Skip to main content

Je! Mume huvutiwa na "u-Wife material" wa dada wa kazi?

Heri ya Mwaka Mpya!

.....yanasemwa mengi juu ya Wasichana/Dada wasaidizi wa Kazi na kwanini hasa wengi huchukua "nyumba" na kuacha wenye nyumba(Wake) wakishangaa. Wengi hudhani kuwa shughuli anazozifanya Msaidizi ni shughuli ambazo Mama mwenyewe nyumba (ambae ni wife material) ndio hupaswa kuzifanya. 




Sasa ikitokea Msaidizi anafanya kila kitu kuanzia kuwa "mama" mpaka Usafi wa nyumba na msimamizi wa Bajeti ya Chakula. Msaidizi huyu hana "nguvu"  ya kulalamika, kutoa changamoto au kubishana na wenye nyumba.....hasa Baba. 


Msaidizi huyo siku zote huonyesha Shukurani na Heshima hata pale anapocheleweshewa Malipo(Mvumilivu). Huenda Msaidizi anafanya yote hayo kama sehemu ya Kazi yake, lakini sehemu ya Kazi yake haiji yenyewe. Kila nyumba/familia ina utaratibu wake na Mkuu wa taratibu za nyumbani huwa Mama/Mke. 



Mama mwenye nyumba ndio humuelekeza Msaidizi afanye nini kwa siku husika......anamwambia afanye yale ambayo anajua Mumewe atafurahi na hatohoji ikiwa atakuta yapo vizuri. Mfano nguo zake kuwa safi na tayari, aina ya chakula/upishi aupendao, usafi wa nyumba n.k.



Ni asili ya Mwanadamu wa Kiume(weka Ufeminist wako kando) kwenye Ndoa kujiona "Mwanaume" pale mwanamke anapoonyesha kujali.....eer kwenye malezi ya watoto,  Chakula, kuandaliwa mavazi(fua/nyoosha) kuwepo kwenye Mazingira mazuri/safi.


Ikiwa Msaidizi anafanya kila kitu nyumbani kwako hakika anakuwa "wife Material" kuliko wewe ambae ni Mke, ni rahisi kwa Baba mwenye nyumba kuhamisha hisia.....kumbuka Ndoa sio Uzuri wa Sura, Umbile na Mapenzi pekee! Kuna Mawasiliano, Ushirikiano, Ulevu na mengineyo kibao lakini pia  Uwepo wako wewe kama Mke na kutimiza sehemu ya Majukumu yako anayofanya Msaidizi wenu ndio husimamisha Ndoa.





Kwa wasaidizi wa Kiume kuchukua Nyumba, ni vema ikazungumziwa na Mwanaume. Mie sijui Majukumu ya Mwanaume.....ila najua kuwa Mwanaume anaemsaidia "Mke" kufanya kazi ngumu "za kiume" mfano anaelinda" iwe Getini au Shambani, ajituma kwenye Mapishi, mwenye kuonyesha Heshima, Asiekufokea au kuhoji umetumiaje Pesa, Halalamiki na kuwa available kwa ajili yako is sexy. Hayo pia yanaweza kumvutia Mwanamke Kimapenzi.




Haijalishi.....hata ukijaribu kuleta Msaidizi wa Kike au kiume "mbaya" bado haizuii kwa Mwanadamu kuvutiwa nae ikiwa afanyayo ni mambo ambayo Mke/Mume anadhani ni sababu ya yeye Kuolewa/Kuoa(nani anafunga Ndoa kwasababu ya Uzuri, Mapenzi na Ngono tu? Ndoa ni zaidi ya hayo).




Kama unamsaidizi ni vema usijisahau. Natambua maisha ya leo ni kusaidiana, kwamba sote tunafanya kazi na tunakuwa na muda mdogo wa ku-catch up kama wapenzi na Wazazi. Lakini hii isiwe sababu ya kumuachia Msaidizi afanye kila kitu......ndani ya siku 7 za Wiki tafuta Muda Kuwa Mke na Mama kamili kwa siku mbili.



Nafurahi umebarikiwa kuwepo nami 2016, naheshimu na kuthamini Muda wako, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao