Skip to main content

Posts

Showing posts with the label msaidizi

Je! Mume huvutiwa na "u-Wife material" wa dada wa kazi?

Heri ya Mwaka Mpya! .....yanasemwa mengi juu ya Wasichana/Dada wasaidizi wa Kazi na kwanini hasa wengi huchukua "nyumba" na kuacha wenye nyumba(Wake) wakishangaa. Wengi hudhani kuwa shughuli anazozifanya Msaidizi ni shughuli ambazo Mama mwenyewe nyumba (ambae ni wife material) ndio hupaswa kuzifanya.  Sasa ikitokea Msaidizi anafanya kila kitu kuanzia kuwa "mama" mpaka Usafi wa nyumba na msimamizi wa Bajeti ya Chakula. Msaidizi huyu hana "nguvu"  ya kulalamika, kutoa changamoto au kubishana na wenye nyumba.....hasa Baba.  Msaidizi huyo siku zote huonyesha Shukurani na Heshima hata pale anapocheleweshewa Malipo(Mvumilivu). Huenda Msaidizi anafanya yote hayo kama sehemu ya Kazi yake, lakini sehemu ya Kazi yake haiji yenyewe. Kila nyumba/familia ina utaratibu wake na Mkuu wa taratibu za nyumbani huwa Mama/Mke.  Mama mwenye nyumba ndio humuelekeza Msaidizi afanye nini kwa siku husika......anamwambia afanye yale ambayo anajua Mumew