rude!!Tangu nimemalizia na mambo ya Kufanya Mapenzi basi unaonaje Post ijayo tuangalie namna ya kubana/Kaza Misuli ya  Uke mara baada ya Kufanya Mapenzi Usiku tayari kwa ajili ya cha Asubuhi/Alfajiri. Sie tulio kwenye Ndoa ambao huwa hatuogi baada ya Tendo(kutunza Utamu eee)....si unajua Manii ikikaa Ukeni, Uke unakuwa "over relaxed" au tuseme "over expand(tanuka/panuka)? au hujui?...Usikose basi(Wanawake tu).

Ahsante kwa kuichagua Blog hii, nathamini na kuheshimu muda wako Hapa!

Babai.

Thursday, 6 October 2016

Sio lazima wote tuseme "Nakupenda"......halafu inatumika ovyo sana mpaka imeanza kupoteza Maana kwa Kiswahili(hatuna "like" au hatutaki kutumia kupendezwa) na kwa Kiinglishi. Mtu humjui...ndio kwanza mmekutana, baada ya  kubadilishana Salamu, mnaagana na kuambiana "nakupenda".....wengine mnakutana tu anakuambia "Jamani Dada nakupenda". Hujambo lakini?Pia kuna wale Ndugu...."nawapenda kweli wanangu(yaani wanao)"...akiishi nao masaa 24 lazma abadili usemi wake(au hisia zake). Pamoja na kusem ahivyo bado Uzito wa neno Nakupenda upo palepale....mtu akikuambia hivyo lazima karoho karuke kwa Mshangao au kwa Uoga(kama mna-date)....Kama nilivyoahidi kutoka Post iliyopita (bofya hapa ) leo tukumbushane namna tofauti ya kusema "nakupenda" bila kusema neno hilo.Umewahi kuambiwa nakupenda na Mke/Mume wako ukaangua Kicheko halafu unajiuliza Kasoma Blog gani leo? hihihihihi au ni Mimi tu!! sio kwamba neno hilo linachekesha bali huwa hulisikii  kutoka kwake.


Wapo ambao husema Nakupenda mara kadhaa kwa siku, pia wapo ambao wanasema hivyo wakati wa kufanya Mapenzi tu na wachache husema hivyo siku wakiwa na Furaha au Hatia (wamefanya kosa) etc....sio unafurahia"I love you" kizembe zembe....wengine wanakuwa wametoka kiunoni kwa mwingine na wanakupigia Simu na kukuambia wanakupenda....shauri yako!Leo hapa tukumbushane namna nyingine ambayo Mwenza wako anakuambia anakupenda bila kutamka hilo neno. Inategemea na Wenza husika, namna nitakazokutajia ni za Kiujumla ambazoo wengi wanaweza kuzifanya....mwenza wako anaweza kufanya zaidi kulingana na Uhusiano wenu na jinsi mnavyojuana.


1-Jinsi anavyokufanya, na huwa anafanya Mapenzi zaidi ya Ngono...unajua tofauti si eti?(Mwanaume).

2-Jinsi anavyokuangalia(wote)...hujawahi kaa  mahali na kumuangalia Mumeo/Mkeo na kujisema "hata siamini Miaka yote hii naneng'enuka na huyu Kaka na bado ni Moto"?

3-Namna anakupa "nafasi" mnapokuwa kwenye manunuzi....mf: Halipi mpaka ahakikishe umefurahia na kuridhika(Mwanaume).

4-Anawahi Nyumbani kabla yako na kufanya kila kitu(Mwanamke)

5-Anakuheshimu...Mf: Haleti  Marafiki/Ndugu Nyumbani bila kuhakikisha kama utakuwa okay na Ugeni(Wote).

6-Anakutambulisha kama Mke/Mume na sio Mama/Baba Mama/Watoto(wote).

7-Anakuwa na "kawivu" na anakuambia kuwa alishikwa na Wivu. mf. amekuona kwa mbaali mahali alipokuwa "mapumziko" na akakupigia Simu nakukuambia amekuona sehemu fulani na akirudi nyumbani hali inakuwa si hali...yaani mapenzi Moto Moto(sio kupigana).

8-Wewe ni Rafiki yake, Mshauri wake na mara nyingi anakuambia wazi kabisa kuwa hana Rafiki kama wewe.(Wote)


Ongezea yako basi eti...Post Ijayo tuangalie yule Mwenza  anaekupenda sana lakini anakuchukulia wewe kama "Mpinzani" badala ya "partner"...Usikose!


Ahsante kwa kuichagua Blog hii, kama kawaida  naheshimu na kuthamini Muda wako hapa.

Babai.

Wednesday, 5 October 2016

Nini Mbadala wa kuomba radhi kwa Mwenza?


Kawaida sisi Wanawake huwa tunanuna pale tunapokoseawa tukitegemea kuwa Jamaa anakereka kwa kuchuniwa na hivyo ama kukuuliza tatizo ni nini ili umpe Risala au straight up agundue kosa alilokufanyia na akuombe Msamaha.Wengine hawajali hata ukiwanunia, wanachukulia ni "mambo ya Wanawake" na Baada ya Muda utakuwa "fine". Wengine hata ukiwaambia kuwa umehisi kuwa amekukosea/umiza hisia zako na hivyo ni vema akuombe radhi bado ataendelea kujitetea, matokeo yake Ugomvi unaibuka. Sasa unakabiliana vipi na Mwenza kama huyu?Kama nilivyogusia kwenye Post iliyopita hapa Malezi ya Mwenza wako yanahusika zaidi kwenye suala la kukubali Kosa na kuomba radhi. Baadhi ya Wanawake wapo hivyo pia lakini tofauti ni kuwa baadhi yetu huwa tunapewa Elimu ya Awali ya Maisha ya Ndoa hivyo hata kama Mama na Baba walijisahau au hawakujali kutupa malezi mema bado tutajifunza Ukubwani ili kuwa tayari kuishi na Mtu Baki(Mume).Makosa ninayoyazungumzia hapa ni yale madogo-madogo na yanasameheka. Sizungumzii Usaliti wa Uhusiano(which sio kosa ni Ushetani bin Dhambi)....Usaliti hausameheki unless wewe mwenzangu ni Yesu/Mungu!!Kabla hujaanza kumlaumu hajakuomba msamaha, anza kuchunguza Matendo yake kwako tangu mpishane/gombane. pamoja na kuwa umemnunia/chunia je amefanya nini ndani/nje ya nyumba? Mara nyingi utaona anasafisha vyombo, au anapika....inawezekana akafanya Usafi, kaamka mapema na kuwapa watoto kifungua kinywa? kakununulia kijizawadi na kukiweka mahali bila kukusemasha? Mkilala anakukumbatia(halafu wewe unamsukumia mbali), ana-over-sifia Chakula ulichopika ambacho huwa unapika mara 3 kwa Wiki n.k.Ikiwa hajafanya lolote kama nilivyotaja hapo juu basi ujue kuwa haamini/hajui kuwa alichokisema kwako kimekuumiza hisia na unastahili Radhi yake. Kitu cha kwanza kabisa kufanya ikiwa Mwenza wako sio "kuomba Msamaha" kind of a person, ni wewe kuwa Mfano(kama Mzazi kwa Mtoto). Irudishe Issue mezani na uizungumzie tena.


Omba msamaha kwa kumchunia kwa siku kadhaa, ni kwasababu ya Maumivu aliyokusababishia. Ulimnunia ili kufikisha ujumbe kuwa amekukosea na hivyo akuombe Msamaha(ambao hukuupata), mwambie kuwa kama watu Wazima ni Muhimu sana kuwa Mfano kwa Watoto(kama mnao) kwa kugundua Kosa, kukubali Kosa na kuomba Radhi na kurudisha Uhusiano kwenye hali nzuri ili kuishi kwa Amani na Upendo.


Hakika hatokuambia Nisamehe Mke wangu....akijitahidi sana "atasema nimekuelewa basi yaishe", sio kwamba hataki kukuomba Msamaha isipokuwa hawezi na hajui aanzaje kusema "samahani" ni neno ndogo lakini linauzito mkubwa na ndio maana kwa baadhi ya watu huwa ni gumu kulitoa/sema.


Wanaume wengi (hasa wa Kwetu Barani Afrika)huamini kuwa Kuomba Msamaha ni kama vile kujishusha kwa Mwanamke. anaona bora afanye hivyo kwa vitendo kuliko kutamka neno hilo.


Siku nyingine akikukosea, mueleze hapo kwa hapo na hakikisha ni ana kwa ana. Usifoke na wala usionyeshe Hasira....mwambie ulichokifanya/sema kimeniudhi na kuniumiza hisia zangu, ikiwa kama nimekuumiza wakati nakuelezea naomba unisamehe. Endelea hivyo kila mnapopishana na atajifunza umuhimu wa Kuomba radhi.


Njia nyingne na kumfunza Mwenza wako kuomba Msamaha ni kuwatumia Watoto wakati Baba yao yupo around, wakikoseana waambie waombane Msamaha, wakikukosea waambie wakuombe Msamaha, wakimkosea baba yao watume wakaombe Msamaha/Radhi. Kila mara unawaambia watoto waombe Msamaha/Radhi, waeleze umuhimu wake Maishani, hasa maisha ya ukubwani. Itachukua muda lakini atakugua Umuhimu wa kuomba radhi.


Post ijayo nitagusia Mbadala wa kusema "Nakupenda"....Usikose. nathamini na kueshimu Muda wako hapa, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Thursday, 18 August 2016

Jinsi ya kumfanya Mumeo kuwa kama "Romeo" kwa Juliet.......sio kiviile ila close(I promise)....Jello!

Kama Jojoba ni Hohoba kwanini Hello isiwe Jello?
Ni kawaida kwa wengi kutafuta "namna ya" kupenda, kuridhisha, kuonyesha mapenzi, kujali n.k. Kuna siku Mtu aliniuliza  afanye nini ili Mumewe amuombe radhi? nikashangaa...kuna watu hawajui kuomba Radhi Wenza wao?Hakika hakuna Kanuni kwenye Maisha ya Ndoa  lakini kuna yale mambo "basic" ambayo ni lazima kila mtu ayajue na kuyafanya/tenda. Mambo hayo huwa tunafunzwa tukiwa angali wadogo, tukianza Shule na kuendelea kuona Wazazi na watu wetu wa karibu wakiyatenda/fanya . Bila kusahau kutukumbusha pale tunaposahau kuyafuata/tenda/fanya. Ndio maana siku zote huwa nasema kuwa Mwenza ulienae hivi sasa ni Matokeo ya Malezi/Makuzi yake  bila kusahau Mazingira aliyokulia. Kiongozi kwenye Malezi hayo mambo huwa ni Mama (au Msaidizi mwenye Values kama wewe au bora Zaidi) kwavile ndio huwa anakaa na Mtoto kwa muda mrefu kuliko Baba.Sasa pamoja na kuwa wengi wetu  hutegemea/dhania kuwa Kila Mwanaume ni lazima awe "loving" kama "Romeo" kwa Juliet, kwamba anakuambia anakipenda mara kadhaa kwa siku kwa aina tofauti ya Maneno, mkiwa mtaani anapachika Mkono kiunoni, anakupandisha garini kabla yeye hajapanda, anakubusu mara kibao kwa siku, anafanya Ngono Kiromansi mara zote mnapohitajiana...Romeo huyo hakulelewa kwenye Mazingira yale yale aliyolelewa Mumeo. Romeo ni yeye na Mumeo ni Mumeo.Suala muhimu hapo ni kwako wewe kumjua  vema Mumeo kabla hajawa Mumeo, vilevile ni kwako wewe kuwa wazi kwake(usi-settle for less ila usiende overboard)....kama kuna mambo hawezi/hajui kuyafanya na sio muhimu sana kwako basi achana nayo. Mf;- Kutolewa nje kwa jili ya Mlo, Yeye kuosha Vyombo, Kukuimbia, kusema "honey i am hooooome" hihihihi. Kuna yale muhimu/basic ambayo ni lazima ajifunze kuyafanya hata kama hawezi,  nayo ni Heshima, Ukweli, Thamini, Shukurani na Kuomba Msamaha/radhi. Ikiwa Mumeo kabla hajawa Mumeo na hujamuweka sawa kwenye hayo basi Ndoa yako itakuwa Chungu...utahisi kuwa Ndoa yenu ni ya Mtu mmoja na utakuwa Mpweke Ndoani. Utahisi kumpenda Mumeo lakini hutopendezwa nae Siku 305 kati ya zile 365 za Mwaka!....je unaweza kuishi na Mtu anaekuudhi kwa Muda huo wote wa Maisha yako?Sie wa "kizamani" tulifundwa kuwa Mke anaweza kuchukua nafasi ya "Mama" kwenye kumuweka sawa Mumewe, ila sasa unapomfunza Mumeo yale muhimu ambayo Mama yake  labda hakutilia maanani hupaswi kuwa kama Mama yake kweli na yeye kuwa Mtoto  wako bali unapaswa kufikisha "Somo" kivingine ukijitumia wewe kama mwenye hitaji la "tabia njema" kutoka kwake Mumeo Mpenzi.Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa Wanaume hawafanyi mambo yale yale ambayo wewe unadhani ndio Kupendwa na  kwamba kila Mwanamke  anapata "Tamu" ya "Romeo" kwa Juliet. Kuna Wanaume ni Wapenzi wazuri sana lakini hawajui kusema "Nakupenda" kila siku, hawajui kusema "samahani/nisamehe" kila wanapokukosea, hawajui kuwa Romantiki.....wana namna zao tofauti-tofauti za kufikisha ujumbe kuwa wanakupenda, wanaomba msamaha na kuromantika.Siwajui Wanaume wote Duniani ila "I lived" hihihihi so nitakupa Uzoefu wangu. Tafadhali usikose kunitembelea tena ili ujue ni namna gani hasa baadhi ya Wanaume hufikisha ujumbe uleule wa kiRomeo bila kuwa kama Romeo.


