Watu unaofahamiana nao(wewe unawaita marafiki).....heiyaaa! Happy Bank Holiday wa hapa nilipo.
Kama bado hujagundua basi utagundua muda si mrefu. Uhusiano wako unaponawiri tu, unaanza kusikia maneno maneno kuhusu Mpenzio au watu wanaomuhusu iwe Familiani au Kazini.
Pengine hakukuwa na vijimaneno lakini tangu umefunga Ndoa wameanza kujitenga au kuanzisha urafiki(kufahamiana na watu wengine.....wale ambao wewe hupatani nao aka maadui zako).
Au kila kitu kipo sawia na hayo hapo juu hayajawahi kutokea lakini tangu umejifungua au Mkeo kazaa basi na wao "marafiki" wanaanza kupunguza ukaribu kwako.
Marafiki hao(watu unaofahamiana nao) wote au nusu na robo yao huwa kwenye Ndoa na Familia na wewe ulikuwa the only SINGLE one or the few of that robo ya mzunguuko wenu wa urafiki.
Unaendelea ku-effort-ika(make an effort) kuwatafuta kwa simu au kutafuta muda ili kubadilishana mawili matatu kuhusu maisha yako mapya na yale ya enzi.
Hawapatikani au hawatokei kwenye mihadi ya kufurahia siku husika, tena wala hawajali wala kuheshimu kuwa una Shughuli nyingi kwani sasa wewe ni Baba/Mama(priorities zimebadilika).
Unatafuta within yourself ili kujua umekosea wapi? Then unakuja kugundua kuwa "aaaah nina familia". Kumbe walikuwa wananipenda nilipokuwa sina Majukumu!
Sasa wananikwepa kwasababu sitokuwa free kwenda kwao ku-baby sit, kuwashauri kuhusu Ndoa zao na kuwakopesha senti(well mie....i still feel used).
Hao sio Fake isipokuwa ni watu ambao wanapenda kutumia wenzao kwa manufaa yao kwa kisingizio cha kufahamiana.....well wewe utasema Urafiki.
Shukurani kwa kuichagua Blig hii.
Babai.
Comments