Skip to main content

Mango Vs Red Bull.....Boost Kitandani kwa busy mama wasio na Wasaidizi!


Sio mpenzi wa Soda au Vinjwaji vyovyote vyenye "Sukari" ambayo sio Asilia na mpaka nikaamua kutumia RedBull ili kujiongezea "nguvu" ili niende Sambamba na Asali wa Moyo, basi ujue hali ilikuwa mbaya! Oh nimesahau kusalimia, Habari za Mwezi mzima? ahsante kwa kunitembelea hata kama sijaweka Post. Nashukuru sana.



Haya tuendelee;  Unajua unapokuwa na Watoto bana, wanakukamilisha. Kwamba wanakupa "Pure love" tena kwa vitendo(ukaribu, kumbatio,mabusu,kukuambia wewe ni Mzuri), huvuka mipaka na kuanza kuonyesha kujali  na kukusifia umependeza, kukutafuta mara tu ukitoweka(kwenda chooni) n.k....pamoja na hayo yote kuna kitu kinaitwa Ulezi(kazi yako kama Mama).....by the time wanakwenda kulala Mama unakuwa  hoi. Suala la Kufanya Mapenzi na Mumeo umpendae huwa sio Muhimu kiviiiile. Sio kwamba hutaki....la hasha! Bali huna Nguvu.




Yaani ile umeingia Chumbani hamu zako zote na "plans" za kuwa Mpenzi ulizo-plan asubuhi zinawekwa pembeni....ile umegusa Kitanda tu unazima.....Kwa waume wengi huwa ni ngumu "kuamini" kuwa Mama unaeza kuchoka(unless Mume huyo awe amewahi kushinda  na Watoto peke yake kwa say 3hrs), Hujitahidi kuelewa kwa eer a day? hihihihihihi baada ya hapo wanaanza tena "kusumbua" Usingizi wako na "bado umechoka"?!




Sasa, Redbull ilikuja haraka na hakika ilisaidia kunifanya nibaki "macho", lakini haikunisaidia kwenye suala zima la kuneng'enuka. Kuneng'enuka kukawa ni "wajibu" which sikupendelea.....ni
Hii ilinifanya nikae Macho muda mrefu, ila inavimbisha Tumbo
soooooo NOT me! Nikakumbuka Embe, yep Embe Dodo kutoka Tabora au Embe Tanga kutoka Tanga. Embe Ng'ong'o na Embe Sindano kutoka Dar!Hizi makitu zina faida nyingi kwa Maili wako pia husaidia kukuweka "pale"haraka Kiasilia. Kwamba huitaji sana "kuhamasishwa" kwa Robo  Saa.  Kwa bahati mbaya huku ScoTigo hakuna aina hizo zote za Embe, isipokuwa unaeza kubahatisha Dodo zile kubwa au za Wastani....anyway they do the same great Job!




Vipande vya Embe na Cream
Mwanamke nimekuwa nakula Embe(Mbivu, Nzima) kila Siku  kama  Dinner kwa Wiki moja na nimeona Mabadiliko makuu sio tu Nguvu(za mwili, sio Ngono) bali pia Hamu haivumiliki (usingizi unapoteza maana hihihihi)na pia Ngozi inapendeza, Busy Mama kama Mimi? Mjaribu Embe, utampenda na hutomuacha!




Nivema kula Embe peke yake bila Cream, kwasababu Cream inanenepesha. Mie hutumia Cream mara moja kila Mwezi kwasababu sitaki kuongezeka/wala kukonda.....na-keep Uchimbonge nlionao wa Size 12.


Ahsante kwa Kuichagua Blog hii, naeshimu na kuthaminiMuda wako hapa.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao