Wednesday, 31 December 2014

2014....what a Year!

Ulitegemea nitaorodhesha matukio yote ya mwaka huu? Hehehehe pole. Napenda kuwa tofauti.Ahsante kwa kuichagua Blog hii siku ya leo ambayo ni ya Mwisho kabisa mwaka huu wa 2014, Ubarikiwe sana.

Wiki mbili zilizopita zilikuwa hectic kweli, si unajua Christmas inavyokuwa ukiwa na Watoto? Hasa mmoja ambae sasa yupo "Shule" na huko anafundishwa zaidi kuhusu "Santa na Presents" kuliko Kuzaliwa kwa Yesu...Achana na hili.


Sasa tangu nimekuwa Mama nimejikuta nasoma sana Forums zenye reviews mbalimbali kutoka kwa "real people" from Vipodozi to Kampuni za Umeme.
Nikawa kwenye Forum moja ya masuala ya Wazazi, Malezi, Mimba n.k. Nikawa nasoma review za aina ya Dawa ya Kuzuia Mimba (Uzazi wa Mpango)....mwanamke sijawahi kugusa hayo mavitu.

Kama kawaida hukosi maswali ya mabinti wadongo ambao wanataka kutumia Madawa hayo, nikisema wdogo kwa huku ninamaanisha 16 kushuka chini(inatisha, najua)!

Binti mmoja akasema anamiaka 22 na hajawahi kutumia Dawa yeyote ya kuzuia mimba zaidi ya Condoms....halafu akaomba radhi kwa kuwa "too late" kuanza kutumia Dawa hizo......hihihihihihihi nikaangalia huku na huku ili kuona kama kuna mtu ananiona(wakati nipo kwangu peke yangu).
22yrs old anajiona kachelewa kutumia Madawa ya Kuzuia mimba....mie mwenye 30na nitasemaje?

Acha uchafu, Mtu sio Mumeo, hujui hatima ya uhusiano wenu, huna mpango wa kuwa na watoto kwa sasa kwanini umruhusu akuwekee mauchafu yake mwilini mwako? Na utawekewe mara ngapi mpaka utakapofunga ndoa na kuamua kuzaa? Tumieni Condom huko mxsiii.

By the path, unataka kujua namna ya kutunza manywele yako? google "Long haire care Forum"....thank me mwakani.
Umaliziaji mzuri wa 2014, kifo hakihepukiki lakini unaweza kupunguza uwezekano....stay at home with your family.

Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 18 December 2014

Je wee ni Muafrika Halisi?

Kwamba vizazi 9 vya pande zote mbili (baba/ yako, Babu/Bibi yako, Baba/Mama wa Babu/Bibi yako, Baba/Mama yake Babu/Bibi wa Baba/Mama yako na whoever kabla ya wote hao) vilivyopita kabla yako ni Waafrika Weusi asilia bila tone la Uarabu, Ujerumani, Ureno na Uingereza?


Baada ya Obama wale Mchanganyiko wakaonyesha "rangi" yao, hasa wa huku....walikuwa wanaongea kwa uchungu na hasira kuwa wao sio Weusi bali ni Mixed, hawataki kutambuliwa kama Weusi bali Weusi na____!....Which was/is fair ila kwanini msubiri Mpaka wakati wa Obama?!!!


Huwa nakerwa na tabia ya baadhi ya watu (hasa Mixed ambao U-mixed wao hauonekani bali Weusi wao) wanaopenda kusema "mie ni robo Mhindi,Nusu na robo Muingereza halafu Nusu Muafrika".


Vita ya Ubaguzi kati ya Weusi Mixed na Real Weusi bado ipo na inaendelea kukua hasa baada ya "mapinduzi" ya Natura hair kwa African american aka Black peeps.


Wale Real ndio wanahisi wanahitaji pongezi kwa kuwa na nywele ndefu mpaka kiunoni kuliko Mixed, sababu technically Mixed sio real Weusi na manwele yao yanakua haraka....HUH!!!Kwenye Kizazi cha Tatu au Nne kabla yangu (Baba yake Bibi mzaa Baba...) alikuwa wa Rangi ya Kigeni....ila huwezi nikuta nakuhesabia robo na nusu....sio tu kuwa sipendi Hisabati bali pia sina hata tone la muonekano unaoashiria kuwa kuna "kadamu" ka weupe....yaani ni kama Mjukuu wa Obama mwenye Baba Mjaluo asilia(umepata lipicha?!!..) Ndio hivyo sasa.Naamini hakuna Real Muafrika, sema kuchanganyika kwetu kumetofautiana kutokana na ukaribu wa Kizazi kilichopita ambacho kilikuwa na Rangi ya Kigeni.


Shuleni kwa akina Babuu wanadhani Baba yake sio Muafirika yule Real hihihihihihi basi safari za Baba mtu kumpeleka na kumrudisha zimeongezeka....!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 9 December 2014

Mwanamke Kujitegemea Kiuchumi....

Ndio kukoje?


Unakumbuka enzi nipo Shule ya Msingi(just imagine...) enzi akina Taji Lihundi, Deo Mshigeni, Ramkim Ramadhani(RIP), Sunday Shomari....kabla ya akina JD hawajaja mjini....ndio walikuwa "the coolest"....Educated (well that is what I (myself) thought) watu kuwasikiliza na kuchukua "maushauri yao"....waliyokuwa wakiyasoma Ebony Magazine (sina hakika nimesema tu).

Taji Lihundi zake zilikuwa "I want a girl who can speak at lest 3 languages, independent, have a job and beautiful" by 3 languages hakumaanisha Kinyamwezi, Kihehe na Kizaramo....alitaka Malugha ya mbele huko.

Sasa huyu Baba(alikuwa mKaka then) ali-influence sana kwa akina sisi (Teenagers) enzi hizo bana, tulipofika miaka 20na na kuanza shughuli za kupenzika tukaanza kukimbia Vijana wanaoonyesha wapo sawa "kiuchumi" ili tusionekane "tegemezi".

Sasa kutokana na "muonekano" wako wa Independent....unapendeza, unavaa vitu vikali nini na nini....wanaonyesha interest wote ni wale wenye nazo....au ku-act wanazo ili wakupate, so unakuwa single, happy and Virgin kwa muda wa kutosha.

Mie sio shabiki wa Kuhongwa (japo napokea zawadi) kwasababu naamini nina uwezo na nguvu za kutafuta Pesa zangu....so babaa keep your Senti halafu ninuliage lizawadi KUU au tuunganishe tufanye jambo pamoja au nikipungukiwa niongezee.

Sijui kitu gani kinaendelea kwenye suala zima la kupeana Habari, Elimishana na kukumbushana kwenye Jamii. Napata mshituko ninaposikia siku hizi mabinti wadogo tu wanatunza wanaume, halafu wanaume wanakuwa-demanding kweli kwa wapenzi wao(wanawake) kutimiziwa mahitaji yao Kiuchumi.....tumepoteza Kizazi cha WANAUME wamebaki wanaume!

Mwanamke Kujitegemea Kiuchumi SIO kuhonga Mwanaume (unless ni Mtu mzima, upo desperate na nanilihu, aii kanunue Sanamu huko) na sio "kumtunza" mwanaume (Ni kinyume na Nature).


Hakuna kitu kinachokufanya mwanamke ujisikie umekamilika kama kuwa-looked after by mwanaume eti?!!

Pamoja na kujitegemea kwako Kiuchumi haina maana unachukua jukumu lake la kukutunza na kukuangalia wewe kama mpenzi au mkewe.

Hata Beyonce anajitegemea kiuchumi lakini Jay-Z anamtunza mkewe si eti? Well sina Mfano halisi kutoka Kioo cha Jamii Tz....so yeah!


Samahani kwa watoto na wenza wa jamaa niliowataja (ikitokea mmekatiza hapa), nyie wengine bana kama nimewakwaza just unread my Post.


Cheers!
Mapendo tele kwako...

Friday, 5 December 2014

Wema hadumu....

Now I have your attention, kaa chini.....Wema hawadumu (hufa mapema) ndio namaanisha.Hivi hujawahi kujishtukia na kupunguza wema ili usije ukaenda mapema? Mwanamke I have!

Wema mtu anazaliwa nao (nadhani) lakini pia unaweza kujifunza kuwa mwema....sasa kupunguza wema sio kwamba unakuwa na roho mbaya bali unapunguza "misaada" iwe ni Pesa, Vitu au Muda wako kwa watu wengine.

Kitendo chako hicho kinafanya wale "watu wengine" wakuone unaroho mbaya au sio mwema kiviiiiile na hivyo kuanza kukujungua na kukudongoa(kukusema vibaya) na hapo siku zako Duniani zinaongezeka (in my head)!

Hayati Bibi aliwahi kusema watu wanapokusema vibaya na hata kukutakia/ombea kifo ni vizuri kwani wanakutakia kinyume chake....Unaona my NUKTA sasa! Muone mzito kumkichwa ka' m-Irish.

Usije anza kumuombea mtu wako mpendwa anaeumwa afe ukitegemea itakuwa kinyume hehehehe lwako.


Furahia Mwanzo wa Mwisho wa Wiki yako.

Babai.
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 3 December 2014

Akina sie on Budget...

Ili kuifanya itoke vizuri huwa tunajiita "the simple life" women....well U-simple unatofautiana nadhani unalijua hilo.

Mfano hapa hunikuti na hautonikuta nazungumzia Manunuzi ya Wiki au Mwezi huko High end (Designers) pamoja na hilo pia hunikuti nazungumzia Maduka ambayo ni Lowest End.....mie nipo kati. Napenda Ubora, Mfano Bag lazma iwe Real/Genuine Leather kwani ndio my Kitu sio Trends.

Sasa si nilipita kwenye Charity Shop maeneo wanayoishi Mastaa Jumamosi iliyopita, nikakuta watu Kibao kwa nje....nkauliza kwani kuna Star humo ndani? Wakasema hapana ila kuna "new stock" by new wanamaanisha Stars wame-donate Ma-used-designer Gear jana yake.