Nathamini na kuheshimu Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Thursday, 11 August 2016

Kukabiliana na Mwenza/Mpenzi "mpya" baada ya Miaka kadhaa...


....kwa maana ya yeye kubadilika/shwa na "Rafiki" zake kama niliyogusia Post iliyopita, ikiwa hukuisoma basi bonyeza hapa. Upo salama lakini?....twenzetu!


Kwanza kabisa usimwambie kuwa umebadilika, lakini akikujia na mambo mapya ambayo awali hakuwa akipenda/fuatlia then hoji kulikoni? mf: tangu lini Mpenzi unatazama Eastenders? Hee siku hizi unafuatilia hiki/kile? hii itamfanya atambue kuwa unaona mabadiliko.Pili, Jiweke mbali, yaani mbaaaaaali na hao/huyo "Rafiki" unaedhani ana/amembadilisha Mwenza/Mpenzi wako. Usimuulizie, akianza kukupa stori bila kutaja jina la Mhusika, wewe sema tu "tunamzungumzia John"(taja jina la huyo rafikie mpya)? Halafu onyesha kuwa huna "interest" ya kujua zaidi.(hii itafikisha ujumbe na hivyo kuacha stori za huyo mtu/watu).Tatu, Ataanza kutaka kukutanisha wewe na huyo "Rafiki" kwa kisingizio chochote tu, kuanzia "ametualika kama familia" au "anataka kuja kututembelea ili awaone watoto/apajue Nyumbani". Weka Mguu chini na mtolee Nje kwa upendo na upole kwa kumwambia kuwa Mpenzi/Mume wangu....vyovyote unavyomuita. Ashura ni Rafiki yako, mmekutana Kazini na nafurahi umejenga urafiki na mtu Mahali pa  Kazi. Ila ni vema kama ukitenganisha Maisha yako ya Kazini na ya Nyumbani.Hapa lazma atabisha kwasababu atakuwa tayari kaongea na kumhakikishia "Rafiki" yake kuwa atakwenda  na Familia/Mke/Mume wake, sasa ili asimuangushe ni wazi atakubishia na hata kuonyesha Ukali na kukufanya ujisikie kuwa hupendi watu, atasema hakuelewi, atasema umebadilika na mengineyo basi tu kukuuudhi ili umkubali. Usi-panick. Tabasamu na Mwambie haupo Comfy  kukutana na Mtu wa Kazini kwake amjue yeye Mumeo/Mkeo/Mpenzi wako huko na sasa amjue Nyumbani pia.Ongeza kwa kusisitiza (ukiwa firm bila kufoka) kwamba  huyo ni Rafiki yake yeye na sio Rafiki wa Familia yenu hivyo basi ni muhimu ya Kazini yabaki huko na ya Nyumbani yabaki Hapa(nyumbani). Kama ni muhimu sana na hutaki kumuangusha rafiki yako, basi nenda mwenyewe. Mimi na Watoto(kama mnao) hatuhusiki na urafiki wako wa Kikazi.Nne, Mwambie mwenza wako kuwa ni vizuri kutengeneza Marafiki lakini ni vema zaidi ikiwa mtatengeneza marafiki kama Pea nje ya Kazi, kwamba muwe na Marafiki wapya ambao hamkukutana Kazini. kwasababu kuwa na Rafiki anaekujua Kikazi, Kisosho na Kifamilia/Nyumbani ni Hatari na ni Mwanzo wa kutengeneza Adui.Kumbuka, wapo watu wanatafuta Marafiki ili kujenga Uadui  mahali pa Kazi. Utendaji ni Ushindani. Kupata kazi na Kubaki kwenye kazi na hatimaye Kupanda Cheo kunahitaji Ushindani. Ushindani huo unaweza ukawa Mzuri kabisa na ulio-base kwenye utendaji na Bidii yako, lakini pia wapo ambao hupenda njia za Mkato.
Sasa unapoanza Kazi mpya, unakuwa "vulnerable" na hivyo  "maadui" huchukua nafasi hiyo ili waje kukumaliza kirahisi huko baadae. Sikutumi kuwa usijenge marafiki kwa kuhofia wao kuwa Maadui baadae, isipokuwa nasema kuwa ni muhimu Rafiki wa kzini wabaki huko na Nyumbani wawe wengine. Ikitokea Kazini kumebuma, angalau Nyumbani kutakuwa Salama....kwamba  hamtowavuruga Watoto na hakutakuwa na "Mama mbona hatuendi tena kwa akina Peter"?  "Mama naomba kumpigia Simu  Antie Rose". Vilevile Adui hatokuwa na lolote alijualo kuhusu Nyumbani kwako na kulitumia ili kukumaliza zaidi.


Nadhamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Thursday, 28 July 2016

Pale Mwenza wako anapobadilishwa tabia na "Rafiki"...


...Mara nyingi watu husema au kuamini kuwa Mtu anapopata Pesa au Kazi mpya inayolipa Vizuri kuliko kazi yake ya Awali huwa anabadilika(nadhani niliwahi kuzungumzia kwanini watu huwa hivyo mwaka jana/juzi). Habari? natumai Uumzima wa Afya.Nirahisi kutodhani kuwa Mtu Mzima hawezi kuwa "influenced" na Mtu au Watu wapya wanaomzunguuka....kwasababu amepita Umri wa miaka 30...lakini kihalisia bado wapo Watu Wazima ambao wamekua Miili tu na Namba zimeongezeka lakini Akili zao bado ni za Kitoto. Bado wanapata hitaji la  kutaka kufanana, ku-fit in, kuwa kama yule/huyu,kukubalika n.k.


Inasemekana hali hiyo  hutokana na Ukosefu fulani wa "attention" kutoka kwa Walezi/Wazazi kipindi ambacho Mhusika alikuwa chini ya Miaka 10. Kumbuka matokeo ya Malezi  tuliyopata kutoka kwa Wazazi/Walezi wetu  huwa yanaathiri maamuzi (mabaya/mazuri) na Maisha yetu ukubwani. Mtu anahitaji kitu kidogo tu ku-triger alichokosa Utotoni. Achana na hili.Sasa kwa baadhi mabadiliko huwa Wazi  mara tu wanapoanza "Shughuli mpya" hivyo ni rahisi kumuweka Mwenzio sawa na hivyo unakuwa umemsaidia kugundua "mapungufu" yake ambayo yanaathiri Uhusiano/Ndoa yenu.Wakati mwingine inakuwa ngumu kugundua tofauti (hasa kwa Wanawake) kutokana na  Uchovu wa Shughuli zisizoisha za Nyumbani na Malezi ya watoto. Uchovu huo unaweza kukufanya ujishtukie na hata kujibebesha mzigo wa Lawama kuwa wewe ndio sababu ya mabadiliko ya Mwenza wako.Utakuwa na bahati sana ikiwa Mwaka umepita tangu apate Kazi Mpya/Cheo/Mshahara Mzuri na Mwenza wako hajakutamkia kuwa "umebadilika sana", Jirekebishe, "Humueshimu", "hukuwa hivi siku za nyuma" bla-bla-bla. Sasa leo nitakupa au kukusaidia kuweza kugundua kuwa Mwenza wako aliepata Kazi Mpya au kupanda Cheo na Mwenye Mshahara Mzuri sio yule uliemjua tangu apate kazi Mpya au kupandishwa Cheo.


1)-Ukilalamika kuwa "leo umechoka", yeye atakuambia umefanya nini siku nzima? badala ya kukupa pole na ku-offer msaada au Massage. Kana kwamba shughuli uliyonayo sio muhimu na haichoshi kama yake. Hivyo ni yeye tu ndio anapaswa kuchoka. Na siku akilalama kachoka basi atategemea umfanyie kila kitu kama Binti/Bwana Mfalme.


2)-Anakuwa Mkosoaji kwenye kila jambo unalofanya/taka kufanya au anatoa Jibu ambalo sio "Possitive" kabla hujamaliza kusema/uliza ulichotaka kusema/uliza.


3)-Anapokuwa na siku za Mapumziko anatumia Muda wake huo kuongea na Rafiki zake badala ya kukusaidia vijishughuli viwli vitatu vya Malezi ya Watoto wenu(kama mnao). Kucheza na watoto sio Malezi...tambua hilo.


4)-Kila mnapofanya mazungumzo kuhusu Familia yenu lazima atachomeka Jina la Mtu wake ambe ndiye anam-influence na familia yake. Utasikia "hata fulani hivi, alifanya vile, anafanya hivi" n.k.


5)-Ukihitaji afanye/toe Uamuzi wa kufanya jambo fulani Muhimu kwa Familia yenu basi ataambia Usubiri/umuachie yeye kwanza afanye uchunguzi(anaenda kuwakilisha kwa Mtu wake anaem-influence).


6)-Akipatwa na Tatizo mbali na Nyumbani mtu wa kwanza kujua ni yule anaem-influence na sio Watu wa Msaada au Polisi na wewe Mke/Mume mtu ndio sahau...utasimuliwa tu.


7)-Zile Simu za Mara x2 kuangalia Watoto wameshindaje hazipigwi tena, Muda wote unamalizwa na huyo mtu wake anaem-influence.


Je! Ufanye nini ikiwa umegundua kuwa Mumeo/Mkeo "amebadilika" kutokanana kuwa-influenced na Mtu  baada ya kupata Kazi Mpya/Pandishwa Cheo? Usikose Post Ijayo.


Nathanimi na kuheshimu muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Wednesday, 27 July 2016

Mtindo 1-10 with a twist....(requested)!!


Mwenye Kwao haachi Jadi si eti? Sasa wewe(na wenzako) "mmepitilizishwa" na Umarekani sijui Usasa bin Usawa mnasahau mpaka Jadi zenu na Maana yake...sio mnasahau bali humzijui na hivyo unakurupuka tu na kusema "Kutoa Mahali ni sawa na Kuuzwa/Nunuliwa"....Hujambo lakini?Sasa ni hivi; kuna mitindo Mingi sana na kumfurahisha Mwenza wako wa Kiume kunako Faragha, kama ujuavyo mwaka 2008 niliandika Topic ya Mtindo wa 1-10 na ikiwa hujui basi endelea kusoma ili uweze kujiongezea au kujifunza "kaujuzi".Mtindo wa  "Moja mpaka Kumi" unafanyika katika Mkao wa Kifo cha Mende Mwanamke juu, Ukishakuwa tayari Bibie weka Mzigo ndani na uingie mpaka Mwisho kisha ujilaze sambamba na Mwili wa Mwenza wako ambae ni Mwanaume(nitatumia Mkibaba kuokoa Muda).Wakati upo kwenye Mkao huo tumia Misuli yako ya Uke kubana na kuachia a.k.a "Piga endiketa", baada ya hapo njoo juu na rudi chini(piga takoz hihihihi) mara Kumi....kwamba kila ukienda chini ndio unahesabu Moja...endelea mpaka Kumi bila makeke na bila kupumzika ili usisahau Hesabu.Ukishafika Kumi, rudi juu bila kutoka kabisa, baki pale Kichwani na tumia misuli yako ya Uke kubana na kuachia alafu nenda tena Chini.Juu na sasa hesabu Mpaka 9...rudi juu "tease Kichwa"....rudi chini.Juu tena Mara Nane...cheza na kichwa....nenda Chini-juu Mara Saba....mpaka ufike utakapo fika au Mkibaba kufika Kileleni, kwa maana kwamba sio rahisi kufikia Moja kutokana na wewe au yeye kushindwa kujizuia na "kucheka" katikati ya mahesabu.Siku nyingine fanya Mtindo 1-10 "with a Twist"

Mkao ni kama nilivyoelezea hapo juu ila sasa badala ya kwenda Chini-Juu moja kwa moja, unaongeza Kiuno, kwamba ukifika Chini(Uume Umejaa ndani)..katakiuno (cha kitandani sio chakucheza Singeli) taratibu huku unarudi juu....nenda tena Chini kwa mara ya Pili na wakati wa kurudi juu zunguusha Kiuno tena...rudia mpaka mmoja wenu atakapofika au  mtakapofika kwa pamoja.


Kama una swali lolote kuhusu Post hii, basi  usisite wala kuogopa kuniuliza. Nathamini na kuheshimu Muda wako mahali hapa na Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Monday, 11 July 2016

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo.


Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani.


Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake).


Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao Wasenge wenyewe. Kwa huku nimesoma nao, nimefanya nao kazi na kuishi nao(sio nyumba Moja)..........wait,Stori Time:  wakati nipo "Foronda" actually nilisoma na mmoja akiitwa "Faruku" kwa Utani....alikuwa akivaa Kaptura fupii na za kubana, pia anafungua vifungo 3 vya juu vya Shati lake hehehehe  wakati Wenzake wakivaa Pensi(zinafika Magotini na pana kiasi) na Mashati ya kawaida ya Shule. Daily alikuwa akichapwa kwa kutovaa Sare sahihi mpaka wakamzoea!Sasa wapo walioamua kuendele kuwa "Wasenge" kwasababu ya Mazoea, kwamba walikuwa-abused kwa muda mrefu walipokuwa wadogo.  Vilevile kuna wale wanaamua kugeuka/kugeuza ili kujikimu(lifestyle), Wengine hutokea tu (naturally) kuwa wanavutiwa na Jinsia kama zao..iwe kuingiliwa au kuingilia au vyote.Nisiwasahau wale ambao hujikuta wanapenda kuwa kama Wanawake/Wanaume au wanaamini kuwa wao ni Wanawake/Wanaume ila wameumbwa na maumbile yasio sahihi na mwisho kabisa tunao wale Wanaume wanaopenda kujiremba na kuvaa kama Wanawake.


Msenge sio Lazima avae na kuongea kama Mwanamke au kujiremba, hata Mumeo na Misuli yake anaevaa Kiume anaweza kuwa Msenge pia. Kumbuka Usenge kwa Wanaume sio Kuingiliwa tu bali hata kumuingilia Mwanaume mwenzio ni Usenge....nyie mnaita Basha!! Pia Wasenge wengi hawana Gender roles kwenye mahusiano yao.Kwahiyo sasa Msenge au Wasenge hawawaibii Wanaume/Wapenzi wenu, bali Wanaume wenu ni Wasenge to begin with.....hali na uwezo wa kusimamisha mbele ya Mwanaume Mwenzio, kuingia, kufanya na kumaliza....huo ni Usenge 100% ila unajificha kwenye Ubasha kibongo-bongo. Basha ni Msenge, Mumeo sio Basha wala Bisexual...Mumeo/Mpenzi wako ni Msenge full stop!! Usijipe moyo...ooh tumezaa, ooh anasimamisha daily. Nani alikuambia Wasenge hawasimamishi?Wasenge wa Mjini hawaibi Wanaume, isipokuwa ninyi Wanawake hamjui kuwa  Wanaume wenu ni Wasenge.....kumbuka Wasenge wanawajua Wasenge wenzao ambao bado hawajitambua(wamejificha kwenye kivli cha Ubasha) au wanajitambua ila kutokana na aibu wanaamua kufunga ndoa na kuwa na familia kama Jamii inavyotaka. Lakini huko nje huitwa maBasha ambapo wengi hudhani kuwa ni "sifa" na inakupa "muonekano" wa kuwa Mwanaume wa "kweli" na pengine kuogopwa Mtaani kwasababu unainamisha/pindisha Wanaume wenzio. Lakini kihalisia wao ni Wasenge/mashoga pia.Ushoga Tanzania haujaanza leo, nani anamakumbuka Shoga Maarufu aitwae Farook ambae alikuwa mcheza Ngoma Asilia maarufu pale Zanzibar(nilisimuliwa na Marehemu Bibi)....Mtu kuwa Ushoga/Usenge sio  Kosa Kisheria, isipokuwa kufanya Mapenzi kinyume na Jinsia (kulawiti) ndio Kosa, sasa iwe unaingiliwa na Mumeo huko Tigoni au Mwanaume anaingilia wanaume wenzie ni Kosa kisheria.Kutokujua kunakufanya kuwa Muoga, kuhofiwa kuibiwa Bwana/Mume.....ukijifunza kuhusu hii Jamii utaelewa na hakika hautokuwa Muoga na kamwe hautojenga Chuki dhidi ya hawa watu. Utawachukulia kama walivyo na maisha yataendelea kwa amani kabisa.


Nathamini muda wako hapa na ahsante kwa kuichagua blog hii.

Babai

Monday, 20 June 2016

Kufanya Mapenzi(Ngono) Hakujengi Ndoa yenye Furaha......


....lakini ni "Madhara" ya Ndoa yenye Furaha! Nimekuchanganya si eti? hata mie sielewe nilichoanza kuandika ila endelea kusoma na mimi niendelee kuandika na kwa pamoja tunakuwa kwenye Mstari na hivyo sote kuelewa. Hujambo lakini?Ngono au Kufanya Mapenzi(kama tunavyopenda kuita sie tulio Ndoani ili kuhisi "Utakatifu" wa Ndoa zetu) sio Muhimu kiviiiiiile, Muhimu ni kutunza au kuendelea kuwa na  ile hali ya kuvutia/vutiwa na Mwenza wako. Kwamba, sasa ni Miaka 8 ya Ndoa yenu lakini bado unapata misisimko uleule uliokuwa ukiupata pale anaposema "kesho nakuja"....tofauti sasa unajua anarudi saa ngapi nyumbani kwenu....Sauku ya kumuona inakupa tabasamu kuu.Wakati mwingine Unajiambia/jisemea ni jinsi gani unampenda Mume/Mkeo bila yeye kukusikia. Wakati mwingine wala huamini kuwa unaishi na Mwenza umpendae hivi(japo huwa anakuudhi na unamnunia)....Ukimuona Mkibaba unahisi "kunyetukanyetuka" na yeye akisikia sauti yako  Mkimama basi tena hana Hali. True Story!! turudi kwenye Topic......Ngono (Kufanya Mapenzi) ni Madhara ya Ndoa yenye furaha.....unajua, kila kitu kina Faida na Madhara yake si ndio? Sasa faida za Ndoa zipo nyingi lakini Ngono(kufanya Mapenzi) sio moja wapo. Kufanya Ngono(Mapenzi) ni Madhara ya kuwa na Ndoa yenye furaha. (Hiki kipengere kimejirudia....Usijali, kuandika na kueleweka sio kazi rahisi kama udhaniavyo)!


Kwamba, ni lazima Madhara hayo yakupate ikiwa Ndoa yako imesimama Imara na imejawa/egemea Upendo, Furaha na yale yote Mema mlioelekezwa, funzwa, jifunza n.k. Pamoja na kusema hivyo bado Ngono(kufanya Mapenzi) haipaswi kufanywa Kila siku. Ikifanyika kila siku inapoteza "Mngaro"? hihihihi mnapoteza "ubunifu" a.k.a mnaishiwa!..........ndio hiyo inatoka kwangu Mie yule wa Enzi pale Dinahicious, ambae nilikuwa nawashanga sana Watu wanalala vipi Kitanda kimoja bila kupandana kila siku angalau Mara 3. Achana na hili. Mnapokuwa kwenye Ndoa mambo mengi hutokea, kumbuka mmeunganisha Familia mbili tofauti. Kila familia hukutwa na issues zake ambazo huwahusisha ninyi pia kwa pamoja. Kwamba likija kutoka kwenu ni lake  na likija kutoka kwa Mumeo pia ni lako. Ukiachilia hayo kuna Malezi ya Watoto na Majukumu Mengine kibao ya Kimaisha.Sasa mnapoishiwa "Mngaro" au Ubunifu ni wazi kuwa mtakuwa na kazi ya ziada ya kutafuta mambo Mapya ambayo katika hali halisi ni yale yale tu sema hamjayafanya kwa muda Mrefu, but Muda wa kufikiria on how to actually do it tena unagharimu kwani tayari Masaa 24  yapo full....ni kama vile hayatoshi.Hivyo ni Muhimu kufurahi pamoja bila kukutanisha Miili nakufanya Mapenzi Daily(mara 3-4 kwa Wiki inatosha), kama bado au  ulikuwa hujui basi jaribu kujifunza  kuwa karibu nae:-

1)-kuonyesha Mapenzi kwa Vitendo popote mlipo bila kuingiliana, Busu, shika/gusa kwa Huba, Mahaba yaani kuwa "Intimate".

2)-Kiroho-kujadili Imani yenu/zenu na Kusali pamoja.

3)- Kiakili-Kufanya Mazungumzo ambayo hayahusiani na Watoto/Kazi/Ndugu.

4)-Ongezea as you go.....Mpaka umefika hapa ni matumaini yangu kuwa umenielewa au tumeelewana. Kama bado basi usisite kuni-Tweet nami nitafanya Blog Post ingine Spesho kwa ajili yako.


Nathamini Muda wako mahali hapa na Ahsante sana kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Sunday, 19 June 2016

Toto Baya, Zuri kwa Mama(au a face only Mother can Love)....

...sio kila Mtoto huzaliwa Mzuri, na karibu Watoto wote (hasa wanaozaliwa Kiasilia) hutoka wamevimba-vimba kama Kiazi Mviringo. Wale ambao huchelewa kutoka au Wale ambao Mama zao hujizuia wasiwazae(sukuma) Garini/Chooni ndio huwa Balaa(wanatisha hihihihi)! Mtoto anatoka, wanakukabishi u-bond nae lakini wewe unamrudisha chap-chap kwa Daktari/Mkunga kisha unaanza kulia. Ile kulia baada ya Kukamatishwa Mtoto ile huwa ina Siri zake, sio furaha tu!Kibibi soon after Birth....0 Day old!Wanangu wote walipozaliwa nili-share Picha zao za Masaa Machache tangu kuzaliwa, sikuonyesha Miguu wala Mikono kwa kisingizio cha "Privacy" zao, nilikuwa Aware Wanangu wamevimba-vimba ila ile hali ya Kujivunia mimi kuwa Mama ndio ilinisukuma ku-share Pics za awali kabisa tangu wazaliwe.....Privacy wakiwa wamevimba-vimba alafu wanapoteza "Privacy" wakifikisha Miezi Kadhaa? Sema tu ukweli tu kuwa katoto kako kabaya  hihihihihihi and it's okay! it's Nature!!
Babuu alipozaliwa alitokea poa tu, hakuwa Kavimba wala nini hehehehe ila Kibibi sasa....eeeh alitokea kama "Small Potato" sijui Homono?...kwa kawaida inamchukua Mtoto Siku 3-28 "kunyooka", kuwa kawaida(Chunguza zile Sherehe Asilia za Saba na Arobaini ya Mtoto kwa undani utaelewa kwanini)...Saba Mtoto anatoka kushikwa na Wanafamilia, Arobaini anatoka Nje rasmi na tayari kukutana na Shida za Mtaa/Dunia.

Kibibi 3Months oldKwa Ughaibuni ya England ni tofauti, Watu tunaenda Shopping day 5(actully sio Shoppng ni Check ups)....wengine Manguli wajitoa same Day. Ile katoka Hospitali tu unamkuta Coffee Shop (Ruksa kushangaa na kucheka)!Mara nyingi mtu anapata Hatia kusema "katoto kako kabaya", anaishia tu kusema "awww she/he so cute",,,sasa ukisema hivyo na wakati Mie Mama mtu najua Kichanga wangu kavimba-vimba nitakukata jicho ambalo litakufanya ubadilishe Sentensi yako kutoka "she/he is Cute" to "she/he looks like you both" which sio rahisi....nani anafanana na Wazazi wake wote? Zaa uyajue na kwambia!Safari apitiayo Mtoto ndani ya yale Masaa Machache ya Uchungu kuanza kushtua mpaka unapochanganya, Maji kumwagika na wewe Kuanza Kusukuma ni ngumu....achilia mbali "stress" unazompa pale unaposema umechoka au huwezi tena kusukuma!! Hivyo usitegemee Mtoto kuzaliwa "Mzuri".Suala muhimu ni kwa Mtoto kuzaliwa Salama na mwenye Afya, Pia wewe Mzazi kumaliza safari hiyo salama(kuzaa is Next to Death). Suala la "Uzuri" wake litajulikana huko mbele na ata-deal nalo mwenyewe bila Msaada wako.


Ahsante kwa Kuichagua blog hii, Nathamini Muda wako hapa.

Babai.

Thursday, 2 June 2016

How to(Jinsi ya) kumheshimu Mumeo...


...muendelezo wa Post ya jana, kama hujaiona bofya hapa. Najua ungependa kujua namna ya kumheshimu Mumeo zaidi badala ya kuwa Chini yake si eti? Kama ujuavyo sote tumepetia Mazingira/Malezi/Makuzi tofauti na hivyo hatufanani Kitabia, hivyo basi Kuheshimu Mume nijuavyo mie huenda ni tofauti na ujuavyo wewe.,...sasa labda chukua ambalo ulikuwa hulijui na ongezea kwenye yale uyajuayo? au acha kama yalivyo ila ukiweza share yako na mie "niangalizie".Kumbuka Heshima ni muhimu kwa pande zote mbili lakini leo tunaegemea kwa Mwanaume kwasababu mimi ni eerrrr Mwanamke? also Topic ilikuwa Mwanamke kuwa Chini ya Mwanaume? Sasa kama tumeelewana hapo, twenzetu;Muachie maamuzi Makubwa-Hata kama Kipato chako ni Kikubwa mara Nane kuliko chake, Sio unajiamulia tu kununua Nyumba au kupeleka Watoto Private School kwa mfano..... kwasababu tu unaweza. Mpe Mumeo nafasi na mjadiliane. Unaweza kuweka Mezani aina/sehemu 3 za Shule/Nyumba na kisha muache yeye afanye Uamuzi wa Mwisho kisha mpe-support. Baadhi ya Wanaume ni wazito kwenye Utendaji na kuna namna ya kukabiliana na hili,  ila sio kufanya maamuzi Makubwa kisha unampa ripoti ya nini ulichofanya.Salamu-Kwasababu tu mmelala pamoja na hukuhisi akigalauka Usiku haina maana alilala vizuri na kumbuka usiku ni Mrefu...pia hamkuwa wote Ndotoni. Kama mlivyokuwa enzi zile kabla hamjafunga Ndoa eeeh! umeamkae leo mpenzi....well sio lazima useme hivyo, Mambo?, Umeamke? Upo okay? etc! Pia katikati ya siku akiwa kwenye mishughuliko yake na atakapowasili Nyumbani.
Shukuru-Pamoja na Usawa wenu bado Mwanaume huwa na Presha kubwa ya kulinda na kutunza Familia yake. Onyesha shukurani kwake kwa yote afanyao kama "mwanaume". Kushukuru hapa kupo kwa aina tofauti sio lazima useme "ahsante Mume wangu kwa kuwa mwanaume wa nguvu/kweli" bali unaweza kusema zaidi kwa vitendo(nitaandika Post inayojitegemea kwenye hili...nikumbushe au vipi?).Pia ni muhimu kumshukuru kwa lolote analokufanyia hata kama ni dogo, Mfano kaamka leo na kasafisha vyombo....mwambie ahsante. pengine kawahi kuamka na kuwaandalia watoto Kifungua kinywa lakini kaenda tofauti na utaratibu uliowawekea watoto na hivyo kuharibu utaratibu wa siku nzima.....mshukuru tu hivyo hivyo.....hihihihihi!Jijali/Jipende/Jirembe-Sijui wale  "napenda Nachuro" nafasi yao ipo wapi Mbinguni? ila ni muhimu sana kujipendezesha na kuonyesha kuwa unajijali kwa ajili ya Mumeo. Ikiwa wote ni Wafanyakazi  nje ya Nyumbani basi Mkimama jitahidi kuwa unawahi nyumbani mapema kabla yake ili upate muda wa "kujiweka sawa" kwa ajili yake. Kupendeza kwako  sio tu kutakufanya ujisikie Vizuri kama Mwanamke pia ni wazi kuwa kutaonekana kwa Watu wengine na hivyo Mumeo kuonekana kuwa anajua kutunza Mkewe.....hii kwa baadhi ni Heshima kwao!Uliza kabla ya Kukosoa-Hasa kama Mnawatoto au Mnabiashara pamoja  au vyote. Kuna sababu kwanini kafanya alichokifanya hivyo basi kabla ya kuanza kumkosoa ni vema kuuliza kwa upole kwanini kitu fulani kimefanyika ili upate kuelewa na hivyo kutafuta ufumbuzi kwa pamoja. Epuka kukosoa-kosoa mara kwa mara!Usimseme vibaya/Mshushua-Mbele ya rafiki zenu, kuna wakati Mumeo anaweza kuteleza/lopoka mbele ya Rafiki zenu kwenye Party au mkusanyiko wowote.....lolote lililomtoka muunge mkono  na kuwa upande wake(bila kusema neno). ikiwezekana kuwa sharp ku-justfy (muokoe kutoka kwenye kujiabisha).....mkifika nyumbani ndio umuweke sawa. usimuweke sawa mbele ya watu wengine no matter how close you are with those watu.Usilalamike au kunong'ona-Kama kuna kitu Kikubwa kafanya hakijakupendeza, tafuta muda weka issue Mezani muijadili kwa upole na Upendo. Vitu vidogo vidogo kama vile Kunya/Kojoa pembeni ya choo(yes some Mumes still do that), kutosafisha bafu baada ya kuoga au kutoweka kitu mahali pake...sio kwamba anafanya hivi kwa sababu wewe ni "kazi ya Mwanamke" bali hivi vitu sio Muhimu kiviile kwake(inategemea na Malezi). So rekebisha na move on au mwambie moja kwa moja ili aache habits hizo.Mhusishe kwenye  Utaratibu wa Siku wa Watoto-Mama ndio huwa Mstari wa  mbele kuweka Sheria, Kuweka Ratiba, Kuweka utaratibu n.k. katika harakati za Malezi na kurahisisha Maisha, mara nyingi Baba huwa Kazini akifanya yake ya Kibaba ili kuweza kutunza familia yake. Hivyo kupitwa na yote uliyoyaweka ambayo wewe na Watoto mnayafuata ili kurahisisha Maisha ya kila siku ni rahisi.  sasa ni muhimu kumhusisha Baba ili ajue yote yanayoendelea. Sio mara zote atapatia lakini itakuwa rahisi kumuweka sawa ikiwa tayari ulikwisha muelezea utararibu wa siku wa watoto. Wakati mwingine watoto watamwambia "Mama hafanyi hivyo, Baba umekosea"!!Muandalie Chakula aka "umtengee" mara nyingi,  natambua kuna zile siku ambazo unakuwa hoi na yeye anaelewa kuwa umejichokea na hivyo anaingia mwenyewe Jikoni na Kujipakulia. lakini jitahidi kuweka chakula tayari kwa ajili yake.


Usikivu-Mumeo anapozungumzia issue muhimu  ya kifamilia (hata kama mwanafamilia wake humpendi) au pengine adha alizokutana nazo Kazini, msikilize kwa makini bila kumkatisha au kuonyesha kuwa haupo inteested.Usimuingilie kwenye Muda wake na Watoto-Hii ni ngumu(nakwambia kama Mama), lakini ni lazima ujifunze kutoingilia afanyacho Mumeo  kwa Watoto wenu so long  hakihatarishi Maisha yao Kihisia au Kisaikolojia...maana some Babaz nao huwaga wapuuzi, hupenda kuogopwa rather than kuheshimuwa na watoto. wanadhani ni sifa!


Uelevu kwenye "Hadithi" zake- Inaweza kuwa Siasa, Uchumi n.k....chochote ambacho kinam-interest. Jitahidi kumuelewa na ikitokea huelewi  mahali ni vema kuuliza kabla hajaendelea ili arudie tena kuliko kujifanya umeelewa halafu uulize tena mbeleni wakati alichokuwa akikielezea kimekaribia Mwisho....hii hukatisha tamaa na kuonyesha kwamba ulikuwa hausikilizi na hivyo  kuua "stimu" ya Hadithi.
Omba Ushauri na wake-Ikiwa kunajambo ungependa kulifanya na huna uhakika, kabla ya kuomba ushaurii kwa shoga zako au Mama/ndugu zako....Muombe yeye kwanza!
Epuka kulimbikiza Makosa ili Kumsuta- Mwanaume kama Mwanaume, usipoliweka wazi Kosa lake linapojitokeza basi ndio imetoka hiyo....ama hajui kama amekukosea au anasahau. Sasa  ukitokea Mzozo na wewe ukayaingiza yote hayo kwake inakuwa kama vile unamsuta kwa Makosa ambayo hayajui(yapo kichwani mwako).
Usiingilie Ugomvi wake- Kabla Era ya Sosho Midia haijajulikana wengine hapa tulifundwa kuwa tusiingilie Ugomvi kati ya Mume na Ndugu zake, na badala yake kuwa "sikio" na usikilize....akiomba ushuari basi shauri kwa makini na hakikisha ushauri wako haukandamizi upande wa Pili ambao ni Ndugu zake. Kuwa upande wake lakini pia kuwa Fair, kwani hao ni Ndugu na wewe ni Mwanamke tu(Ouch)!!


Sasa Era hii watu na wake zao wanafuatana humo Sosho Midiani, time to time Mume anaweza kupishana na Mtu/watu.....ikawa ngumu kwako kama Mke kushuhudia Mumeo akiwekwa Konani. Jitahidi usiingilie, mwache amalize Ugomvi wake mwenyewe!Kwa leo wacha niishie hapa, Tambua nathamini Muda wako hapa na Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai!

Wednesday, 1 June 2016

How to(Jinsi ya)...kuwa Chini ya "Mumeo"....


....imekuwa kawaida kwa Wanandoa Wake kwa Wame kutafuta "jinsi ya" kufanya mambo mbali mbali ili kuifanya Ndoa kusimama Imara na kuepusha misuko-suko ya kihisia na hivyo kupelekea Ndoa kuwa Ndoano na pengine kuharibika.


Hii kuwa "chini ya Mumeo" hata mie siijui na vyovyote ilivyo kamwe sitokubali kuwa "Chini" ya  Mtu yeyote achilia mbali Mwanaume ila nitakuambia ninachokijua ambacho huenda ni tofauti lakini bado kinamrudishia Mwanaume hali ya kujihisi/sikia kuwa anaheshimika/heshimiwa na Mkwe.Tatizo kubwa linalofanya Wanawake kukumbushwa au lazimishwa na Jamii kuwa ni LAZIMA wawe chini ya Wanaume (asiwe na Sauti) pale wanapoamua kufunga Ndoa ni kutokana na Imani kuwa Mwanamke anaposimama na "kujitetea" na/au kum-challenge Mwanaume basi huesabika kuwa hana Adabu, hana Heshima kwa Mwanaume husika.
Ukweli ni kuwa unapokuwa kwenye Ndoa ya "ndio Bwana"  kwamba kila anachokisema Mwanaume wewe unakubali tu....huondoa Changamoto na hivyo kufanya Ndoa kuwa a bit "boring" na ni wazi kuwa hautofurahia Ndoa hiyo kwa sababu hautokuwa na Sauti,...Ndoa inaendeshwa na Mtu mmoja, kwamba kuna maamuzi yatakuwa yakifanywa na Mumeo ambayo wewe hupendezwi nayo lakini kwa sababu ya "Uoga" aka kuwa Chini yake ambako wewe unadhani ni "heshima" unaendelea kuwepo humo.
Ikiwa unatoa "Heshima" huku unahasira au  Moyo/Roho inakuuma ujue hiyo sio Heshima bali ni "Uoga" ambao ukiendelea utakusababishia Matatizo ya Kiakili na Kisaikolojia(bila wewe mwenyewe kujua), utaishi kwenye Ndoa kwa sababu ya kufurahisha Jamii/Famili/Ukoo na sio kwa ajili yako na Mumeo na pengine Watoto kama mtaajiliwa.Huenda ukawa unamalizia "machungu" yako kwa...labda Msaidizi wako,Marafiki zako au Watoto. Unaweza kuwa mwenye hasira kwa watu wengine ambao hawahusiki.....unatoa Sauti/unakuwa juu huko kwasababu huwezi kufanya hivyo kwa Mumeo. Hivyo unaumiza watu wengine wasio na hatia kwa Upumbavu wako wa kuwa Chini ya Mumeo kama sehemu ya Kumheshimu!!
Ndoa ni Muungano wa Watu Wawili, Wewe na Mumeo. Msingi wa Ndoa yenu unatakiwa kuwa-based na kuendelea kujengwa na pande zote....baadhi ya Mafunzo kutoka kwenye Imani za Dini yamepitwa na Wakati, ni vema kutumia Common Sense rather than kufuata "Mafunzo" ambayo ni Radical na zimeegemea kwenye Mfumo Dume zaidi na kutokana na Maisha yalivyo sasa ni kama vile baadhi hazileti maana? Kwamba tunakabiliana na changamoto tofauti na zile za Miaka 2000BC.
Sasa Heshima kwa Mwanaume ndio sababu kuu/pekee ambayo husababisha Wanawake waambiwe/lazimishwe kuwa Chini ya Mwanaume. Kama nilivyokusia hapo juu, Kuheshimiwa kwa Mwanaume  ni Muhimu sana kama ilivyo kwetu Wanawake kwenye kujaaliwa,kulindwa na kupendwa (kuwa cherished).Nnachojaribu kusema hapa ni kuwa, huitaji kuwa Chini ya Mwanaume! akifanya ujinga muweke sawa ila sio kwa Kumfokea bali kuwa-firm.....kwamba aone kuwa unachosema hutanii na  hutaki mchezo...upo very serious.


Chagua Maneno ya kutumia, ikiwa unahitaji muda kufikiria, jipe muda na tafuta nafasi uwakilishe Issue inayokusumbua. Ikitokea kitu na kinahitaji mabishano basi Bishana kwa heshima bila kutoka nje ya Mstari wa Heshima na kutumia maneno machafu/kashfa..Mara nyingi Wanaume huchukia ikiwa wewe Mwanamke unaonekana "smarter" kwenye Mambishano yenu na ili kukunyamazisha hukimbilia kutumia Kashfa au maneno machafu yatakayokuumiza hisia, sasa hata kama yeye atayatumia bado huitaji kumrudishia hapo kwa hapo. Ugomvi ukiisha/poa muelezee hisia zako za kutokupendezwa na matumizi ya maneno Machafu/Mabaya/Matusi.Kuwa Chini ya Mtu yeyote sio rahisi, achilia mbali Mumeo, mie binafsi siwezi na sitokaa niweze na Yaye Mume wangu analijua hilo....sitaki/sipendi ujinga(naturally mie ni Mkali), nina hoji kwenye kila jambo/kila kitu ambacho kinagusa Familia yetu na hasa Watoto wetu....nadhani hii ni kutokana na sehemu ya "career" niliyopitia? sijui!!Ndoa ni Kazi ya kila Dakika, Kila saa na Kila Siku, ukiwa mvivu basi utakimbilia "mwanamke lazma awe chini ya Mumewe"....acha Uvivu, do your Job! Kama huna Muda wa kufanyia kazi basi usifunge Ndoa....Ndoa haihitaji wavivu.


Usikose Post ijayo ya "Jinsi" ya kuonyesha Heshima kwa Mumeo. Nathamini na Kuheshimu Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai!

Saturday, 28 May 2016

Kubishana/Fokeana Mbele ya Watoto...


....kuna Ubaya?
Baadhi ya watu wanasema SIO vema kwa Watoto wenu kuwaona mkigombana iwe ni Ugomvi Mkubwa(Pesa za Savings acc zimenda wapi?) au ule mdogo(kwa makusudi hujasafisha Bafu). Nyie huwa hamgombani? Kama hamgombani basi mmoja wenu anaishi "kisiri", ulie nae sio yeye...au mmoja wenu anamuogopa mwenzie.Mie ni that Woman ambae nina Sauti kali/ya juu which is a shame kwasababu huwezi kujua kama ninafoka au ninaongea kawaida, sasa ukitaka kuongea kama mimi ni wazi kuwa Utakuwa unanifokea kitu ambacho kitanikera na hapo moto kuwaka...umeona? hihihihihi nataia!!
Wazazi wengi hujizuia  kuanzisha "Mabishano" mapema na hivyo, husubiri mpaka Watoto watakapokwenda Kulala ndio wanaanza kubisha/fokeana. Nakumbuka wakati nakua Baba na Mama walikuwa wakifokeana Chumbani kwao(wakiamini tumelala) kumbe some of us (Mie) tulikuwa tunaenda kusimama Mlangoni na kuwasikilia ili tujue kama wanabishana/gombana au wanaongea kawaida tu na kama wanagombana, wanagombania nini?....haiwezekani iwe ni mimi tu? hehehehe.
Wakifungua Mlango ghafla najifanya nilikuwa naenda Chooni, nimepotea njia....Sikuwahi kuwaona Wazazi wangu wakifokeana/bishana/gombana mbele yetu, lakini najua kuwa walikuwa wanafokeana time to time.Unapokuwa na Watoto(Mzazi), wakati mwingine inakuwa ngumu "kugombana" na kumaliza Ugomvi kwasababu watoto wanaingilia (huyu anakuja nakuambia anaaka Maziwa, mwingine  hivi na vile)na hivyo kuharibu "ugomvi" na matokeao yake "issue" inabaki inaning'inia. Hii ni moja ya sababu ya Wazazi wengi kusubiri mpaka Watoto walale ndio "wagombane" kwa "uhuru".
Sasa, inasemekana/Aminika kuwa ni vizuri Watoto wakijifunza "real life" kutoka kwa Wazazi wao na hivyo inashauriwa kuwa ni Salama kwa Watoto kuona Baba na Mama wakibishana/gombana kwa Maneno(bila kutumia matusi), kupena nafasi ya kila mmoja wenu kujieleza ili kwa pamoja kufikia Muafaka na kumaliza tofauti zenu zilizosababisha mkwaruzane.Pamoja na kugombana huko hakikisheni kuwa hamdhalilishani kwa kuitana majina Mabaya/Machafu au kutumia Matusi, Watoto ni kama Sponji.....wanachokisikia na kukiona kutoka kwa Wazazi (watu wa kwanza kuwaona, kuwapenda na kuwaamini) "hukinyonya" na kukitunza. Kwao itakuwa ni kawaida kwa sababu Baba na Mama hufanya hivyo pia!Mambo vipi lakini?

Tambua kuwa Nathamini sana Muda wako hapa, Mwambie na Mwenzio. Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Friday, 27 May 2016

Je ni Muhimu kurafikiana na Rafiki wa Mumeo/Mpenzio....

...just incase? Mie binafsi siwapendi Rafiki zake wote...well sio wote, wapo  ninaowapenda ila Asali wa Moyo hayupo karibu nao so nimebaki na nisio wapenda which means siwapendi WOTE!! anyway...Siku nkaenda shiriki Semina ya Wanandoa Wachanga(mie mepita Miaka Saba so nilienda kama Mzoefu). Dunia ya leo watu wanadanganyana sana aisee. Mke wa Pastor aliedumu kwenye Ndoa kwa Miaka 28, akawa anashauri Wanawake walio Ndoani ambao hawana "uzoefu".Mengi yalisemwa ila lililonigusa ni hili la LAZIMA na MUHIMU sana kuwa karibu na Rafiki wa Mumeo, just incase siku moja mkikorofishana na wewe ukashindwa kuongea moja kwa moja na Mumeo. Kwamba unaenda kwa Rafiki yake/zake na kuwaomba wamfikishie ujumbe....au "Ongea na mwenzio, maana mimi hanielewi" Kweli Mama Pasta? kweli kabisaa??
Huyu ni Mume wangu(najisema kimyomoyo Seminani), tulipokula Kiapo ilikuwa kati yake Yeye, Mimi na Mungu  na tuna-share kila kitu(isipokuwa Miswaki na DNA?) ikiwa kuna issue kati yetu Mama Pasta tunaiweka Issue Mezani, tunazungumza na kufikia muafaka wenyewe na Mungu wetu. Ndoa ni ya Watatu Mama Pasta, Mungu, Mume na Mke, ikitushinda tunaipeleka kwa alietufungisha ndoa, akishindwa(which is rare) basi tunarudi Nyumbani kwa Wazazi.....huko nako ikitokea Sufuri basi tutajaribu Kansela ambae ni Mtaalam na hatujui sote(hatopendelea)....duh! mpaka tufike huko Ndoa itakuwa imekwisha uwawa...mie Mwenyewe Mshauri hihihihihihi!
Hakuna Uhusiano usio yumba, sema miyumbisho inatofautiana. Jambo kubwa kwenye Ndoa yetu huenda ni dogo sana kwenye Ndoa ya Watu wengine. Mfano mie sipendi kutukanwa au kudharauliwa, sasa siku Asali wa Moyo akinitukana au kuonyesha dharau huo utakuwa Mwanzo wa Mwisho wa Ndoa yetu! hii haina Kansela wala Mfungisha ndoa....Kuvumilia? vumilia wewe....mie sijui kuvumilia matusi wala dharau.
Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa, huitaji na sio lazima kurafikiana na Rafiki wa Mumeo/Mkeo ili tu iwe rahisi ikitokea mmepishana/kosana/gombana na mwenzio. Kama ilivyo kwenye Mapenzi, Urafiki/Ukaribu na Mtu  haulazimishwi....ni ku-click au unclick!Kwa wewe ambae hukufundwa na Bibi/Shangazi yako labda (Kama Somo la Sayansikimu, sio muhimu ila inasaidia sana Maishani) na unategemea/amini zaidi Wake wa Mapasta/Wachungaji wakushauri kutokana na "umri mkubwa" wa Ndoa zao. Tambua kuwa Umri wa Ndoa sio kielelezo cha Ndoa Imara yenye Furaha, Upendo na Amani. Wengi hubaki kwenye Ndoa kwa sababu nyingine nyingi tu ambazo hazihusiani na Maana wala Lengo la Ndoa.Pia kumbuka kuwa Uzoefu wa Mtu sio mara zote muhimu bali Elimu. Kufundwa ilikuwa ni Elimu  ya Kijadi ya Awali ya kumuandaa Binti Kimaisha(sio kingono pekee kana wengi wanavyofanya siku hizi) atakapokwenda kuwa Mke na Mama.Sijui nyie, lakini jinsi mnavyokuwa pamoja kwenye Ndoa ndivyo ambavyo mnajifunza zaidi kuhusu  mambo mengi kimaisha kama Pea, vilevile inafikiwa mahali mnajikuta hamuendani tena na "marafiki" zenu wa zamani ambao kila mtu "alikuja nao". Mara nyingi mnaachana na baadhi as you grow older na kutengeneza Marafiki Wapya kama Mke na Mume by the time umefikia utu Uzima mnajikuta na Marafiki wa kweli wa chache na wengi wao ni wale mliotengeneza Pamoja kama Wanandoa.
Sikutumi uwafukuze rafiki wa Mumeo ambao labda (kama mie) huwapendi, bali husihisi presha ya kujenga urafiki nao, ila ni muhimu Mumeo aelewe kuwa Humpendi fulani na fulani ili ikiwezekana apunguze kuwaleta kwenu.....you know some watu wana bad energy, ukiwaona tu energy yako na yake zina-crush(weka Smile Emoji)!!"Waheshimu Ndugu na Rafiki wa Mumeo, lakini usirafikiane nao"-Marehemu Bibi yangu Binti Z.K.Waulize Google for me, kwanini hatuna Emojis kwenye Blog via PC ambayo ni Google Product?

Babai.

Monday, 23 May 2016

Faida za Kumnunia Mwenza wako....

...Habariyo?


Wanawake tunajulikana kuwa tunapenda  sana kununa-nuna si eti? Lakini hata Wanaume pia hununa, ila wao huwa hawaiti "kununa" bali "nataka kuwa peke yangu ili nifikirie" au pengine anaweza kukuambia hajisikiii vizuri au anamawazo.


Sote tumetofautiana, jambo dogo kwako linaweza kuwa kubwa sana kwangu, hali kadhalika kauli yako ambayo wewe unadhani ni ya kawaida inaweza kuwa Tusi kuu kwa mwenzio na hata kuhatarisha Ndoa/Uhusiano wenu. Inategemea na Malezi/Makuzi, Mazingira, Uzoefu n.k.Wakati mwingine Kununa is all you need! Biga Mnuno kwa Siku 5(ukizidisha Mkeo/Mumeo ataku-cheat hihihihihi siku ya 6 kidate na ya Saba one night stand....Hisabati Muhimu).....the rule(Bibi yangu alisema), nuna  Maximum Siku Tano tu ukizidisha huna Mume/Mke!Kununa huko hupunguza ukaribu kati yenu kama Mke na Mume, unapokea majibu kwa mkato, ukiingia tu ndani, mmoja anahisi usingizi  ghafla hihihihihi....pia hukupa hisia ya "nampenda" lakini sipendezwi nae...ananiuDhiiii( ndio love___ but don't like___?)....Kizungu sijui, Kiswahili sijui....nipo nipo tu sijui kama naenda au narudi....anyway!Kununa kwako huwa hakuna faida(Machoni mwao) lakini huwa kuna sababu ya Msingi tu kwanini hasa Mkeo/Mumeo kakununia. Unajua unapokuwa kwenye "Ngazi" ya Urafiki na mapenzi ni rahisi kupata nafasi ya "kufikiria" Tusi au kosa/kwazo alilokufanyia Rafikio wa Kiume/Kike....so hata ukinuna utakuwa kwenu na yeye Kwao.Lakini unapokuwa kwenye Ndoa na Mnaishi kwenye "Kanyumba"....Nafasi hiyo hupotea, huwezi kuikimbia Nyumba yako kila mara ambapo Mumeo/Mkeo wako anakuudhi! Mbaya zaidi ikiwa wewe kama Mie hapa, unaishi Ughaibuni....hakuna "kwenu" kule alipo Mama yako ambako ungeweza kwenda na kupumzika kidogo ili kufikiria mpaka Hasira ziishe(Uache kununa) hivyo unaishia kupishana na Mwenza wako bila Jambo wa Habari.Kwa kawaida, Mnapopishana Maneno na kupelekea Mabishano  na labda mmoja wenu hatoi nafasi ya mwingine kujieleza, ili kukunyamazisha....anatupia "tusi" na Maneno mabaya ambayo pengine yataumiza Hisia zako.....Maumivu hayo hukufanya uamini kuwa Mumeo/Mkeo atagundua kuwa amekukwaza/kosea na hivyo atakuomba Msamaha.
Siku inakaribia kuisha na hakuna Msamaha wala Dalili yake.....kinachofuta hapo ni "Kula Bati"....yaani unamnunia....akiwahi kulala wewe una-stay late watching Tv, aki-stay late wewe unaenda kusoma Kitabu. Hakuna kula pamoja wala kupika(kwa Mwanamke kupika ni sehemu ya kupendezwa na mwenza, kama hakupendezi kwa maudhi yake kwanini Umpikie eti?) kwa Wanaume huja na chakula chao au hula Nje(kwanini ale chakula chako wakati hujamuomba msamaha).Sasa kuna watu wameumbwa kusoma wenza wao na kugundua kuwa wamekosea mahali, wengine huuliza "nimekukosea nini Mpenzi, mbona unaonekana haupo sawa" na wengine huwa hawana habari mpaka uwaambie makosa yako(kama vile wewe ni Mzazi kwao). Wengi hasa Wanaume hawajui au niseme Wazito kuomba Msamaha? au Wanaomba Msamaha kwa vitendo?


Haombi msamaha mpaka umwambie amekukosea wapi, which inaondoa uzito wa Msamaha wake.....kwasababu Msamaha mzuri ni ule unaotoka kumoyo bila kulazimishwa au kuambiwa sio ndio?!!Nukta ya Post hii ni hivii.....unapomnunia mwenzio kwasababu amekuudhi sio Utoto na wala sio Ujinga. Ni sehemu muhimu kwako ili kuweza kutuliza Akili na Hisia zako zilizoumia  na kufikiria Kosa(kauli yake chafu iliyo kukwanza) na hivyo kuwakilisha issue Mezani tena katika hali ya Upole lakini Firm.


Fundisha Mwanao umuhimu wa Kuomba radhi/Msamaha, na ikiwa wewe Mzazi umemkosea mwanao usisite kumuomba msamaha, kwani "tufanyayo kwa Vitendo ndio hufanywa/igwa  na Watoto wetu"-Christian Bwaya.


Shukurani kwa Muda wako hapa ambao nauthamini pia Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Baibai.

Tuesday, 3 May 2016

Kurekebisha/Komesha Tabia online, inawezekana?

Habariyo!

