Skip to main content

Posts

Showing posts from May 24, 2015

Msafi au Unajipenda?

Kuwa msafi ni tofauti na kujipenda.....Habari gani? Mimi sio Msaaaaafi to the point nahitaji "Tiba" ya Ushauri Nasaa, lakini napenda kusafisha Bafuni/Chooni na Jikoni (nachukia kuosha vyombo though). Maeneo au vyumba hivyo ni muhimu sana kwangu na kwa familia yangu kwasababu  natumia muda mwingi zaidi. Unapoenda Kushundi sharti utulie kwenye mazingira Masafi, haependezi kushundi(kutoa haja kubwa) huku unahofia kupata Maambukizo. Pengine unaharakisha kutoka na kukatisha Haja yako kwasababu ya harufu ya uchafu mwingine zaidi ya Kinyesi chako. Nahitaji kweli kuelezea kuhusu usafi wa Jikoni au Mahali unapoandalia chakula? Kuna siku nilikabidhiwa Jiko...si unajua wale akina Wifi/Shemeji ukienda kuwatembelea wanataka wakutumikishe? Basi nikapewa Jiko....mwenye Jiko mwenyee anajipenda huyo! Jikoni kwake sasa.....kulikuwa na uchafu worth of 3yrs akyanani nikashindwa kupika ikabidi nisafishe jiko na maeneo ya karibu. Kwenye Sinki kulikuwa na vyombo vichafu worth of 5days(Uanaum...

Matiti Makubwa(asilia) Vs Madogo....

Hi! Matiti ni fuko la Fat ambalo halina umuhimu....well zaidi ya kunyonyesha watoto. Sasa kama umemaliza kuzaa what do you do with them hasa yale Makubwa? Sie tulionyimwa matiti bana tukimaliza kunyonyesha tumatiti twetu tunapotea, yaani unabaki na alama ya matiti ambayo hayahitaji Brazia....well inategemea na umbile la titi, maana kama yako ni yale Papai shape au Embe sindano Shape mwenzangu hadithi ni ingine. Kwasababu ukubwa uliongezeka mara 3(mara mbili) kutoka B mpaka D na kifua kutoka 28-34inch.....yes nilikuwa 34D!!, hofu yangu kuu ilikuwa ni matiti kulala baada ya kumaliza kunyonyesha. Lakini baada ya watoto wawili yapo pale pale kati japo sio firm kiviiiiile lakini hayajalala (too small to sleep hahahahaha to sleep). ***Faida chache za kuwa na tumatiti tudogo ni kama ifuatavyo:- -Unanunua Sidiria Duka lolote kwa bei chee(japo huitaji one).....Ile shughuli ya kunyanyua Titi ili kujiswafi chini yake huwezi kuipata -Mambo ya kulala chali na matiti kukimbilia Kwapani haitok...

Wanataka uwe single Milele....

Watu unaofahamiana nao(wewe unawaita marafiki).....heiyaaa! Happy Bank Holiday wa hapa nilipo. Kama bado hujagundua basi utagundua muda si mrefu. Uhusiano wako unaponawiri tu, unaanza kusikia maneno maneno kuhusu Mpenzio au watu wanaomuhusu iwe Familiani au Kazini. Pengine hakukuwa na vijimaneno lakini tangu umefunga Ndoa wameanza kujitenga au kuanzisha urafiki(kufahamiana na watu wengine.....wale ambao wewe hupatani nao aka maadui zako). Au kila kitu kipo sawia na hayo hapo juu hayajawahi kutokea lakini tangu umejifungua au Mkeo kazaa basi na wao "marafiki" wanaanza kupunguza ukaribu kwako. Marafiki hao(watu unaofahamiana nao) wote au nusu na robo yao huwa kwenye Ndoa na Familia na wewe ulikuwa the only SINGLE one or the few of that robo ya mzunguuko wenu wa urafiki. Unaendelea ku-effort-ika(make an effort) kuwatafuta kwa simu au kutafuta muda ili kubadilishana mawili matatu kuhusu maisha yako mapya na yale ya enzi. Hawapatikani au hawatokei kwenye mihadi ya  kufurahia...