Aii! Mwanamke sijawahi kumiliki Designer Bag Genuine....wee! Mie huyu ninunue Hand Bag kwa £2,340 wakati hata Tofali la Choo (sio Jimmy Choo, Choo as in Toilet eeh) sina.....hata Fake ones sina.

Nikaweka u-simple pembeni....nkaunga foleni....nkajipatia "Chloe Python Paraty Tote Bag". Mpaka jana bado nilikuwa na-google ili kuhakiki kuwa sio Fake hihihihi kutokana na bei yake.

Pamoja na kuwa nimepata Hand bag, napata amani moyoni nikijua senti yangu imeenda kumsaidia mtoto somewhere Duniani.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 2 December 2014

Happy December.....nimekuwa huru!

Nikajikuta nashindwa kusoma maandishi au kutambua Sura ya mtu kwenye Tv au popote pale ambapo ni umbali wa hatua 4, sasa naona (Navaa Miwaani baada ya kuikwepa kwa Miaka zaidi ya 15).

Halafu Binti kaacha kunyonya full-time (haombi na wala hadai) hooray...whoop!...whoop!Sasa siku moja nipo Bafuni najilola(najiangalia) nikaona pale nyuma kati pamekuwa a bit "firm" and more Duara(maana ukizaa matako yanashuka/tepeta kidogo ujue)....nkasema wohooo mazoezi yangu yanalipa!

Kuja kuhamaki....kumbe nimenenepa hihihihihihi(nlijipima kitu kutoka 32inch to 46). Side effects za kuacha kunyonyesha nazo, mxsiii (kama unataka kuzijua zote nitafute nikumwagie mauzoefu).

Na mwisho kabisa Asali wa Moyo anaumwa "Flu"(Homa, body ache, Kikohozi na Mafua).......si unajua wanaume wakiumwa "Flu"...full kudeka hehehehe I mean "hoi" imagine wangekuwa wanazaa the Puuzi kabisa!Babai.
Mapendo tele kwako...

Friday, 14 November 2014

Wale "naenda Africa", Natoka Africa....

Unawajua?

Huwa hawasemi Nchi zao.....mf: unauliza (kwa kizungu) unatoka wapi? Wanasema "Africa"....where about in Afrika...."East Africa"....yes...where exactly?

Sasa tangu Ebola ime-"cotton fire" Afrika inaitwa the Land of Ebola....hihihihihi watu hawasemi tena wanatoka Afrika bali Tanzania au nchi yeyote ambayo sio Magharibi ya Afrika (au karibu)!

Kuna jamaa enzi akiwahi kusema (na wakamuamini) kuwa yeye anatoka Afrika, akaulizwa Afrika wapi....akasema "a small Country inside Tanzania called Tabata" na Baba yake ni King of Tabata!


Mie siipendi Tanzania Kisiasa(sipendezwi na Siasa za Tanzania), lakini naipenda kama Nchi niliyozaliwa, na ndio maana sina (nimekataa) Ganda Jekundu kwa makusudi kabisa....(Kwa faida ya Wanangu)!Nilivyojihami hapo juu!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 13 November 2014

Vyombo vya Wageni....!

Vinakaa Kwenye kabati KUUUUUUUbwa sebuleni (I used to hate that thing)....ila nilikuwa naelewa kwanini wengi wao (nilikuwa mtoto so simo) huwa na Kabati la vyombo (vitumiwavyo only wageni wakija) Sebuleni.


Nyumba nyingi za kupanga ama Mna-share jiko au kila mtu anapika Sebuleni kwake kama sio nje ya mlango wake pale Koridoni/kwa nje, hivyo kuwa na Kabati la vyombo Sebuleni inaleta maana(Wapangaji sita, wote muweke makabati yenu jikoni? Hapatatosha).
Achana na hilo...turudi kwenye "vyombo vya wageni"....mpaka leo (well mwaka juzi niliponunua Gold China Dinning Set and Tea Set*) ndio nimeelewa umuhimu wake.

Kuwa sahihi naweza kusema nimejua umuhimu wa viatu vingi baada ya kuwa "Temp house wife", vitu kama vile kusafisha nyumba mara kadhaa kwa siku (nlikuwa nasafisha once a week, ile deep cleaning).

Sasa nikienda madukani, lazima nikasalimie kwa akina "Home Departments"....yaani hadi nimeanza kuwaza mambo ya kuwa "Part time Interior Designer"
Je, unataka ku-feature? Weka maelezo yako kwa kifupi ambayo ni maisha halisi na unauzoefu nayo....fundisha au kuonya in kuchekesha way.... weka kwenye email halafu bonyeza Send.Babai!
Mapendo tele kwako...

Sunday, 9 November 2014

Kuchamba or Kutokuchamba (kwa Maji)

Wewe una prefer ipi?


Kabla ya Waarabu (Wachamba kwa Maji) na Wazungu(Wachamba kwa Karatasi)....Watu walikuwa wakitumia Majani au Mchanga kujiswafi baada ya kushundi(Kutoa haja kubwa).

Tulikuwa (utotoni) tunatumia "karatasi" (toilet tissues) siku maji yakikatika. Maji na Mkono ni sehemu ya "utamaduni" (ambao tuliletewa na Waarabu) na baadhi ni Usafi.

Hii haina Uzungu bana, ila mambo ya kushika mavi yako moja kwa moja mie hata sipendezwi nayo!....angalau ukitumia "tissue" huyashiki mavi moja kwa moja pale mahala.

Baadhi ya watu hudai kuwa wasipotumia maji hujihisi "sio wasafi" huenda ni kutokana na Mazoea au....well nenda karudie kuchamba tena kwani ni wazi umeacha mabaki.

Ukitumia muda wako vizuri baada ya kushughulika utakuwa msafi(usisahau kuosha mikono kwa kutumia Sabuni hataka kama hujagusa Shundi lako).

Kwanini nakuambia hivi? Well ni kwasababu ya Wanangu...najiuliza niwafunze kutumia Maji au niendelee na Karatasi?

Lakini kutokana na Mazingira waliopo kutumia maji itakuwa trick (sitaki kushika mavi hata kama ni ya wanangu) au a bit confusing kwao kwani kwa marafiki zao hakuna "utamaduni huo", Mashuleni haipo (unless ni shule ya Kiislamu) in which hawatokwenda.
Na-sound Mzungu sana eti?!!! Hii haina uzungu ni Logic tu.....Kutumia maji wakati unashika Mavi yako direct sio Usafi hata kama utaosha Mikono baada ya hapo!

Nakuona hapo unataka kuleta habari za "mbona Qatar kuna facilities za kuchambia bila kugusa eneo la kutolea kinyesi" au "when I was in Dubai"..... ntakutukana.

Baadhi ya Hoteli pale Dar kuna facilities za kuchambia (zina-flash mavi outta your O) but how many of us live in Hotels....eti?!!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Friday, 7 November 2014

Inapendeza sana na unapata hisia maalum za kipekee unapokutana na "High End" new publication wanazugumzia kitu ambacho wewe(Mimi) "nisiejulikana End" nimekizungumzia Mawiki na Mawiki yaliyopita!

Unakumbuka Feminisim?hiyo ilikuwa Wiki iliyopita so achana nayo!....unakumbuka "kujilinganisha/fananisha"?.....aaah Dinah naona mbali sana ujue, nafaa kuwa Rais wa KissWay?!!! (*nimeacha kuchapa nacheka kwanza*).

Pengine bila kujua unachapisha maelezo ya siku yako ilivyokuwa "njema" au unaweka picha au unaweza tu ku-share ulichonunua wiki hii kwa ajili ya wanao au mwenyewe n.k.....ni sehemu ya maisha yako hivyo unadhani ni poa tu uki-share na watu wanaofuatilia "kurasa" yako popote ulipo kwenye Social Media.

Kuna mahali unafikia unakuwa karibu sana na watu hao ambao huwajui(mnakuwa connected), sometimes mna-miss-iana.....Jinsia tofauti hapa lazma "lust" au hata "love" hujitokeza....duh! Nilikuwa nazungumzia nini kwani? Mweeee.....!!!

Oh, nimekumbuka....Baadhi ya wafuatiliaji wako (au wewe mwenyewe maana Sosho midia ni 2ways) ama wanaumia kwasababu hawawezi kuwa na maisha ka' wewe au wanataka kuwa na maisha kama wewe au wanataka kukupita au kuonyesha kuwa wamekupita.....hapo sasa Kujilinganisha/Kujifananisha kunapojitokeza.

Hii sasa inachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza hali ya kujiamini kwa baadhi ya watu, wanakosa raha na kujiongezea msongo wa Mawazo.

Ongezeko la Kipato kwa Wanasaikotherapi na ni Tenda mpya ya Wa-Famasia kuja na Dawa ya "disorder" hii mupya iitwayo CCD(Constant Comparison Disorder"....ambayo inaharibu maisha ya watu.

Ujue Maisha ya Kawaida ya Ulayani nilipo ni Luxury kwa baadhi ya watu huko nilikotoka, sasa sio mbaya kama tukijaribu ku-limit tu-share-ayo na wenzetu hasa wale wa Kunyumba!
Hivi by the time nafikisha Miaka 50, Cosmetics surgery si itakuwa imeshuka bei?!!!Babai
Mapendo tele kwako...

Thursday, 6 November 2014

Zawadi kutoka kwa Mwenza!

Kwa siee wa Ulayani huwa tunapenda sana zawadi kutoka Nyumbani, zawadi (Radha ya Nyumbani) kama vile Ubuyu, Mahindi Mabichi*, Matembele ya Kukausha, Dagaa wa Kigoma, Viuongo vizima vya Pilau, Maembe Dodo au Embe Tanga bila kusahau Embe Ngong'a(unazijua?!!), Maharage ya Mbeya au yale ya Njano, Njugu Mawe n.k.

Mimi binafsi huwa napata hizo mavitu moja kwa moja kutoka kwa Mama, lakini kwa wale wenye Wenza wanaopenda kwenda Bongo Mara kwa Mara huwa wanavipata moja kwa moja kutoka kwa Wenza wao.

Tatizo ni kuwa Mwenza anapokuletea zawadi wakati mwingine inakuwa imetoka kwa Mme/Mke mwenzio bila wewe kujua.

Inasemekana wenzetu walioungana na "rangi" tofauti huwa wana-miss sana "rangi" yao hivyo wanaporudi Nyumbani huwa rahisi kupata wanawake/wanaume ambao huwapatia kile wanachokikosa kutoka kwa wenza wao Weupe....Maisha yaha....namaanisha Haya!!!

Halafu kuna wale ambao wanapenda tu kulala hovyo(Malaya)....Ujue! Ili uendelee kuwa interested na Kimada wa Kiume/Kike kila unapotoka Ughaibuni ni vema kuonyesha unaipenda Familia yake (ili akuamini) na hapo ndipo suala la Zawadi linapokuja!

Mke/Mume anarudi kutoka Bongo na makilos ya kila kitu nilichokitaja hapo awali, hadi dawa za Miti shamba.....hihihihihi mambo ya "radha" ya nyumbani!

Mwenyewe unapokea kwa furaha ukidhani zatoka kwa mwenza kumbe ni kwa Mke/Mume mwenza! Mara unaanza kumchukia Mumeo/Mkeo bila kujua sababu.....hehehehehe.

Kabla hujanijaji! Mama amekuwa na tabia ya kuniandalia mavitu hayo akijua naenda au kuna mtu anaenda so nina uhakika havitoki kwa "mwenza" bali Mama yangu mpendwa.
Halafu anavyojua kuvifunga sasa, hehehehe nadhani ni kwasababu ya "security" Uwanjani.....amekuwa akifanya hivyo Tangu sijakutana na Mume wangu. Enzi nasoma!Isitoshe hakuna mtu anakula "radha" ya Nyumbani bali mimi peke yangu.


THE POINT is........


Babai.
Mapendo tele kwako...

Friday, 31 October 2014

Kuaga au kutokuaga Marehemu!

Hiyaaaa!

Leo si Halloween bana, wacha nami niungane nao kwa kuzungumzia Wafu.


Jana tulikuwa (Mimi na Asali wa Moyo) tunaangalia Tv, mara Tangazo la Documentary ya Ebola (Ebola crisis) hilooo!


Nkasema mie sipendi kuona/onyeshwa miili ya wafu hata kama imefunikwa(hifadhiwa vizuri), kama wameenda wameenda tu hata mkituonyesha haifanyi Ebola kuwa Hatari zaidi ya ilivyo!

Mwenzangu akasema, "mie sielewi kwanini watu hupenda kwenda kutoa "Heshima" za mwisho wakitegemea kumuona Marehemu kwa mara ya Mwisho, marehemu ambae hawakuwa nae karibu kama Ndugu(wa Damu). Kwanini utake kumuona Mtu akiwa Maiti?

Nikakumbuka Msiba wa Marehemu Kanumba(Mungu akuongezee heri huko uliko, Ameen), ambao sasa umekuwa (in my head) kama "model" ya Misiba ya MaCeleb wa Bongo kwa Uwingi wa watu....*whispering* nasikia MaCeleb wa Kibongo wanaombea nao wajekuzikwa na watu wengi kama huyo nliyemtaja!

Walioshiriki walilalamika na wengine kukasirika kwanini hawakupewa nafasi ya "kumuona" Marehemu kwa mara ya mwisho!

Waingereza waliotuletea "utaratibu" wa Kuaga Marehemu kwa kuiangalia Maiti hawafanyi hivyo tena kwasababu wanakiuka Haki za Marehemu (Binaadamu) husika....unless alisema kwa maandishi kuwa anataka kuonwa akiwa hana uhai.

Sasa leo nilikuwa Duka la Madawa nasubiri Dawa(wanangu wanakohoa kwa Mashindano.....ahsanteB *nahisi umenipa pole*).

Pembeni alikuwa amekaa Mmama mmoja Mweupe(Mzungu), kachangamkaa, kama kawaida akaanza Stori...mara nikamaliza yangu (pata Dawa) nikamuaga.....akasema "am trying to be nice to everybody, because I don't know who'll look after me in a Nursing Home or Hospital".....mie nkatabasamu nkasema "aww how kind"....Do I look like a....never mind!

Point hapa ni kuwa, kwanini tunapenda kuhofia nani atanizika....nani atakuja kwenye Msiba wangu na kuishia kujenga urafiki na watu wengi ambao ni Maadui!

Hebu tujaribu kuwa nice/kind kwa kila mmoja wetu bila kurafikiana kwa kuegemea kwenye kuhofia nani atatusaidia Hospitalini au tutakapopata Udhuru mahali ambapo hakuna umjuae/akujuae.

Babai.
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 29 October 2014

Wacha kuzungumzia Wanao, unatukwaza!

....ambao hatuna watoto!


Kabla sijawa na Watoto sikuwahi kukwazika ikiwa mtu anazungumzia mtoto au watoto wake. Niliona ama chukulia kuwa ni sehemu muhimu ya maisha yao.

Wakati huo nilikuwa nazungumzia mambo ambayo hayahusishi "wazazi" hivyo ni wazi mimi pia nilikuwa nawakwaza wenye watoto (in my head).

Maisha tunayoishi siku hizi "Ulayani" au Ulaya ya hapa nilipo yametawaliwa na "hofu" ya ku-offend (kukwanza) wengine.....imefikia mahali mpaka Sikukuu ya Krismasi inakwaza wasiohusika (mostly Waislamu).

Yaani ule uhuru wa kuzungumza na mtu kisha kuulizia kama anawatoto haupo tena. Ila mie huwa nauliza kwanza kabla sijaanza habari za akina B-I(initials za majina ya wanagu).....wakisema hawana watoto then siwazungumzii wanangu, wakisema wanao hapo inakuwa sherehe.

Suala la watoto linatetewa kwasababu lina umiza hisia za baadhi ya watu ambao kwasababu mbalimbali hawana watoto.

Well, binafsi nimeacha kuzungumzia na kufuatilia Siasa za Dunia, sio mpenzi wa kuzungumzia Celebs, na sipendi kuzungumzia Misha ya watu wengine.

Sehemu kubwa ya Maisha yangu ya sasa yametawaliwa/chukuliwa na Wanangu hivyo sina mengi ya kuzungumzia zaidi ya wanangu ambao wanafanya mengi ambayo sijawahi kuyashuhudia mbele ya Mcho yangu.

Meenda mchukua Babuu kutoka Vidudu,"Development officer" wake akaanza kunipa "ripoti", baada ya maongezi nikauliza kama anamtoto...akaniangalia kwa uchungu kisha akasema "bado sijabarikiwa" akaanza kulia.Babai
Mapendo tele kwako...

Monday, 27 October 2014

Feminism....

Na ugomvi wao wa nani ni "real Feminist", yupi ni "fake Feminist" anatumia U-feminist kama "PR" na yule sio "feminist enough". Women....WOMEN!!
Majuzi yaleee, well Wiki iliyopita)....nilipokuwa naandika post ya maJuzi yalee nikajihisi nakuwa Feminist!
Then nkakumbuka....Nimeitwa majina mengi sana mabaya, machafu na makali tangu nimeanza kujihusisha na "maisha " ya online mwaka 1999, yote huwa hayaniumi kwasababu najua mimi sio hayo majina wanayoniita (wote hawanijui zaidi ya maandishi/text).

Ila walipoanza kuniita "Dinah ni Feminist" kiasi cha kutosha, nikaanza kuchukia na kutamani kubishana au kujibu...."acha Uswahili" inakuja kichwani, nadharau na kupoteza Comments husika!

Binafsi sipendi kuitwa Feminist pamoja na kuwa baadhi ya "views" zangu za kimaisha zinaweza kukufanya udhanie kuwa mimi ni Feminist.

Sababu nyingine inayonifanya nichukie kuitwa "feminist" ni kibongo-bongo na baadhi ya Wamagharibi (stupid ones) U-Feminism unahusishwa na chuki dhidi ya wanaume au kutaka kuwa "sawa" na wanaume .

NAWAPENDA wanaume na kamwe sitaki kuwa sawa nao (isipokuwa Kiheshima, Kielimu na Kiuchumi) vingine wabaki navyo, ahsante nashukuru!.

Napenda, ninafurahia na kuridhika kusafisha nyumba yangu (sipokuwa kusafisha vyombo), kupamba na kuremba Kitanda chetu,....kupika na kumuandalia Asali wa Moyo chakula.
Napenda kuwa "in-control" kwenye masuala ya nyumbani ambayo wewe unayaita "kazi za mwanamke".....time to time Asali husaidia shughuli hizo kama wote tumekazika(wote tulikuwa job).

Oh! Kabla sijasahau...(Feminists lazima waniuwe kihisia hapa) ninaamini kuwa mwanamke anapojipendezesha halafu apite mtaani bila kupata "sifa" kutoka kwa wanaume au hata "ka mluzi", lazma atajishtukia.....Tunapendeza ili kuvutia wanaume, nao wanaume wanapendeza kutuvutia Wanawake....ni Nature!!Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 21 October 2014

Vita dhidi ya Ebola imeSiasa-iwa!

Kila mtu anakuja na lake, mara Wazungu wametengeneza Ebola ili "kumaliza" Kizazi cha Weusi(Waafrika)...huyu ni Mwafrika/Mweusi aweza kuwa Manasiasa au Mtaalam(daktari) n.k.

Mzungu wa kawaida (mtaani) anahoji Kwanini mnahaha na Ebola iliyoua watu Chini ya Elfu Kumi wakati Malaria inaua Mamilioni ya Waafrika kwa siku? Vipi kuhusu HIV na Umasikini ambavyo vinaondoa mamilioni ya Watu....TB je?