Mengi kama sio karibu yote siku hizi yanawezekana Online, lakini kurekebisha Tabia ya mtu au watu Online? mie Mshamba hivyo sidhani kama inawezekama. Huwezi kumfunza mtu tabia njema ikiwa hakufunzwa hivyo na Wazazi/Walezi wake! Utakachokifanya ni kufanya watu wakuogope au Waogope kuwa karibu na wewe (unless ufiche Utambulisho wako).Inaaminika kuwa ni vigumu sana kwa Mtu kubadilika Kitabia akisha vuka Umri wa Miaka 25, atajaribu "kuacha" tabia yake ikiwa tu  kaamua iwe hivyo na kuna mtu wa karibu yake pembeni anamsaidia, lakini "msaidizi" akiondoka maishani mwake basi Mhusika hurudia tabia yake/zake Mbaya.Vilevile, ikiwa Mhusika mwenye Tabia mbaya amejenga Familia na Mtu ambae ana-support au kuelewa au samehe tabia yake mbaya, basi ugumu wa mhusika kubadilika huongezeka, kwasababu ana "support system"kutoka kwa Mke/Mumewe ambae ni Muhimu kuliko watu wengine wote wa online included.Kitambo hivi, kuna jamaa Walipatwa na Msiba. Sasa jamaa walikuwa wakiishi kivyao-vyao(hawana habari)na hawakujichanganya na Watz wenzao huko waliko Ughaibuni. Inasemekana walikuwa hawashiriki "Sosho events" za watu soooo walipofikwa na hiyo "life situation". Watu wakaamua kuwafunza "adabu Online".
Mie nilipoambiwa nikawashangaa watoa Adabu. Kwanini mtumie Maumivu ya watu kuwadhalilisha.....sawa nyie ni Watz zaidi yao(Wafiwa wanaishi Kizungu) basi toeni Adabu kiTz, Kijadi. Unakumbuka Utani Msibani? yep watu bado wanafanya haya na tulipofiwa na Mzee(Baba RIP) watani walitutania na kumuigiza marehemu Baba, baadhi unacheka na mengine yanakuongezea Uchungu zaidi.Watani hutumiwa Misibani kufikisha Ujumbe/Funzo/Tia Adabu  "live" uliochanganyikana na Utani, sasa kama alietangulia alikuwa wa kujidai-Pua juu ndio mtajuzwa siku hiyo, Kutokana na Utu Washiriki watakuja Msibai lakini watafanya kwa "utani" vile ambavyo ulikuwa ukifanya kwenye matukio kama hayo kwa wenzako na mwisho kususia "Shughuli" ili kuwafunza  Adabu Waliobaki. Baada ya tukuio kupita utaanza kuona Wanafamilia wakianza "kubadilika" na kuanza kushiriki Matukio ya Kimaisha ya Jamii inayowazunguuka.Hili haliwezi kuhamishiwa Online, unachokifanya Online ni kuiaibisha Familia ya mwenzio kwa kisingizio cha Kufunza tabia. Asilimia 99.9 wahusika hawatosoma/ona na wengi watakaosoma sio wahusika uliowakusudia. Kwa maana nyingine wale uliowakusudia wataendelea na "Uzungu wao" kama kawaida.Mie binafsi sio Mtu ninaependa Mikusanyiko lakini huwa nashiriki kwenye Matukio ambayo nahisi kuwa ni Muhimu kama vile Msiba au Michango kwa ajili kusaidia Matibabu. Kwenye sherehe-sherehe hunikuti.


Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa ni sawa kabisa  kujitenga(kutokuwa mtu wa mikusanyiko) lakini mtu unaemfahamu anapopatwa na Shida ni vema kutafuta muda na kushiriki. Natambua maisha ya Ughaibuni yanabana sana linapokuja suala la Muda(nafasi), Ugumu huongezeka mnapokuwa na Watoto.Lakini ni muhimu kujigawa, hii ita-sound kizungu pia hihihihihihi tupo Uzunguni babu wee hehehehe. Kama ambavyo tunajigawa kwenye maswala mengine ya kimaisha kama vile bills, shopping....mjigawe, nani atakuwa anawakilisha Familia kwenye "life situation" kwenye jamii inayokuzunguuka iwe ni ya Wabongo wenzako au mchanganyiko.


Wakati mwingine sio rahisi kuwepo "live" kwenye tukio kutokana na Umbali wa Jimbo to Jimbo, Mkoa toMkoa, kwa UK ni Nchi na Nchi, basi tumia Simu eeh, shiriki ki-Digital.


Nashukuru na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Monday, 2 May 2016

Juice na Soda husababisha "Homa" zisizoisha kwa Watoto....


Heri ya Mwezi mpya wa May. Mungu abariki kila jema upangalo kufanya(na-sound kama Pastor sasa eti?)!


Umewahi kujiuliza kwanini Mwanao/Wanao huwa na Homa au Vikohozi visivyokwisha? Ukimpeleka Hospitali na kupima Damu na kila kitu majibu ni kuwa hana Malaria wala Typhoid (hatuna huku ila inawezekana ulipo haya Magonjwa yapo) na magonjwa Mengine ya Utotoni. Wahenga...well Bibi yangu alisema "Mwanangu kuwa Uyaone", mie nasema kuwa na Watoto ujifunze!

Wazazi wengi huamini kuwa Soda  husababisha  Watoto kuchangamka kupita kiasi na pengine kukosa usingizi, baadhi huamini kuwa hufanya Watoto kuwa na tabia za ajabu(wabishi,wakahidi, hawakusikilizi, wananguvu kupita kiasi) kutokana na Soda ambayo huwafanya kuwa "high". Sasa hizo ni Soda na zina some sort of "hewa" sio, kwamaana hivyo Juice za kawaida ambazo hazina Sukari ni salama(nilidhani) tena zile ambazo unachanganya na Maji(squash) ndio Bora zaidi(nilijidanganya).
Kuna wakati tulikuwa tukinunua aina Juice ya Matunda"asilia"bila kuongezewa Sukari, maalum kwa Watoto. Matokeo yake (bilakujua) Babuu akawa na Homa zisizokwisha, yaani karibu kila siku Anachemka. Siku moja tulipoenda "Manunuzini" ile Juice haikuwepo in Stock hivyo tukanunua Brand nyingine ambayo ilisema kuwa ni  jutoka kwenye Matunda Halisi aka "Natural" hakuna addictives. Babuu hakuwa na Homa tena. Ziporudi  zile zilizokuwa out of stock tukanunua tele(maana alikuwa akizipenda), Homa zikarudi, hapo ndio nikagundua kuwa Zile Juice zina kitu ambacho sio Salama!Kama Kacha(kawaida, Utamaduni) nikaenda Gugo, na kuuliza sababu ya juice "husika" kusababisha Mtoto kuchemka/Homa. Nikakutana na "Aspartame" ambayo ni Sweetner wanayoweka kwenye Juice kuongeza Utamu badala ya kutumia Sukari ya Kawaida. Na huu ndio ukawa Mwazo wa mimi kuwa "Mlevi"wa Kusoma Ingredient(Vitu walivyotumia kutengeneza Bidhaa husika). Natumia muda mwingi kusoma "ingredient" zaidi ya kulinganisha Bei.Nia ya Post hii ni kukupa mwanga kuwa sio Soda tu zinazoweza kufanya Mtoto "achangamke" sana hata zile Juice laini zinazosema "no Sugar added" zinamadhara kwa Watoto kwa namna tofauti. Mwanangu Homa(naturally ni very active), Wengine wanakuwa too High/Over activeBaada ya Muda nikaja gundua lingine, Mwanangu Hapatani(Allergic) na Karanga au anything Nuts....kuwa na Watoto ujifunze eeh! Tulipiga sana Misele kwa Dermatologist nikaja kugundua Mwenyewe kuwa tatizo ni Karanga(nilizila sana nilipokuwa Mjamzito) na Ngozi yake ni Sensitive na hivyo haitaji Hash Soaps,Lotion etc....hii ni Topic ingine(nikumbushe nikusimulie na nikuambie tunatumia nini ku-keep ngozi safi na yenye afya, no miwasho wala ukavu).


Pamoja na kusema hivyo, usitumie Post hii kama Ushauri wa Daktari, Ikiwa Mwanaoa anaugua Homa mara kwa  mara nenda kwa Daktari kwa Ushauri wa kitibabu na Vipimo/Tiba. Lakini pia ondoa vinjwaji ambavyo sio "Asilia".


Unaweza kutengeneza Juice mwenyewe kutokana kwenye Tunda Fresh. Natambua kuwa kila tulacho siku hizi kina Kemikali(sio natural), lakini mpaka sasa hakuna Issue kiafya inayotokana na Maji ya Matunda kutoka Tunda asilia.


Ahsante sana kwa kuichagua Blog hii, tambua kuwa na heshimu na kuthamini Muda wako hapa!

Babai.

Wednesday, 6 April 2016

Jipe Changamoto Deilee....

Mambo?
Kama ni mfuatiliaji(mshiriki) kwenye mambo mbali mbali yanayoendelea Online iwe ni kutoa Misada kusaidia wengine, kuhamasisha juu ya Afya, kuelimisha wengine kuhusu issue mbali mbali za Kijamii na hata yale ambayo ni Binafsi.Utagundua kuwa hayo niliyoyataja hapo juu huwaunganisha watu wote na kuwa kitu kimoja kwenye Suala husika linalofanyika kwa Wiki/Siku husika, Pamoja na kuungana huko bado hutokea kutofautiana na kutokana na "utoto" wa baadhi basi kufarakana hujitokeza na hivyo kufanya baadhi kutengwa, semwa vibaya  hali inayopeleka wengi kuogopa au kukwepa "kushiriki" kwenye hayo mambo ambayo baade hutumika kusuta wengine.....hukufanya hivi tulivyo fanya vile, halafu leo kimbelembele....si unajua?Sasa ikiwa wewe ni kama mimi(sio mtu wa Drama) na hupendi kujionyesha au hutaki watu wakujuuuuuuue, yeah naandika mengi kuhusu mimi (Kila kitu Mie...got it?)lakini bado hunijui amini nakuambia hihihihihi. Anyway kama wewe upo kama Mie utakuwa na ile tabia ya kujipa Changamoto kivyako kwa faida ya watu wengine.Changaoto za kujipa zipo Nyingi kuanzia kuchangia Ujenzi wa Choo Kijijini kwenu, Kuajiri Vijana kadhaa Wakati wa Kilimo, Kuchimba Kisima, Kusomesha Sekondari Watoto wa Fukara kila baada ya Miaka 4 n.k. Ili kukamilisha hili hutumii Savings bali unajitahidi ku-cut back matumizi yako ili kufanikisha Changamoto uliojiwekea.Ukiachilia Mbali hilo, kuna zile Changamoto za kila Mwaka/Mwezi/Wiki ambazo ni za kibinafsi zaidi, na mimi nimeamua kujipa Changamoto ya Mwaka ya kutonunua Tope(Foundation) mpaka nilizonazo ziishe(namna ya kuzimaliza pia ni changamoto ndani ya Changamoto ambayo naifanya weekly).
Pamoja na kuwa tayari nina Changamoto inaendelea nikaona sio mbaya "nikisafisha" Mwili na nikajipa Changamoto ya kukata/ondoa Chumvi kwenye Chakula nilacho kwa Mwezi wote wa Rent, Nilipofanikiwa nikaamua kujipa Changamoto  mpya ya kunywa Maji Mengi kwa Wiki moja ili niweze kufanya unywaji wa Maji kuwa Habit. Kawaida nilikuwa nakunywa 60ml kwa siku, hii ni kutokana na hali ya hewa na unywaji mwingi wa Chai.Leo namaliza Wiki Moja tangu nianze kunywa Maji 1200ml kwa siku, safari haikuwa rahisi na siku ya Tatu nikaongeza na hivyo nikanywa 3000ml nadhani Mwili ulishtuka na hivyo nikaumwa sana Kichwa(too much water i guess). Siku kata tamaa nikaendelea na 1200mil zangu. Unatakiwa kunywa maji kulingana na Uzito wa Wili wako, kamuone Daktari wako au Kaguge au Pakua App, weka Kilo zako na app itakuambia unatakiwa kunywa mil ngapi kwa Siku ili kuepuka Kifo, yep Majini ni Uhai lakini too  much yachukua Uhai(kifo).Nilikuwa nakunywa vipi?

Najua unatambua kuwa hupaswi kunywa Maji hayo kwa mkupuo kwani utakuwa bloted na hata kusababisha matatizo mengine ya Kiafya ikiwa ni kuvimba Ubongo, hii ni kutokana na Maji kuwa zaidi kwenye Damu kuliko Chumvi na Sodium. Pia hupaswi kunywa Maji peke yake kwa wiki kwasababu unapata vimiminika vingine kutoka kwenye Chakula na Matunda bila kusahau Chai.-Nikiamka  tu 6am-Nakunywa 600mil(bila kusafisha Kinywa....heei)
-Dakika 30 kabla ya kifungua kinywa namimina 150ml
-Baada ya kifungua Kinywa namimina 150mil
-Dakika 30 kabla ya Mlo wa mchana nachukua 150mil
-Dakika 30 kabla ya Mlo wa jioni 150mil


Natumai Post hii imekupa mwangaza kiasi kuhusu faida ya kujipa Changamoto  mwenyewe, Unaweza kujiunga na watu wengine kwa support online ila mie ni Loner na Control freak, i am much happier when I do things  my way and all alone.Shukurani kwa kuichagua Blog hii, naeshimu na kuthamini Muda wako hapa.
Babai.

Monday, 4 April 2016

Wanaume hawajui kunung'unika/kukaa na Kinyongo....


