Skip to main content

Posts

Showing posts with the label majukumu

Mtoto wa Kiume vs Wa Kike....

....wanatofautiana kwenye kila kitu, kuanzia utungwaji wa Mimba zao mpaka wepesi wa malezi, Ulaji wao na bila kusahau Ughali na Urahisi wa Mavazi. Kwa uzoefu wangu so far Mtoto wa Kiume ni rahisi ku-deal nae kuliko wa Kike(labda ni Homono).....Lakini Mtoto wa Kiume ni Ghali kuliko wa Kike linapokuja suala la Toys na Mvazi. Tukiacha tofauti hizo na nyingine ambazo wewe unauzoefu nazo, bado wote ni Watoto na wanahitaji Upendo, Mafunzo, Elimu, Ulizi etc sawa sawa. Natambua kwa Wazazi wetu ilikuwa tofauti, kwamba Msichana alikuwa akilindwa zaidi kuliko Mvulana. Baadhi ya Wazazi wa sasa bado wanaendelea na "Kasumba" hiyo ambayo mie nahisi kuwa imepitwa na wakati(inaharibu upande mmoja). Ni imani iliyojengwa miongoni mwetu kuwa Mtoto wa Kike ni "dhaifu" na hivyo ni rahisi kushawishika na kufanyiwa mabaya/kuharibiwa kuliko Mtoto wa Kiume.  Hii inafanya kuongeza "ulinzi" na Elimu juu ya "Watu wabaya" dhidi yao. Inasahaulika  kuwa huyu

Je! Mume huvutiwa na "u-Wife material" wa dada wa kazi?

Heri ya Mwaka Mpya! .....yanasemwa mengi juu ya Wasichana/Dada wasaidizi wa Kazi na kwanini hasa wengi huchukua "nyumba" na kuacha wenye nyumba(Wake) wakishangaa. Wengi hudhani kuwa shughuli anazozifanya Msaidizi ni shughuli ambazo Mama mwenyewe nyumba (ambae ni wife material) ndio hupaswa kuzifanya.  Sasa ikitokea Msaidizi anafanya kila kitu kuanzia kuwa "mama" mpaka Usafi wa nyumba na msimamizi wa Bajeti ya Chakula. Msaidizi huyu hana "nguvu"  ya kulalamika, kutoa changamoto au kubishana na wenye nyumba.....hasa Baba.  Msaidizi huyo siku zote huonyesha Shukurani na Heshima hata pale anapocheleweshewa Malipo(Mvumilivu). Huenda Msaidizi anafanya yote hayo kama sehemu ya Kazi yake, lakini sehemu ya Kazi yake haiji yenyewe. Kila nyumba/familia ina utaratibu wake na Mkuu wa taratibu za nyumbani huwa Mama/Mke.  Mama mwenye nyumba ndio humuelekeza Msaidizi afanye nini kwa siku husika......anamwambia afanye yale ambayo anajua Mumew

Wanataka uwe single Milele....

Watu unaofahamiana nao(wewe unawaita marafiki).....heiyaaa! Happy Bank Holiday wa hapa nilipo. Kama bado hujagundua basi utagundua muda si mrefu. Uhusiano wako unaponawiri tu, unaanza kusikia maneno maneno kuhusu Mpenzio au watu wanaomuhusu iwe Familiani au Kazini. Pengine hakukuwa na vijimaneno lakini tangu umefunga Ndoa wameanza kujitenga au kuanzisha urafiki(kufahamiana na watu wengine.....wale ambao wewe hupatani nao aka maadui zako). Au kila kitu kipo sawia na hayo hapo juu hayajawahi kutokea lakini tangu umejifungua au Mkeo kazaa basi na wao "marafiki" wanaanza kupunguza ukaribu kwako. Marafiki hao(watu unaofahamiana nao) wote au nusu na robo yao huwa kwenye Ndoa na Familia na wewe ulikuwa the only SINGLE one or the few of that robo ya mzunguuko wenu wa urafiki. Unaendelea ku-effort-ika(make an effort) kuwatafuta kwa simu au kutafuta muda ili kubadilishana mawili matatu kuhusu maisha yako mapya na yale ya enzi. Hawapatikani au hawatokei kwenye mihadi ya  kufurahia