Karibu Miezi Nane tangu mlipuko "mpya" wa Ebola kuibuka(according to my kumbukumbu) Wamagharibi walielekeza nguvu zao Ukraine na Iraqi ambako kuna faida zaidi ya kuokoa Maisha ya Muafrika, Afrika.....mara boom wanapigana zaidi kuliko wenye Tatizo (waafrika)?!!

Mwenyewe jana nikajiuliza, kwanini US, EU na Cuba (is Cuba....never mind) wanapeleka "jeshi" la Wataalam kupigana na Ebola which ni more expensive kuliko kupeleke Vifaa na Wataalam wachache wa kutoa mafunzo kwa Locals (Waafrika).
Nikapata jibu kuwa, labda Wazungu wanajua wakiwapa Vifaa na Dawa (zile Trials) mtauza na tatizo(Ebola) litabaki pale pale na hivyo litawafikia huko waliko (EU na USA)....wanataka kulimaliza huko huko lilipoanzia lisifike kwao.
Au pengine wanashindana tu kiSiasa ili kujisifu "nani" alikuwa mstari wa Mbele kusaidia. USA wanafaidika sana na Afrika Magharibi (ukitoa Naigeria) na EU inafaidika na kwingine kote kulikobaki.

Kuna wakati napata aibu ya kuwa Muafrika kimoyomoyo, ila ukiniona mtaani ninavyojivunia Uafirika wangu wee....but kwa ndani naona SOO sana...tunatia aibu sana sometimes.
Over to you to argue kama I hate my skin or my Africanismness*(is that a word? usi-google tafadhali hihihihi).


Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 20 October 2014

Kwanini Mtoto awa wa Baba?!!

Nimekaa hapa nikafikiria(sio kweli)....limenijia tu kichwani.
Kwanini tunaaminishwa kuwa Mtoto akizaliwa ni wababa, Jina lake la ukoo lazima liwe la Upande wa Baba. Ukimpa mtoto jina lingine la mwisho....baba anakuwa Mkali au anahoji kama kuna "mwenzie"!

Kutokana na Mfumo Dume, nahisi(in my head) kuwa wali/na lazimisha hivyo kwasababu walijua/wanajua kuwa Baba ana sehemu ndogo sana kwenye Uumbwaji wa Mtoto.
Baada ya zile Dakika Tatu (if you are lucky that is) kazi yake (baba) imeisha, isitoshe Mbegu hazina Damu so mtoto kuwa na Damu ya Baba yake ni kama 0.5% hihihihihi (lazma mnipige mkinikamata wababa).
Hebu angalia suala hili kwa undani kwenye jamii bila kuhusisha Sayansi wala Dini! Kwanini hasa Babaz au ndugu Upande wa Mwanaume ndio huwa na viherehere vya kuendeleza Undugu kama sio kujishtukia kuwa hawana undugu (wanalazimisha).
Stori time: Kuna siku nipo shereheni, mkaka mmoja akaanza kutambulisha ndugu wa Mama mbali-mbali lakini baba Mmoja kuwa "yaani ukimkata huyu ukachukua Damu yake ni Asilimia Mia moja inafanana na yangu".
Nkacheka kimoyo-moyo huku najisemea mngekuwa mlizaliwa na Mama mmoja then YEAH mngekuwa Asilimia 99 ya Damu....na ile 1 ndio ya baba zenu (0.5 each) bwihihihihihihihiiii.
Wee unafikiri ni kwanini Wanaume wanapenda kusema "wee mwanamke tu"....wanataka ujione "mdogo", "huna thamani", "huna umuhimu" ili wakutawale kwa nafasi na wewe unawapa nafasi eti?!!.....duh! I sound kama Feminist sasa.....*zima Device*


Baibai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 13 October 2014

"Ngoja nitakupigia" = Stop calling me....

Za milimo?


Unawatambua wale watu ukiwapigia simu hawakawii kukuaga utafikiri wao ndio wamepiga....mnasalimiana vizuri, mara baada ya salamu...enhe nipe stori au "mamo mengine vipi?"
Upande wa pili wa Simu(uliempigia) anaanzisha stori, unamsikiliza ukingonjea kwa hamu zamu yako ije ili uongezee kwenye stori husika (uongee).....yeye anakuambia " eh bwana eh, ngoja nitakupigia" halafu kimyaa.

Baada ya Wiki kadhaa unampigia tena na kabla stori hazijachanganya yeye yulee "nitakupigia baada ya dk 20"....ndio imetoka hiyo mpaka umtafute tena.
Mtu hutakiwi lakini hukomi mpaka mtu akuambie "sitaki Urafiki/Ujamaa/kujuana na wewe"....baadhi ya watu wanakupa "ujumbe" ili "muachane" vizuri bila kusutana, ukikimbiwa once na "nitakupigia baadae"....subiri mpaka akupigie (obviously hatokupigia).

Unajua kuna watu wanapenda kuwa tegemezi kifikra.....hata sijui kama inaleta maana kwenye nilichokigusia hapo juu.
Kuna baadhi yetu tunapenda kuonekana Wema, tunajali hata mahali ambapo hapahitaji Wema wala kujaaliwa. Huitaji kushi ili kufurahisha watu(kila mtu kaja kivyake/kazaliwa kivyake) sasa ishi kufurahisha nafsi yako kwani ukifa utazikwa peke yako kama ulivyokuja.
Hopefully kuna walikutangulia wa kutosha angalau wakupokee huko utakapofikia.....but wait! Ukienda(kufa) unaenda kuanza maisha "mapya"! Au?!!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 9 October 2014

Kutoboa Mtoto Masikio(Kutoga)

Ni umri gani hasa unapaswa kumtoga Binti yako Masikio? Na je yeye kutoga masikio na kuvaa Hereni ni muhimu kwake au kwako wewe Mzazi?
Mie nilitogwa nikiwa mchanga (Miezi Sita) na nilichelewa, kutokana na Imani sijui Desturi ya mmoja wa Wazazi wangu ni lazima Binti wa kwanza atogwe na kuvalishwa Dhahabu.

Binti yetu alipofikisha Miezi 3 Baba yake akasema tumpeleke akatobolewe(Togwa) Masikio, mie nikapinga na ku-suggest kuwa tumuache na akikua ataamua mwenyewe kutoga au kutokutoga.
Nikaongeza, tena atakuwa na kitu cha ku-look forward to, mf: "nikifikisha miaka 15 natoboa Masikio".....kuliko tumalize kila kitu akiwa Mchanga halafu akikua tu tunaletewa Bf au Mjukuu kabisa sababu kila kitu tumekifanya akiwa bado mtoto.
Isitoshe (in my head) tunatoboa watoto masikio kwa ajili yetu wenyewe Wazazi, yeye mtoto wala hajali kama anavaa Hereni ama hana "kitobo" cha kuweka Hereni.
Baadhi ya Wazazi huku Ulayani wanachukulia kumtoga mtoto masikio ni abuse kwasababu hajui kwanini anaumia.....mmmh! Nakumbuka kwenye Kumtahiri Babuu, niliambiwa na Dokta wangu kuwa ni "abuse".....ikabidi tuende Private.
Aaah! Adha pekee ya kuzaa Kidume ni hiyo ya kushuhudia Kichanga wako "akikatwa" aiii mwanamke nililiaaaa sikujali cha Ganzi wala nini, kitendo cha kuona mwanangu mduchuuu "anatengenezwa"....labda akiaanza kuniletea Wakwe wa Kizungu hihihihi.
The thing is, kwa mtoto wa Kiume ni tofauti na Mtoto wa kike kwenye Kutoga. Kutahiriwa sio Urembo/Vanity ni Jadi/Utamaduni.
Alipoanza Nursery nkawa nahofia(ogopa) Carer wake atakuwa anamchunguza wakati wa kumbadilisha Nepi....maana hawajui kama watoto hutahiriwa wakiwa wadogo.....Ndio! Hihihihihi I am mwehu like that.

Babai.
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 8 October 2014

How to be Mum, Wife, HomeMaker and Blogger...

Mimi sijui!

Hihihihihihi huyooo unapenda kutafutiwa kisha wee unameza tu (copy and paste)!!
Mwanamke mwenye maisha kama yangu (not exactly ila kwa mbaaaali) unawezaje ku-keep up na Blog updates kila siku?
Sio blog kama hii ambapo sihitaji kufikiri bali natiririka tu. Zile ambazo unatumia akili kimtindo kwa kuvuta kumbu-kumbu (Uzoefu) na kufikiri.......aiiiii Imenishinda!
Basi nimefika nyumbani siku hivi, nawakilisha nilichoambiwa na Walimu wa Babuu.....Baba mtu wacha aanze kung'aka....."Mimi sifuati wanachotaka wao kwenye nyumba zao za Kizungu, nafundisha mwanangu nijuavyo mimi".

Nikajiuliza kwa hasira bila kutoa sauti....hihihihi "sasa ni kwanini tunampeleka mtoto shule ikiwa hatutaki kuwa kitu kimoja na Walimu wake?".

Nikasema....Asali wa Moyo, shuleni kuna Mihula (mipya imeanza August) na ili watoto waimalize vizuri, kuelewa na kwa wakati ni lazima Wazazi wa-work together na Walimu, vinginevyo mtoto atakuwa Nyuma au kuiona Shule Mbaya/Ngumu/Task.

Baadhi ya Wazazi wa Kiafrika ni waoga, mtu wa jamii ya Kizungu akikuambia jambo, unahisi kuwa anataka kuku-Zungu-rize Uafrika wako.

Badala ya kumfanya mtoto ajifunze kwa furaha akiwa comfortable na achague anachotaka kujifunza huko baadae....tunaishia kuwafanya watoto waione Shule kama "Task" na kuwa- confuse (Shuleni anaambiwa hivi, wewe unapinga unamwambia vile).