....Sosho Midia si imewabadilisha? Hakika bado wapo hivyo ila namna wafanyavyo ni tofauti na walivyokuwa wakifanya kabla ya Sosho Midia(nionavyo mimi).Unakumbuka ulipokuwa mdogo(au ni mimi tu), Baba yako akisikia jambo kutoka kwa Mwanaume mwenzie halizungumzii ila anakwenda kwa huyo Mtu na kuzichapa/kumkung'uka Magumi? well Baba yangu alikuwa mtu Mwema na Mtu wa watu lakini alikuwa Ngumi Mkononi, anakutandika halafu yanaisha. sasa hii ndio "Wanaume hawakai na Kingongo" niijuayo mie. Niliendelea kuona hiyo  kwa Kaka zangu na rafiki zao pia na hivyo kuweka Sementi kwenye hilo.
Siku hizi Waanaume, wanaanika mambo ya wenzao nje (mitandaoni)ikiwa wamekorofishana, kwamba mmoja akiudhiwa/kasirishwa na mwenzie basi Jamaa wa Shosho Midia wote watajua. Kwa sisi Wanawake ambao hufikiria baada ya action(sio kabla) na kisha kuomba msamaha baada ya kuharibu ni Kawaida(ilizoeleka hivyo), lakini sio kwa Wanaume.
Sio kwamba  nasikitika kuwa Wanaume wamebadilika na wala sisemi wakarushiane Magumi, bali nasema Unapotoa Siri ya Mwenzio  adharani kama sehemu ya "kutokukaa na Kinyongo" haikusaidii in a long run, kwasababu  unajitia aibu wewe mwenyewe na kuondoa Imani/Heshima kutoka kwa watu wengine(sio muhimu lakini can be muhimu huko mbele)na baadhi kukuogopa kwenye Issue zao za kimaendeleo labda....?Aibu hiyo husambaa kwa Familia yako ikiwa una Mke na Watoto, Mpenzi.....ikiwa Wewe ni single kwa mfano, inakuwa kama vile unakimbiza  potensho Mpenzi. Inawezekana bado unaamini kuwa hizi Sosho Midia ni Apps tu, lakini kumbuka kwa karne hii ni sehemu ya Maisha. Picha zako na short vid zipo kwenye "www", mtu akikuona Mtani au popote "wachumba" wanapopatikana sio ngumu (kama unavyodhania) kutokukutambua/kumbuka upuuzi wako Online.Mie Binafsi nafanya  karibu kila kitu Online kuanzia manunuzi yangu, na-chat na watu nsiowajua juu ya bidhaa fulani, naweka mihadi na Daktri online, Na-book holiday online, nafanya kazi online,.....so online is "part of life".....huwezi kuendelea kufanya mambo ya kudhalilisha mwenzio (hata kama kakukosea) ukijitetea kuwa ni online so sio that serious!
Mie sio Mama yako so sitokufundisha Manners ambazo Mama yako labda alishindwa au alisahau au pengine Baba hakuwa na Muda na kukuweka sawa namna Wanaume wanamaliza "tofauti" zao. Ila nitakuambia kuwa, ni vema na ni Uanaume(whatever Uanaume is).....kumuita aliekukosea na kuzungumzia Issue iliyokukwaza na kuyamaliza pmbeni.
Ikiwa aliekukosea ni wa Online, kwa kawaida kila Sosho Midia ina mahali faragha, basi na muitane huko yaishe. Huu sio ushauri bali ni maoni yangu kuhusu sehemu ya  tabia za Wanaume tulizozizoea kubadilika kutokana na ukuaji wa Maisha ya Online.


Nathamini, muda wako hapa na ahsante kwa kuichagua blog hii.

Babai

Saturday, 26 March 2016

Mango Vs Red Bull.....Boost Kitandani kwa busy mama wasio na Wasaidizi!


Sio mpenzi wa Soda au Vinjwaji vyovyote vyenye "Sukari" ambayo sio Asilia na mpaka nikaamua kutumia RedBull ili kujiongezea "nguvu" ili niende Sambamba na Asali wa Moyo, basi ujue hali ilikuwa mbaya! Oh nimesahau kusalimia, Habari za Mwezi mzima? ahsante kwa kunitembelea hata kama sijaweka Post. Nashukuru sana.Haya tuendelee;  Unajua unapokuwa na Watoto bana, wanakukamilisha. Kwamba wanakupa "Pure love" tena kwa vitendo(ukaribu, kumbatio,mabusu,kukuambia wewe ni Mzuri), huvuka mipaka na kuanza kuonyesha kujali  na kukusifia umependeza, kukutafuta mara tu ukitoweka(kwenda chooni) n.k....pamoja na hayo yote kuna kitu kinaitwa Ulezi(kazi yako kama Mama).....by the time wanakwenda kulala Mama unakuwa  hoi. Suala la Kufanya Mapenzi na Mumeo umpendae huwa sio Muhimu kiviiiile. Sio kwamba hutaki....la hasha! Bali huna Nguvu.
Yaani ile umeingia Chumbani hamu zako zote na "plans" za kuwa Mpenzi ulizo-plan asubuhi zinawekwa pembeni....ile umegusa Kitanda tu unazima.....Kwa waume wengi huwa ni ngumu "kuamini" kuwa Mama unaeza kuchoka(unless Mume huyo awe amewahi kushinda  na Watoto peke yake kwa say 3hrs), Hujitahidi kuelewa kwa eer a day? hihihihihihi baada ya hapo wanaanza tena "kusumbua" Usingizi wako na "bado umechoka"?!
Sasa, Redbull ilikuja haraka na hakika ilisaidia kunifanya nibaki "macho", lakini haikunisaidia kwenye suala zima la kuneng'enuka. Kuneng'enuka kukawa ni "wajibu" which sikupendelea.....ni
Hii ilinifanya nikae Macho muda mrefu, ila inavimbisha Tumbo
soooooo NOT me! Nikakumbuka Embe, yep Embe Dodo kutoka Tabora au Embe Tanga kutoka Tanga. Embe Ng'ong'o na Embe Sindano kutoka Dar!Hizi makitu zina faida nyingi kwa Maili wako pia husaidia kukuweka "pale"haraka Kiasilia. Kwamba huitaji sana "kuhamasishwa" kwa Robo  Saa.  Kwa bahati mbaya huku ScoTigo hakuna aina hizo zote za Embe, isipokuwa unaeza kubahatisha Dodo zile kubwa au za Wastani....anyway they do the same great Job!
Vipande vya Embe na Cream
Mwanamke nimekuwa nakula Embe(Mbivu, Nzima) kila Siku  kama  Dinner kwa Wiki moja na nimeona Mabadiliko makuu sio tu Nguvu(za mwili, sio Ngono) bali pia Hamu haivumiliki (usingizi unapoteza maana hihihihi)na pia Ngozi inapendeza, Busy Mama kama Mimi? Mjaribu Embe, utampenda na hutomuacha!
Nivema kula Embe peke yake bila Cream, kwasababu Cream inanenepesha. Mie hutumia Cream mara moja kila Mwezi kwasababu sitaki kuongezeka/wala kukonda.....na-keep Uchimbonge nlionao wa Size 12.


Ahsante kwa Kuichagua Blog hii, naeshimu na kuthaminiMuda wako hapa.

Babai.

Wednesday, 2 March 2016

Jinsi ya kutojali.....au niseme jinsi ya kuto-give a damn?


....pengine how not to give a F*ck imekaa vizuri!! najua maana moja tu ya hilo neno F, nakumbuka Mwaka wa Kwanza Chuoni(when I was in London)....Jamaa mmoja alinambia "go f**k yourself" nkamwambia really?can you show me how?.....Darasa likawaka moto kwa kicheko. sasa sijui walikuwa wananicheka mimi(sijui Kiingereza) au jamaa. Achana na hili!Kujali kuhusu kila kitu au mambo ambayo watu wanajaribu kukufanyia na kwanini wanafanya hivyo husababisha maumivu ya Hisia.....unajua ile hisia unayoipata(ulipokuwa mdogo) pale unapomsalimia mtu Mzima halafu haitikii? Unaanza kujiuliza huku "umia" Baba/Mama nanilihu kwanini haitikii "shikamoo yangu"(labda alikuwa anakutaka) but kwa umri wako mdogo unahisi kama vile umenyang'anywa kitu cha thamani kinachoitwa "Heshima kwa wakubwa" ambacho Baba na Mama yako walikufunza.Mie binafsi nilikuwa nalalamika daily Watu Wazima wakinichunia, siku Marehemu Baba akanambia "kama hawaitikii Salamu yako basi usiwasalimie, achana nao" nkahisi huyu Mzee vipi? Unatufunza  daily tuwe na adabu na kusalimia wakubwa wetu, leo unaniambia nisiwasalimie.....tena? 


Tangu siku hiyo nikawa "Mwanzilishi" wa kuuchuna, nikiamini kuwa huwzi kunichunia mimi wakati mie ndio CEO hihihihihi silly eeh! Ukinichunia kwasababu ya issue zako za Kimaisha na mie nakuchunia milele. Hii imenisaida sana kwenye kutojali kuhusu watu wengine watanifikiriaje.
Ni rahisi sana kumwambia mtu asijali watu wanasema nini juu yake na kwamba yeye aendelee na Maisha yake, hasa kama mhusika ni Mdogo(20s). Unaweza kudhani kuwa Era  hii ya Sosho Midia ni rahisi kwasababu kuna Memes, Ushauri wa Jinsi(hows)  na Quotes kila kona. Uwingi wa hizo "makitu" ni  kithibitisho cha ongezeko la Ugumu wa "kutokujali" watu wengine wanasema/fikiria nini kuhusu wewe au chochote ufanyacho.Kila mtu Duniani anamaoni yake kuhusu kila mtu na kila kitu....Wakosoaji, wafuatiliaji na kila aina ya watu wapo huru na karibu zaidi na wewe(japo hawakujui) kuliko ilivyokuwa Miaka ya nyuma(wakati mimi nakua miaka ya 90).Pamoja na kuwa sehemu ya kukosolewa huko kunaweza  kukusaidia kufanya mabadiliko na kuwa mtu bora/mwema zaidi bado kama binadamu una hisia na unaweza kuumia  kwa kiasi fulani na ukashindwa kufanya kile ufanyacho au kuboresha kile kilichokosolewa9inategemea na Uimara wako sio).Kama kawaida, mimi nimeishi maisha  tofauti sana na "dada yako" mkubwa  na kwa muda mrefu  kukupita wewe hihihihihi hivyo nitakupa Hows zangu za  kutokujali Walimwengu wanasema nini, Kwanini na wapi? Chagua unalodhani unaweza kulifuata na kisha changanya na ya kwako na ya watu wengine ili kufanikiwa kwenye hili. Ila  ukifanya haya (bila mpangilio huu)yote  na kuchanganya na uyajuayo utanufaika zaidi. Twende sasa:-1-Uvumilivu- Unapitia hayo yote kama sehemu ya Ukuaji, unajifunza along the way na  the moment unaingia 28 utaona mabadiliko Makuu ya jisni unavyopokea na kuchukulia vitu/mambo. Haya unayopitia sasa utakutana nayo tena baada ya Kuolewa/Oa, yatahusisha watu ambao ni Muhimu kwa Mkeo au Mumeo....usipojifunza kuchukulia watu kama walivyo au kutojali sasa, ni wazi utaiona Ndoa ni Chungu na kuhisi umeolewa/Oa Ukoo Mzima.2-Focus-Weka Focus yako kwenye mambo muhimu zaidi kwako kuliko mtu/watu wengine ambao sio muhimu. Unacotengeneza sasa ndio kitakachokusimamisha huko mbele kimaisha, iwe ni Elimu, Biashara, Mafunzo n.k. Pia Focus yako kwenye ufanyalo itasaidia usiwe na Muda wa "kujali" yasioyo na Muhimu.3-Toa time out-Kwa Ndugu/Jamaa/Marafiki ambao ni wabaya/wasio na umuhimu kila baada ya muda(mie nilikuwa nafanya kila mwaka).....usisubiri mpaka wakukosee. Angalia tu ni nani anaumuhimu kwa sasa na ubaki nae karibu, wale ambao hawana umuhimu wachunie kwa muda. Hii huokoa muda na kupunguza Lawama.


Wazuri sio wale anaokuja kwako/kwenu kila siku au kukupigia simu kila siku na kuchat/catch up(kila siku?). Wazuri ni wale wanaoheshimu Muda  na  Nafasi yako....lakini ukipatwa na Shida watakuwa  karibu na kusaidia kwa namna yeyote awezayo.
4-Jione/Tambua kisha Jisifie- Ukingojea kusifiwa, utangoja sana na ukitegemea  Likes, RTweets tambua tu kuwa wasifiaji wa Online sio wakweli hihihihi (most of them). Sasa ni lazima utakuwa na moja (au yote)kati ya haya  mf. Elimika(kishule au kidunia), mrembo/mtanashati, Imara, unamahali pa kulala(hata kama ni kwa mama/baba), unajilipia/changia bills, unafanya mambo na kufanikiwa bila mchango wao. Lolote zuri au unalojivunia wewe kama wewe.....Jipe sifa!
5-Jitolee Muda-Kusaidia wengine. Kumsaidia Mtu sio lazima umpatie pesa. Muda wako ni Mali tosha, na huitaji kujitolea Siku nzima.....somea watoto kitabu mara moja kwa mwezi/wiki, saidia wengine kujifunza somo ambalo ni gumu kwao lakini kwako ni jepesi. Fanya jambo kwa ajili ya mtu mwingine ambae hakuhusu(toa msada/saidia).6-Jisomee...iweni Koran(Koroani), Biblia, Makala, Vitabu, itakusaidia kujifunza zaidi na kupata Amani.