Unamlazimisha mtoto kujua mambo yaliyojuu ya uwezo wake ili aonekane na Akili sana Darasani, akishindwa unamuadhibu(bila kufanya uchunguzi kwanini hawezi)!
Au unaifanya Elimu yake sehemu ya Malipo.... "kasome kwa bidii ili upate kazi(pesa) utusaidie wazazi wako".

Niligombana na Baba (marehemu) sababu alitaka nichukue PCB, mie nkaenda kwingine kabisaaaa.....though niliipenda shule na mpaka leo napenda kusoma.
Sinilikuambia mie ni "AcademicHolic"....looking forward to my 50yrs birthday so I can do my PHD.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Friday, 3 October 2014

Blogger wapya!

Hellooooo*clear throat*....hi!


Kuna kipindi wana-blog (wapya) walikuwa wanasemwa sana, "kila mtu anaanzisha blog" baadhi ya Blogger wakaacha (mie nakaribia kuicha ile ingine maana.....takuambia siku ingine) hivyo naangukia kwenye "newbes" si ndio!!!
Kipindi naanza ku-blog 2005(kabla sijawa serious 2007), hao hao walikuwa wakilalama kuwa Watu (Wabongo) wapo nyumba, hawa-blog kama wenzao wa MBELE(hasa Wahabari na Watu mashuhuri).
Mara haooooo wote wakawa na Blogs(well baadhi).....kinachoKERA ni kuwa na habari zilezile bila kusema chanzo/Kielelezo.Mambo ya Beauty, Lifestyle, Fashion and News(kila mtu).
Aaah! Who cares....maisha ya kila mmoja wetu yapo tofauti na interesting in a way hivyo sio mbaya kuongea mwenyewe via Blog kwa matumaini kuwa mtu mmoja atasoma na kucheka au kujifunza.....asa uta-Copy vipi na Ku-paste mtindo wa Maisha na Uzoefu binafsi ya Mtu? Hihihihihihi lione!

Hata hivyo....Mbio zimepungua ila mizunguuko imeongezeka! Hivi nilikuambia Babuu kaanza shule (as if ni muhimu kwako hihihihi) anyway....basi mbio zimegeuka kuwa Mchaka-Mchaka.

Si unajua mizunguuko ya Mchaka-Mchaka? Bora mbio unakimbia mara moja unamaliza....kuliko Mchaka-mchaka.Tumbe: "Jua lile literemke mama aiyayaya iyaa iyaaa mama"......"Sijui nini na nini Pua kama Kijiko, Midomo kama Bakuli....nini na nini"!


Nikutakie Mwanzo Mwema wa Mwisho wa Wiki.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 30 September 2014

Lugha ya Mama kwa Mtoto...

Huku (UK) watu ambao tunaongea lugha zaidi ya Moja huwa tunashauriwa kuachana na "local" Lugha na kuwafunza Watoto wetu Lugha ya "mama".....in my case Kiswahili.
Kama kawaida ya Mzungu(anajua kila kitu)....wanadai kuwa Mtoto husika atajifunza "local" Lugha (Kiingereza) akianza Shule na hii itamsaidia Mtoto huyo ku-master "Lugha ya Mama vema".
Kwenye hili kuna Mawili muhimu(Kichwani kwangu): Mosi; Wanataka mtoto wako awe nyuma Darasani, kwamba akianza shule huku hajui "local" Lugha wanaoijua (wenyewe) wataendelea mbele wakati Mwanao anapoteza muda kujifunza.
Pili; Aki-master lugha ya "mama" watamtumia vizuri (hawatoajiri Mgeni wa Lugha yenu) ili kufanya kazi ya Kutafasiri na pia atakuwa kajifunza Bure(hawakulipi kumfunza M-british Lugha yako).

Kwanini nawaza/fikiri hivi? Well....Muingereza hana Lugha nyingine zaidi ya Kiingereza, iweje akuhamasishe wewe umfunze mwanao Kilugha chenu badala ya Kiingereza, akijua wazi Shuleni hakuna "Kiswahili" bali Kiingereza?!!

Nilikuwa a bit hard kwenye Kiswahili, nilitaka wanangu wazungumze Kiswahili lakini wakiongea wanaongea Lugha ingine.....nimeamua ku-relax na niwaache wazungumze "local" Lugha.

Pamoja na kusema hivyo bado najitahidi kuwafunza wanangu Kiswahili(sijakata tamaa). Mkaka(Babuu) anaelewa ila kutamka maneno bado kunamtatizo.
Mdada nae anaiga/rudia kila neno la Kiswahili usemalo which ni dalili nzuri.
Oh Jana, nikakutana na Site yenye Methali za Kiswahili.....the excitement niliyoipata sasa! Ni kama 2002 nilipoingundua DHW/DHB(very 1st Tanzanian Forum ya Kiswanhehe)."Mwenda Tezi na Omo Marejeo ni Ngamani".

Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 29 September 2014

Nanyanyapaa au na-practice

Freedom of expressing my view? Sijui...


Alikuwa Mwanaume, akaathirika Kisaikolojia kwa kuishi kwenye Mwili wa "mwanaume" wakati yeye anajijua na kuwa ni Mwanamke.
Akaoa na kuzaa ili kuficha "tatizo" lake....akashindwa kuvumilia akawa anaibia Mavazi ya Mkewe na kujiremba mkewe akiwa hayupo nyumbani.

Anapenda urembo na kuvaa kama mwanamke, baada ya Miaka kadhaa akaomba "Shirika la Afya" ku-fund Upasuaji ili abadilishe Maumbile na Jinsia na kuwa complete au legally "Mwanamke" .

Ombili lake likapita kwa "ground" ya Kuathirika Kisaikolojia na asipofanyiwa Upasuaji(kubadilishwa Jinsia) anaweza kuji-harm.....so akanza Tiba ya Homono, baada ya Muda akabadilisha Jinsia na Documents zote zikabadilishwa kutoka Mwanaume kuwa Mwanamke.
Sasa amepata Mpenzi mpya na anampango wa kufunga nae ndoa, Mpenzi huyo ni Mwanamke.Anadai kuwa anavutiwa sana na wanawake hihihihihiihi which make him a real Man(in my head....mmh naturally)!
Wananchi wanadai Pesa zao(Kodi) zilizotumiwa na Shirika la Afya kumbadilisha Jinsia Mwanaume kuwa Mwanamke.
What a confusion Planet!!! Or I should ask, why complicate your life eiiii! Hii ikitafsiriwa nitashitakiwa kwa Unyanyapaaji dhidi ya Transgenders.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 25 September 2014

Bank Kuu Tz na Gmail account...REALLY?!!

Huenda wana account yao Official ambayo inawawepa mahali pazuri KIUSALAMA online.

Nimepokea Email kutoka Bank Kuu ya Tanzania, ikinipa tahadhari kuwa nisipobadilisha "Details" zangu via Link waliyoiweka basi sitoweza ku-Bank Online na Bank yeyote Tanzania!

Nikaenda kwa "sender" nikaona mtumaji ni "blablabla BankOfTanzani@gmail.com".....nkacheeeka halafu nikapachika tusi!

Kwanza mimi siBank na Bank yeyote Tz online, Halafu huwezi tu kuwaambia watu wabadilishe "details" zao via link, kwa sababu za Kiusalama kila mtu angepata taarifa hiyo kwenye account yake ya Online ambapo anaingia kwa kuweka "details" ambazo ni zaidi ya jina lake na Namba ya Card, yaani za "siri" na ni yeye tu ndio huwa nazo na hubadilika kila unapo BankOnline.

....aiiii naona nazungumzia System ya huku na sio ya huko Tanzania ambayo siijui.
Nachojaribu kusema ni hivi;- Kama ilivyo kwenye Kutongozwa kuna Maharage ya Mbeya na Maharage ya Kigoma....Watu tunatofautiana, kuna wale wanao-panic haraka so wataenda na kuweka "details" zao kwa hao Scams!

Halafu kuna akina sie ambao kabla ya yote tunahoji na wepesi kwenda Bank na kuwauliza kulikoni?
Najua kwa Watanzania wengi ku-bank Online ni kama "status" ya kuendelea....ni kama vile watu kukimbilia kuBank na Bank ya Nje (kwa status reasons) badala ya kubank na Local Bank.

Well hata mimi na Bank na Bank ya Marekani na Ya Honk kong sio ya UK.....nadhani bank zote za UK sio za UK, hata (niliambia wakati wa Yes/No reforandamu Kampeni) Royal Bank Of Scotland ni ya Down under.....so naezajitetea SI kwa STATUS reasons.Babai.
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 24 September 2014

Misinformation za Online nazo.

Hellooooo!


Urahisi wa kuweka chochote online kwa nia ya ku-share au "kuelimisha" wengine ni mzuri sana!
Sote tunajua kuwa kwenye kila kitu kuna Faida na Hasara zake, kama Mwanadamu unatakiwa kupima na kufanya uamuzi kwa kuzingatia faida zaidi (utafaidika?).

Sio sote tuna-share yote(kila kitu) online....kwenye Blog ya D'hicious nimeshare mengi tu ila sio yote nijuayo (mengine naweka kwa ajili yangu mimi binafsi) na Binti yangu na Mwanae huko mbeleni Ntakapo kuwa Proper Bibi.


Hali kadhalika kwenye Blog nyingine Mf za Urembo, Fashion hufanya hivyo pia....tena hawa huwa hawabani some info, wanakudanganya kabsaaaaaa(wanapindisha ukweli) ili uogope au ukosee na hivyo usitokee as Mrembo kama wao wanavyoonekana au Nywele zako zisikue kama zao.


Safari yangu ya Nywele (nilishawahi kukuambia about) imenifanya nijaribu Mengi, kukosea Mengi na Kujifunza Mengi halafu nikarudi kwenye "rutini" yangu ya enzi ambayo kabla ya YouTube na Blogs za Nywele na Afya ya nywele zangu imekuwa njema.....(The new thing kuongeza Oils kwenye Conditioner).

Narudia tena, usichukue kila unachosoma online kama kilivyo, pima Faida na Hasara....kama ni Tiba(Madawa) au Afya ni vema kuangalia chanzo chenye uhakika Mf: site za Hospitali au Shirika la Afya, kwa huku nilipo NHS.com ina info nzuri sana kuhusu Magonjwa yote, yep Mpaka Ebola....sio Blogs ya mtu anaejiita Doctor(could be anybody).


Story time:Nilipoanza Kazi miaka ka' 20? Iliyopita....sikumbuki(tafanya hisabati baadae)....anyway! Niligundua kuwa ile Makala nzuri sana ya Urembo iliyokuwa inaendelea kwenye Gazeti Fulani na "mmiliki" alikuwa Mwanamke(kwa mujibu wa Picha na Jina).....kumbe MUANDISHI wake alikuwa Baba mtu mzima na hakuwa Mtanashati, alikuwa a bit rough(hajipendi)!


Sasa linapokuja suala la Afya yako au matumizi ya Madawa hakuna "Trial and Error" kama kwenye Urembo(utanawa) au Nywele(utazikata)Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 23 September 2014

Kabla ya Mobile Simu na Net....

Ulikuwa unafanya nini na muda huu unaotumia Simu yako au Mtandao eti?!!


Jinsi Teknolojia inavyozidi kukua ndivyo ambavyo maisha yanazidi kuwa busy na kuhisi muda haukutoshi (Masaa 24 yamekuwa machache).Binafsi nilichukua hatua ya kutoka Mtandao mmoja wa Jamii na Kujiunga na ambao ni latest one (Mwisho ilikuwa Twitter karibu Miaka 5 iliyopita) hivyo sikuwa kwenye Mitandao Saba ambayo ingenichukulia Muda wangu mwingi.
Kabla ya hapo hakukuwa na Mitandao ya Kijamii, kulikuwa na Forums na Chatrooms pamoja na kuwa nilikuwa na Muda mwingi bado sikujiunga na kila Forum/Chatroom iliyojitokeza.Hapa juzi nimemsikia Business Woman akisema ameamua kufuta Email address yake na baadhi ya namba za Simu za Ndugu, Jamaa na Marafiki wasio na Mpango (wasiomsaidia kwenye Biz yake) ili aweze ku-focus zaidi kwenye Uzalishaji na Uendelevu wa Kampuni yake.

Anadai kuwa Teknolojia ya Smartphone imesababisha yeye kupoteza muda mwingi kujibu Mails ambazo hazina umuhimu maishani mwake, hivyo akazuia kuzipokea, lakini akawa anapata lawama kila anapokutana na Ndugu, Jamaa na Marafiki....hiyo ikamsukuma kuifutilia mbali "account" yake.

Nimesoma hiyo Wiki mbili baada ya mimi "kupumzika" kwenye ile Blog yangu ingine ambayo husababisha mimi kupokea Mails za kila rangi ya usumbufu na Lawama kwanini sijibu mail "binafsi"(sijui hawaoni kuwa D'hicious sio blog ya kurafikiana)!

Sasa leo hii nina "kajeshi" ka' watu wa Tatu(watoto na Baba yao) ambao ni muhimu maishani mwangu. Wawili kati ya hao (watoto) wanahitaji kufunza HISABATI (nalia sana kila nikifikiria Hisabati).
Nahisi kama muda umefika wa kuifunga ile Blog. Wee unaonaje?


Babai...
Mapendo tele kwako...

Monday, 22 September 2014

Binti "akiharibika" arudishwa kwao....

...ambako hajawahi kuishi (hajakulia) huko maisha yake mapya ya "ukubwani hivyo kuwa Mgeni.

Hii tabia mie huwa inanikera sana, enzi zile nakua nilikuwa nasikia tu watu wakisema "aah fulani, kashika mimba nimemrudisha kwao" au "amelimbukia sana maisha ya mjini, nimerudisha kwao".

Unapochukua mtoto wa Mtu akiwa Mdogo kwa nia ya Kuishi nae kama "msaidizi" (which ni kinyume cha Sheria) au kukubali jukumu la kulea mtoto baada ya Wazazi wake kutangulia(Kufariki) unapaswa kuendelea kuishi nae na kumpa support/saidia ili arudi kwenye "mstari" sio kumpeleka "kwao" ambako ni Mgeni!

Pia sio haki kwa watu wa kule "kwao" kubeba "Mzigo" ambao wewe Mlezi ndio uliyesababishwa kwa maana moja au nyingine.

Unalea Binti tangu anamiaka, tuseme sita....tabia atakazokuwa nazo ni matokeo ya Malezi yako, hivyo ikitokea "kaharibika" Hatia ni yako, sio ya watu wa "kwao".

Usimwambie mtu: Wengine huwarudisha mabinti wa Watu kwao baada ya kuhusika kwenye upatikanaji wa Mimba aka KUHARIBIKIWA.....

Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 16 September 2014

Watoto wanahitaji role Model sio Model!

Ah! Nimekua busy kweli....unajua umri ukienda Majukumu yanazidi/yanaibuka kila kukicha.

Hapana sio majukumu kuhusu Watoto, Baba yao na Bills ni majukumu ya kuutunza Mwili na Uso ili kurudisha Miaka nyuma. Si nilikuambia by the time nafikisha Miaka 40 nataka kuwa kama Gabriel Union!! (Au niliota tu?).

Nataka wanangu wawe proud of my "look" nikienda wadondosha na kuwachukua Shule hihihihi....sio wakikuona tu wanakimbia kwa aibu au wanasema "that's not my mummy, she's my Shangazi/Bibi".

Eh! Nilipokuwa Msingi kuna mdada mmoja (sasa maarufu kwenye MaTv huko kwenu) alimkimbia Mama yake, tena akawa analia kabisa kuwa yule sio Mama yake....si wajua Mama wa Kinyakyusa alietoka Mbeya beak ya kwanza Shuleni hihihi hi akina Mwakaninini(naambiwa ninyi ni watani wangu upande wa Mama so usi-panic)!
Eti "Children need role model Not a Model"....wacha uvivu, hebu jipende huko.....you can be both!


By the path I AM FAR FROM a MODEL na nikijiremba sirembeki.


Babai!
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 10 September 2014

Mwanaume ka' Mwanamke na Nyumba Ndogo!

Only Mwanaume husika akifanya jambo baya, la kizembe au akionyesha "emotions"! Mfano akisema ukweli pasipotakiwa (Umbea), akilia baada ya kuumia, akizimia Msibani (Wanaume hawazimii, huwa wenda wazimu hihihihihi) n.k.

Tabia hiyo huwafanya Watoto wa Kiume kuwa na Tabia mbaya za Baba zao, kwasababu wanaogopa au hawataki kufananishwa na Wanawake.


Kwenye Jamii yetu (Tz) Baba kuwa na Kimada siku hizi imekuwa suala la kawaida, jamii imelikubali hilo na kuwapa jina zuri eti "Nyumba Ndogo" which is sooooooo annoying, Yaani ndio kukata tamaa au?!!

Sasa nyumba ndogo huwa haijengwi kwa siku moja, na mara zote Mtoto wa Kiume huwa wa kwanza kujua ikiwa Baba ana Kimada.....Vijana hujua mengi sana Mtaani/Vijiweni.

Wengi huwa wanaumia kuona kuwa Mama zao wanakuwa cheated na Baba zao lakini kwa vile wanaogopa kuitwa "Wanawake" wanaamua Kuuchubua (do you still use this word??).

Baadhi ya Vijana (watoto wa kiume) husika huamisha maumivu yao "emotionally" na kujenga Hasira na Ukaidi dhidi ya Mama zao (hawawaheshimu tena) na huwakwepa Baba zao.


Kwanini Baba anashindwa kumheshimu mama na kwenda kuwa na mtu mwingine nje ya Ndoa? Au Kwanini Mama anamuachia Baba amtende....hapo ndio inakuja sehemu ndogo ya "Wanawake sio Imara" au "Dhaifu"....

Hakuna mwanaume anataka kuwa Dhaifu! Kila mwanaume anataka kuwa Jasiri na Imara.....

Hii hubaki kichwani na wao kufanya walichofanya Baba zao, matokeo yake "Nyumba ndogo" imekuwa the new Norm!
In My Head....hii haina Uchunguzi wala Utaalam wala Uzoefu.

Babai
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 9 September 2014

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!!


Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana!

Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima.

Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu).

Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!!

Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu".

Kaongeza: "Vumilia tu mwanangu, ndio Ukubwa huo, Vaa Bra kusapoti Uzito".....anyway baada ya Wiki yakaanza kukauka na kurudi yalivyokuwa kabla sijazaa.

Sasa leo nimeamua kumuachisha Binti yangu, yaani hakuna ku-give in.....atalia, atarusha tantrums (maana ni kabingwa) walaaaa sijali.
Haya ni pale Mshauri anapoomba Ushauri....anyone?!!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Friday, 5 September 2014

Mungu ni wa Afrika tu?

Umewahi kujiuliza kwanini sisi Waafrika Mataifa Mengine ambayo ni Masikini kuwa pamoja na kuamini Mungu na kusali kwetu kote bado hakuna Maendeleo?


Kwanini Mataifa hayo yanaendelea kuwa Tegemezi wa Nchi za Ulaya Magharibi na Marekani?(Wacha sababu za Kisiasa na Historia hapa sio mahali pake)....


Leo hapa (kwako itakuwa Jana) Mimi na Asali wa Moyo tulikuwa tunajadili kuhusu Ubinafsi wa sisi wanadamu, tukafikia mahali tukakubaliana (kwa kawaida huwa hatukubaliani)!