-7-Usiogope kujitoa "mhanga".....Kama kuna issue inajadiliwa popote ulipo (kwa mfano)na unahisi kuwa unataka kuongezea, Uliza au kupinga with facts/points au kuunga mkono. Ingia kati na chukua sehemu yako na simamia usemacho lakini pia kubali kujifunza/elewa points kutoka kwa washiriki wengine.-8-Usiogope kukosea..... lakini usikosee makusudi(makosa yatakusaidia kujifunza zaidi)


9-Jipe time off Sosho Midia, au kama unaweza chagua  Platform Moja na usiwe kwenye kila Sosho midia "outlet". Kumbuka Dunia imekuwa Kijiji(Ahsante Teknolojia na urahisi wa kuifikia Internet), kwenye kila Sosho Midia utakutana na watu walewale na tofauti itakuwa majina labda, lakini mitazamo yao inaweza isibadilike. Sasa kama hawakupendezwa na wewe Insta hawawezi kupendezwa na wewe Snapchat etc.
-10-Kuwa Mbinafsi....ulikuja Duniani(ulizaliwa) peke yako na utaondoka(kufa) peke yako! So yeahaa don't give a fuck of what-who-where or why. Post hii nimelenga wadogo zangu, lakini kama wee umekua mwili tu na akili bado imebaki in your early 20s.....hongera kwa  kuibamba Post hii.


Ahsante kwa kuichagua Blog  hii na tafadhali share, tambua kuwa nathamini muda wako hapa.

Babai.

Tuesday, 1 March 2016

"Sheria" ya wa Ughaibuni kuwaletea Zawadi/kuwalisha Bata...

....nani aliiweka? au ndio mambo ya Mgeni karibu wenyeji tupone?


Nakubali upatikanaji wa vitu ni rahisi zaidi huku kuliko Tanzania, lakini hiyo haina maana kuwa ukusanyaji(ununuzi na utunzaji) wa  makorokocho(vitu) na kusafirisha ni Rahisi pia! Ukiachilia mbali hilo, pia badhi yetu tunapokuja Nyumbani ni kwa ajili ya mambo  mengine na sio kulishana Bata kwenye sehemu mbalimbali za Kisasa hapo Nchini.


Tandika SokoniEti wanataka ujisikie kama "upo nyumbani" kwa kukupeleka/tembeza meneo ya "Kisasa" ambako wanauza mavyakula(sumu) na vinywaji kama vya huko utokakao. Ukweli hapa sio wewe, bali wao ndio wantaka kenda kufanya watakayo kwa kutumia Vihela vyako vya huko utokako.

Stori time: Nimerudi zangu Bongo na Mwanangu wa kwanza, tena akiwa mchanga(miezi 8). Kiutamaduni ndugu na jamaa hakuna kumshika mtoto "mikono" mitupu si ndio? heeee! Mwanangu kashikwa na Mikoni Milioni na hakuna hata mmoja aliemshikisha "Senti"....well isipokuwa Mama yangu.
Baada ya muda wetu kuisha tukajikusanya na kurudi kwetu Ughaibuni, huku  nyuma watu wakaanza kulalamika kwamba tumekuja Tanzania Mikono mitupu....."Mwanamke hata zawadi looo!"."kutwa kutembea kwenye Masoko na Vichochoro badala ya kwenda Mjini...wajameni si nimewaletea Mpwa, Mjukuu, Kitukuu, Binamu, mwana kama Zawadi au? hihihihihi. Halafu ni hivi! ninachokuja kukiona ni kile mabacho sikioni Ughaibuni.....nafurahi kula vile ambavyo sili Ughaibuni, tatizo ni nini?Inawezekana ni sisi wenyewe wa Ughabuni ndio tumewazoesha baadhi ya watu, kwamba tunaporudi tunatumia pesa ili "tupate heshima" au "wasitusahau".... Mimi binafsi nabeba zawadi kwa Wadogo zangu(nilichukua sehemu ya Urithi wao kuja Huku) so automatikali wana kwalifai au wanaamini kuwa ni Haki yao na ni Jukumu langu(Ukubwa shughuli).Sasa, tangu nimezaliwa sijawahi kufika Mlimani City sijui ndio mnaiita Mall. Mie zangu Tandika Sokoni, Mwenge Sokoni, Kariakoo, Soko la Samaki Ferry, Kunduchi Sokoni na sehemu nyingine zote ambazo ni za kawaida.


Natumai Post hii imekupa tabasamu, kicheko, mshangao......vyovyote vile nashukuru kwa kuichagua Blog hii. Tambua nathamini muda wako.


Babai.

Tuesday, 16 February 2016

Kujua kila Kitu vs Kujua kila situation ya Watu........nirahisi kupatwa/kabiliana  na mengi kwenye Maisha yako na hivyo kujifunza zaidi, kuliko kujua kila situation ya mtu, achilia mbali watu ambao sio wewe. Niliwahi ku-blog kuhusu tabia ya watu "kujifanya" wanamjua kila mtu au zaidi "celeb" na life situations zao. Hakika hilo linawezekana, lakini ni vema kuweka wazi kuwa unayajua hayo yote kwasababu ya kusoma Gossip Sites/Blogs/TvChanells/Vijiwe/Joints n.k. na sio kwamba unawajua hao watu individually.
Kutokana na Maendeleo ya Kiteknolojia,  mawasiliano yamerahisishwa na hivyo baadhi yetu huwa tunapata Majibu/Ushauri wa Maswali/Matatizo yanayotukabili papo kwa hapo. Urahisi huu unafanya wengine kupitiliza kwenye kuchangia "uzoefu" wao kwenye "situations" nyingi kwenye Sosho midia husika na hivyo kukera baadhi.

Mie binafsi nina majibu mengi zaidi kuliko your "normal" Dada, kwasababu pengine n iliyopitia mimi kwenye maisha yangu na kujifunza au kupambana na kutatu ni tofauti na Dada yako au Pengine Wazazi wako ukiwachanganya pamoja(hihihihi this sounds ka' tusi) na  hata Mwalimu wako! Najua Mengi Kimaisha lakini sijui Kila kitu.
Hivyo huwa sishangai au kumkejeli yeyote ambae anaushauri/jibu kwenye kila jambo au mambo mengi(wewe huamini kuwa mtu huyu mmoja anaweza kupitia yote hayo maishani). Kuna Magonjwa mtu  amekabiliana nayo, ambayo watu wako hawajawahi kuugua. Kuna changamoto nyingi tofauti alizopambana nazo katika maisha yake nakushinda wewe hutokaa uzipate, Huenda anafanya kazi kwenye jamii na hivyo anakutana na Mengi anapokuwa kazini na hivyo kujifunza even more!
Sio hayo niliyoyataja tu bali kuna mengine anashuhudia na kuhusishwa na ndugu/jamaa zake ambao wanapatwa na matatizo ya Dunia, na yeye akajifunza, sasa badala ya kumsimanga/mcheka/kejeli mtu kuwa "anajifanya" anajua kila kitu au kumshangaa "haiwezekani ajue kila kitu" kumbuka na zingatia hili  Mwalimu Bora  Duniani ni Uzoefu wako Binafsi pia Mengi sio Yote!Ahsante kwa muda wako hapa, Nathamini na kuheshimu uamuzi wako wa kuichagua Blog hii.

Babai.

Monday, 15 February 2016

Mtoto "anaechagua" Vyakula....

....ndio mnaita "Fussy eater" eti?

Baadhi ya Watoto huanza mapema(au wazazi wao wanaamua kuwa watoto wao ni fussy kama sifa) katika hali halisi ni Uchovu unaopelekea kutokuwa na utararibu wa "kula" na attention ya kutosha kwenye kula kwa mtoto husika!


Kamwe sitokufunza namna ya kule mwanao, isipokuwa nitachangia uzoefu wangu ili kwa namna moja ujione kuwa haupo peke yako na hivyo kupata nafuu na pengine kuchukua "tips" na kujaribu ili mwanao apate virutubisho vyote Asilia ambavyo ni Muhimu kwa Ukuaji wake.Mwanangu wa Kwanza(Babuu) alianza kula Vizuri sana akiwa na Miezi Sita, alipofikisha Mwaka na Miezi 3(Miezi 15) akacha kunyonya mwenyewe(bila kuachishwa). Babuu alikuwa anakula kila aina ya Chakula unachompatia. Alipofikisha Miaka 2 hali ikabadilika, akaanza kukataa Nyama na Samaki which was Okay kwasababu alikuwa akila Mayai vema. Alipofika Miaka 2 na Nusu akawa anakula Viazi tu.....tena viwe vimepondwa(mashed).
Ukichanganya Mchuzi au Mboga-mboga kwenye  Viazi vyake "mashed", anasema "sipendi harufu" so anagoma kula na kuomba Maziwa.....then unampa Maziwa wakati anasubiri umtengenezee Viazi vingine bila "shombo". Mimi kama mimi, nikabeba Mwanangu huyoo mpaka kwa Daktari wake nakushtaki(kuelezea), Daktari akasema so long anakula Viazi, Mayai na Maziwa ni okay, ila niongeze matunda between meals! Hapana, sikufanikiwa.....tukarudi na kubaki kwenye  Viazi vya kuponda/Saga.
Wataalamu wanasema kuwa ni kawaida kwa Mtoto kuwa mchaguzi linapokuja suala la kula na kwamba ni sehemu ya Ukuaji. Wao wanatoa "Tips" kwa ujumla ili wazazi wenye watoto fussy tuzijaribu....napenda kukuhakikishia kuwa  nimejaribu zote na hakuna hata  moja iliyonisaidia.
Nikagundua kuwa Mama (au anaekutunzia mwanao unapokuwa Kazini) unakuwa na shughuli nyingi na zile Homono huwa hazijirudi haraka kwa baadhi yetu na hivyo kuna wakati unajisahau na badala ya kumpa mtoto chakula unampa maziwa kwanza ili aponze  njaa kisha ndio chakula(hapa lazma akatae), kosa ni kuwa anaponyonya njaa inakwisha, watoto sio kama sisi watu wazima. Kwamba njaa ikuma unakunywa Chai na kipande cha Mkate wakati unasubiri chakula kiive, Maziwa tumboni mwa mtoto wa umri wa Miezi 6 hadi miaka 4  hudumu kwa Masaa2+.Kumbuka, mtoto bado anajifunza kil akitu kwa mara ya kwanza, sasa usipokuwa na utaratibu unaojirudia utakaomfanya azoee na kuona kuwa ni "kawaida" anachanganyikiwa na kusahau at the same time!Sasa ile kutokuwa na utaratibu unamchanganya mtoto (kama nilivyosema)na matokeo yake anaanza kuchukia kula(unamlazimisha kula wakati hana njaa), hii haina "mtoto anataka kujitegemea kama Wazungu wanavyosema", hii  ni Mzazi/Mlezi kutokuwa  na utaratibu unaojirudia na wao kula kama Mazoea badala ya kula ili wapate nguvu/wakue(nia ni moja kuwa wale wakue na kujenga mwili ktk mtindo tofauti).Haikuwa kazi rahisi kumfanya Babuu aanze kula vizuri au niseme kawaida (isipokuwa Nyama), Zifuatazo ni Tips zangu Binafsi ambazo zinaweza kukusaidia  kama Mwanao ni Fussy eater;-


easy way kupata Matunda na Mboga 5 a day

1-Weka utaratibu wa Masaa ya Kula, Mf: Saa 8 Kifungua kinywa, Saa Nne na Nusu Snack, Saa Sita  Mlo wa Mchana , Saa nane na Nusu Snack, na Saa Kumi  na Moja Mlo wa Jioni na Saa Moja jioni Maziwa(husisia ku-relax na hivyo analala haraka)2-Usizidishe kipimo kwenye "snacks", kumbuka hii ni kupitisha muda kabla ya Chakula, sasa kama umeweka Maziwa/mayai ndio snack basi hakikisha unampatia kidogo ili asishibe.3-Mpe Choice(kama uchumi unaruhusu na anamika 2+), Utapenda maziwa na vitumbua au Maziwa na Mayai?....anaweza kusema Mziwa tu, mwambie ale kitafunwa kwanza halafu atapata Maziwa.4-Usimfokee, usimkaripie na wala usimlazimishe kula.....mbembeleze kula, ikiwezekana Mlishe(memlisha Babuu mpaka mwaka jana hihihihihi).....achana na  ile "tukienda kwa watu itakuwa aibu mtoto wa miaka 4 bado namlisha",...pima Wao vs Afya ya Mwanao.5-Kama kuna shughuli, hakikisha unambebea mwanao chakula chake unachojua anakipenda, ikiwezekana mlishe kabisa kabla hamjatoka.
6-Chagua aina moja ya Mboga ambayo ni "super food" lakini haina Harufu/Radha kali.....mie nilichagua Mchicha na Kale. Changanya Tutunda tamu na laini kama vile Papai, Embe, Zazibu, Ndizi na Moja ya Mboga hizo zikiwa Mbichi(bila shaka ni baada ya kuosha ) halafu changanya Vijiko Viwili Vikubwa cha chakula kwenye Mlo wake wa Mchana au Jioni. Na ikiwa mwanao ni mpenzi wa Mash basi ni nafuu kwako na kwake.
Kumbuka Mwanao ni  tofauti na hakuna kama yeye Duniani, ni an individual/his/her own little person hivyo usimfananishe/linganishe na watoto wengine wa umri wake au wadogo kwake. Muhimu ni kwa Mwanao kupata uzoefu wa radha tofauti tena kama ilivyokuwa mwanzo wakati unaanza kumtambulisha kwenye vyakula ili aache kunyonya, tofauti sasa  ni Mkubwa na anahitaji virutubisho zaidi kwani havipati via Nyoyo yako anymore. Amekuwa so Mashed kila kitu ni muokozi wako kwa sasa.Inakatisha tamaa, inachosha wakati mwingine.....lakini usikate tamaa. Jaribu Tips zangu.....hata akila vijiko 3 bado mchanganyiko huo utamsaidia ndani na nje ya Mwili.


Babai.