Wazungu ni Washenzi kote-kote na wengi wao hawaamini Mungu as in kusali kucha kutwa na kwenda kutoa Sadaka kanisani kila J'2 lakini linapokuja suala la kusaidia Binadamu wengine wenye Matatizo huwa mstari wa Mbele!


Huenda hilo ndilo linalowafanya waendelee kufanikiwa, kwamba hawakai(kupoteza muda) kusali na kutegemea Mungu awashushie Mahela ili wawasaidie wengine au kukesha na kuomba ili Mungu awape Makazi wakimbizi mahali palipo na Vita.


Wanafanya yote hayo kwa Vitendo.... kuna Maduka kibao ya Misaada ambapo watu hujitolea vitu ambavyo hawavihitaji tena(Mitumba) na kuuzwa ili kusaidia Masikini wa Nchi zinazoendelea, Waathirika wa Vita n.k.


Pamoja na kuwa watumishi wa juu sehemu hizo za "misaada" hupata faida bado sehemu kubwa ya mapato ya "Misaada" inakwenda kwenye "kusudio".


Pia kuna wale ambao hujitolea kwenda "umasikinini" (Nchi zinazoendelea) au Vitani kusaidia Wakimbizi.


Ndani ya Nchi husika iliyoendelea kuna "Vikundi" kibao vya kupigania Haki za watu ambao hata hawawahusu, mf; Kusaidia watu wasio na Makazi, Kusaida wanawake wenye matatizo, Kusaidia "fund" kwa ajili ya wagonjwa wa Saratani na Uchunguzi ili kupata Dawa n.k.....ndio wanapata Mishahara mizuri lakini kazi zao zinatekerezwa na Matokeo yanaonekana.


Wote hao hawakeshi na kuomba kwa Mungu, bali wanathubutu na kufanya sehemu yao kwa Akili na Nguvu zao walizopewa na Mungu(niaminivyo mimi).....Mungu anawarudishia Baraka Zaidi ndio maana wapo hapo walipo(in my head).

Angalia Ebola(kwa mfano) inavyotupelekesha Afrika, halafu tunakesha na kukemea "pepo la Ebola toka kwa Jina la Yesu" aliekuambia Ebola ni Pepo nani?.....na bado unasubiri Mzungu akuletee Dawa....Madaktari wa Afrika na Serikali zao walikuwa "Wavivu" kufanya research tangu Ebola ilipo ibuka Demokrasia ya Congo kwa mara ya kwanza?......Aiiii nimeingia kwenye Siasa sasa, wacha nifunge Simu.

Furahia Mwanzo wa Mwisho wa Wiki yako...

Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 4 September 2014

Na-admire sana watu wa Medical...

Nakupenda kwa kuichagua Blog hii...

Unajua wale wadada wakubwa inatokea unawapenda, unatamani kuwa kama wao (Kielimu) utakapokuwa Mkubwa?!!


Mie nilikuwa nawapenda sana Wadada Wanasheria, Waandishi wa Habari na Young Docs (au tuliwaita Medical assistants sababu walikuwa hawajafuzu).....sasa kuna mmoja alikuwa jirani yetu enzi hizo bado kabinti, alikuwa anasoma Russia.


Kwasababu alikuwa Mkubwa sana kwangu hatukuwa na utaratibu wa kuongea lakini tulikuwa karibu sana na alionyesha kunipenda kweli-kweli!


Kila J'Mosi alikuwa ananiita "Dinah Mdogo wangu unakazi?(Za shule)... ukimaliza naomba uje unikwangue Mba"!! Usicheke tafadhali (hihihihihihihahahahahaha)...Basi mwenyewe nafurahi naenda kumkwangua "dada MA" Mba....honestly!!!


Namkwangua, nikimaliza nampaka mafuta halafu namsuka....heee! Najua kusuka blaa tangu nina miaka 7 shukurani kwa Bibi na MSesere(Doll) wangu....nika-master Kusuka Mitindo nilipofika miaka 15 hivi....by 18 nilikuwa nasuka watu kwa Hela including Dada mMedical Assistant baibeee (Nimeanza kujitegemea kiuchumi kitambo ujue!).


Sifa kuu ni kuwa nikimsuka mtu simvuti/umizi ngozi na nywele zake hazikatiki akifumua....SISUKI watu usijedhani najitangazia Biashara bure!!


Baada ya Muda Dada akawa sijui "MD" sijui nini nini na akaolewa, akahama na kuhama....bado na admire sana Medical People, Naomba sana wanangu waje kuchagua kusoma Medicine.


Napenda Proper Degrees, sio zile useless zile sijui ninininiLogy zile....ah nimepoteza Track ya nilichokuwa nazungumzia.....Hebu nikumbushe!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 2 September 2014

Nguvu ya Mama....

Sio aliekuzaa bali uliezaa nae (Mwanaume) na wewe Mkimama mwenye mtoto au watoto.
Embu ngoja kwanza!!....Mama aliekuzaa ndio chanzo cha ninachotaka kusema hapa siku hii ya leo.
Nilibahatika kulelewa kwenye Mazingira ya Imani Kuu Mbili za Dini (Wazazi walikuwa na Imani tofauti za Dini), hali ambayo ilitufanya watoto kuwa na Dini ya Baba mpaka tulipofikisha Umri wa Miaka 18!!!

Aiii.....angalau tulikuwa na kitu cha ku-look forward to....errr 18th birthday na 1st Key for your own house au kuanza kulipa Kodi ya chumba unacholala hapo kwenu (nisikuchanganye na mambo ya Ulayani).

Kabla ya Miaka 18 sote tukahamia Dini ya Mama...Mzee akabaki peke yake na Dini yake masikini.....hapo ndio "nguvu" ya mama inapokuja sasa.

Mama akiamua watoto wasitambue baadhi ya Ndugu anaweza kufanya hivyo kirahisi kabisa na kufanikiwa.

Mama akiamua kumkufanya mtoto amchukie Baba yake anaweza kufanya hivyo like pie!
Mama akiamua kukuambia au asikuambie ukweli kuhusu Baba yako halisi anaweza kufanya hivyo pia.
Kitu muhimu ambacho wanaume hawajui au wanasahau ni kutambua kuwa unapofanya Ngono bila Kinga na Mwanamke kushika Mimba, unakuwa umempa "POWER" juu ya mtoto atakaezaliwa, Maisha yako na Bank account yako (kwa wa mbele).

Nawee mwanamke utambue kuwa unaposhika Mimba uzembe ni wako kwasababu unamamlaka na Mwili wako (wacha mambo ya Mimba yake BS) ila wakati huohuo unakuwa umepewa "POWER" juu ya Mwanao hivyo itumie vizuri kwa Manufaa ya Mwanao.


Ni watoto wachache sana ambao huegemea upande wa Baba zao na most ni kwababu ya "pesa" au Tamaa ya maisha fulani.

Nawapenda wazazi wangu wote na nilikuwa "dad's girl", ila namsikiliza na kumuamini Mama yangu zaidi. Sina hakika kama hii inauhusiano na ku-share damu na mama kwa Miezi 9?!!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 1 September 2014

Raha ya Tako Kubwa kutikisika...

Sanaaa ila sio kila siku though!


Kuna siku mwanamke unahisi hitaji la "kikaza" Maungo huko nyuma katikati....maana mtikisiko unazidi kiwango cha kawaida(au ni mimi tu?!!).


Kwa wale ambao hatukujaaliwa "Choo" huwa hatuvai "kyupi" ili kuongeza "mtetemeko".....lakini waaapi bana, kitako kigumuuu ka' Jiwe.....ila angalau halipo. Sasa usiombe uwe umebebeshwa "lichoo" halafu halitikisiki!!
Au linaenda Ti------Ti-----Ti badala ya "SingidaDododoma-SingidaDodoma"

Anyway! Kama wewe huna "Litako" na ungependa mtikisiko time to time (pale unataka attention) bila kubadilisha mwendo na kuendelea kuvaa "kyupi" yako.....Hongera sana kwa kuichagua Blog hii hihihihi!

Unapotembea mbele ya "mhusika" achia sehemu ya Haja kubwa kama Vile unataka "Kushusha Mzigo".....Hakika tumbo lako liposawa maana.....!!!
And oh....unafanya hivyo ukimkaribia Mlengwa, sio Siku nzima...utajaza mahewa tumboni!!

Babai.
Mapendo tele kwako...

Friday, 29 August 2014

Ijumaa moja Baada ya Mauaji ya MwembeChai!

Maisha haya!

Nimekumbuka 1996/97 Mauaji ya Mwembe Chai (siku mbuki vema na sitaki ku-google vilevile)!

Siku chache baada ya Mauaji yale bado kulikuwa na Maandamano ya Siri ya "Waislamu wenye Hasira".....Kile kifo cha yule Kijana pale Mwembe chai akianguka LIVE baada ya kupigwa Risasi na Polisi (FFU sijui) akiwa amevaa shati la Bluu Mpauko(light Blue) kamwe haitonitoka Kichwani! Ni kifo cha kwanza nilishuhudia live(on Tv)!!


Sasa bila kujua si tukaenda Kariakoo siku ya Ijumaa! Ile tumemaliza manunuzi si tukakutana na Waandamanaji na FFU...wakayaachia Mabomu ya "Machozi"....oh boy! Nilihisi Vita kuu ya Mwisho wa Dunia ambayo sina Uzoefu nayo ndio imefika!!!


Kimbia, huku na kule mara Tukakutana na jamaa (sijui Katibu au Mlinzi, ila alikuwa Mhindi) Wa SSC pale Msimbazi, akatufungulia Mlango kwenye Jengo la Simba....akawa anaita akina Mama na Watoto waende kupata Huduma ya kwanza....hihihihi kunawishwa Maji Usoni(wasn't a laughing matter then)!

Anyway! Baada ya hapo kukatulia, tukatolewa nje ya Jengo la SSC kwenda kupata Usafiri....kwenye Daladala! Tulikuwa tumepanda na baadhi ya Waandamanaji!

Akamuuliza Mzee mmoja na Kanzu yake...."Baba na wewe ulienda K'koo kuandamana".....Mzee akajibu "ndio mwanangu, tunapigania haki yetu"....Mdogo wangu akaulia "una watoto"...yule mzee akasema Sita na wote wapo Sekondari.

Mdogo wangu si akaanza Risala sasa? "Wee Mzee mzima badala ya kuhangaikia maisha ya wanao na kuboresha maisha yako, unaenda kupoteza muda kuandamana. Sasa kwa bahati mbaya umepigwa Risasi umekufa au Bomu umekatika Miguu nani atatimiza mahitaji ya wanao?"

Akaendelea "Wazee wengine hamfikirii, mnakuwa wabinafsi sana na Dini zenu, Pigania haki ya kupata vifaa Mashuleni, sio Dini"

Mie hapo nywiii(kimya) bado natetemeka huku nafikiria Mabomu ya Machozi yataniathiri vipi huko mbele, sikuwa na sauti wala nguvu....ujue mie ni Muoga mnoooooo linapokuja suala ya kuingiza mahewa, madawa, sumu mwilini mwangu!!

Ah! Mauaji yanayosababishwa na Dini hunisikitisha sana.


Mungu amrehemu yule Kaka alieuwawa pale Mwembe chai.

Heri ya Mwanzo wa Mwisho wa Wiki.

Bai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 26 August 2014

Kujikanganya nako!

Kuna siku nilisikilizishwa Nyimbo za Bi Rozi Mhando akizungumzia "Kunyang'anywa" Mali zao na Wageni..."Wao kuwa Wageni Nchini mwao".
Aliendelea na kuimba kuhusu kuchukua na Kunyang'anya vilivyo vyao kwa Jina la Yesu!.....Nkajiuliza Kunyang'anya(kutumia nguvu) si ni Dhambi?!!

Halafu nikakumbuka Ubunge ni Career Path kwa watu Mashuhuri ila issue nzima inayonifanya niandike hapa ni ile ya kuji-contradict!!

Isitoshe kuwa Mlokole kwa Miaka zaidi ya 20 lazma utarudi nyuma (utachoka) kumsubiri Yetu (hihihihi my ribs... Wapendwa na Watumishi habari gani?) na hivyo kuhama Kanisa, Kuanzisha Kanisa Lako au kujiingiza kwenye mambo mengine ambayo ni tofauti na Misimamo yako.

Si walokole tu wanaoji-contradict kwa kukataa "Mikorosho" lakini wakati huohuo Kumuita Yesu ni Mume wa Wajane (Wajane sio Wanawake tu kama ulikuwa hujui, kuna Wajane wanaume) kwa mfano tu!!

Kujikanganya ni kitu cha kawaida ailimradi sio kwa wakati mmoja na kumbuka kuepuka unapobishana na Mumeo/Mkeo au kwenye utetezi wako Mahakamini (siku ukishtakiwa)....!

Mwanadamu unapitia maisha tofauti na ni vema kujaribu kubadili Maisha yako au misimamo yako(ikibidi) ili uweze kufanikisha Lengo fulani ambalo ni muhimu kwako na pengine familia yako au Career si eti!

Mimi mwenyewe najikanganyaga hapa kama ifuatavyo.....unaikumbuka ile Post kuhusu SAHM (Stay At Home Mum) aka Mama wa nyumbani! Unadhani miaka 6 iliyopita ungeniambia siku moja nitakuwa Mama wa nyumbani ningekuelewa?!! Lazma tungepigana.

Ni kazi ngumu sana tu lakini inanifanya nifurahi Moyoni kuwa wanangu hawapo mikononi mwa mtu/watu wengine bali mimi mama yao ninaejua Uchungu wa kuwasukuma nje ya Mwili wangu!
Kwanini nawaita W****ge "Mikorosho"? Errr is it kwasababu Korosho imepinda au kwasababu Mikorosho inapadwa....chagua utakalo na ufaje kuwa Jawabu.Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 25 August 2014

Kizazi cha Santuri, Kaseti CD Vs MP3...

Nimekatiza mahali mtaa wa ki-Posh nikakutana na "Bei Nanini CafE" haraka haraka akilini ikaja "Price and what's not"....not exactly what they meant ni mimi tu na Utamu wa Kiswahili.....liwache hili!

Unakumbuka enzi zako ulipokuwa unakuwa miaka ya 92+ hapo ndio Tv zinaanza kuchanganya(sio Vituo) bali watu kumiliki Tv(wageni wa Jioni wakapungua nyumbani kwetu).
Kila ulichokuwa ukifanya Mzazi wako anakukatalia akisema "enzi zetu tulikuwa hivi na vile....sio nyie watoto wa siku hizi"!

Halafu unatamani kumuambia "sasa Mama enzi zako si zimeisha, hizi zetu" lakini huwezi, unaishia kununa.

Nakumbuka Baba(Marehemu) alikuwa anasema "hivi huko Madukani hakuna nguo za wakubwa, zote ni za watoto tu?" Akimaanisha zinabana au fupi!....tukamwambia "Baba hii ndio mitindo ya kileo".....alisema "vaeni mtakavyo lakini mkija Ofinisi kwangu sitaki kuona chupi ndefu" (Suruali za Kubana).

Je! Huoni kuwa na wewe umekuwa kama wazazi wako? Kutwa kufananisha enzi zako na enzi hizi....Lione vile!(Hihihihi).


Akyanani vile mie nimekuwa ka' wao....ila tofauti yangu najikumbusha mwenyewe kuwa ule ulikuwa wakati wangu na huu ni wakati wao.

Wali kizazi cha Santuri, Mie Kizazi cha Kaseti, wao Kizazi cha Mp3 wapi na wapi?!!!!.....Dinah funga Domo lako muda wako wa Kaseti?!! Kaseti kweli si nimezikuta mie! Nadhani mie ni Kizazi cha CD....(Nimesahau jinsi ya kumalizia hapo).

My 3yr boy aniambia "mummy you are useless on games, let me show you how to play"....hiki kizazi cha Code ni balaa asavali cha Mp3!!!Cheers!
Mapendo tele kwako...

Friday, 22 August 2014

Kizazi cha Miaka ya 90!

Na haraka zao!! Yaani wapo mbio-mbio tu japo mbio zao zinatofautiana.....kuna wale wa starehe(Now) na wa maisha yajayo(Future)!!

Mdogo wangu wa Mwisho anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Nilipopata habari za yeye Kuposwa nilipata hasira za ajabu!

Nikabaki nalalamika "yaani mdogo wangu mdogo hivi anaolewa"...."Vipi huyo mwanaume akienda kumtesa"? "Kwanini asisubiri kidogo jamani akue (huku nalia) bado mdogoooooooo" she's 23yrs!

Mama akaniuliza(Simuni), ningekupa taarifa kuwa anamimba au kazaa ugelia kiasi gani?!! Kabla sijajibu!! Asali wa Moyo nae akauliza swali hilo hilo(live).....nikasema but she's my little sister....can she just wait another 2yrs?!!!

Anyway, ilinichukua mwezi Mzima kukubali kuwa my baby little sister-o anaenda kuolewa!!


Sasa leo naongea nae, ananiambia "nipo site dada" Nkauliza Site ya maandalizi ya Ndoa? Akanijibu "Hapana Da Dinah, tunajenga"!!

Nkajisemea D'oh! Watoto wa 90s wanakua haraka Kiakili kuliko akina sisi the "tumuachie Mungu one day Yes"....the shenzi!!!
Tena afadhali sisi the Shenzi, kuna kile Kizazi cha 1951-1973 Oviooo yaani the Bongolala kabisa!!

Usijumuishe maelezo yangu ukapata Kiburi au ukapata hasira, sio watoto wote wa 90s wanakua haraka kiakili, inategemea na Mtu, Mazingira, Malezi n.k.Nikuache kwa sasa!
Mapendo tele kwako...

Thursday, 21 August 2014

Nimeachwa na Teknolojia...

Ah! Nimebanwa kweli siku mbili hizi....ila nafurahi kuwa nimepata muda wa kuongea na wewe kabla sijaenda kulala.....mmh! Tangu nimekuwa Mama wala hakuna kulala ni kujilaza tu.

Kuna tuwimbo tuwili twa Ali Kiba tunanikuna kweli yaani "Mwana Daslama" na "Kimaso" ingekuwa zile Kanda za enzi ninge-rewind kwa Penseli mpaka Kanda ikatike....ujue kuna Wasanii wa Bongo Flava halafu kuna Ali Kiba(I just love that Kid). Achana na hili.

Jana nikaenda Dukani kuangalia Simu....Teknolojia imenishinda au niseme tu imenipita!

Simu yangu ya mwisho ilikuwa (usicheke) Blackberry Bold 9900, ikatumbukia chooni (umama siku za mwanzo uliniCost!!!).

Siku naenda mtembeza mwanangu City center kwa mara ya kwanza si nilipanda Treni heheheheheeeeeeee mwanamke nashuka na "Pram" lenye Mwanangu obviously!!....nikaacha Hand bag kwenye Treni(walinirudishia though)!

Turudi kwenye Teknolojia ya Simu, wala siamini kama nimekaa Miaka 3 bila Simu Mpya....nilikuwa nabadilisha simu kulingana na Toleo jipya la Teknolojia kwa mwaka huo.

Baada ya kujiona "mshamba" wa Technolojia nimeamua niingojee hiyo Sa-Msang'i inayosemekana ni bora kuliko iSimu6.Nikuache kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 19 August 2014

Mtu chake...

Kwa kawaida mimi sina tabia ya kuangalia watu ninapokuwa natembea na hata kama nimekaa mahali nitakuangalia kama nimependa ulichovaa....na kuangalia kwenyewe ni kwa Sekunde chache tu.


Kuna watu wanajua kukodolea macho wenzao bila kupepesa! Yaani anakukazia macho mpaka unaona aibu kwa ajili yake!

Ukitaka ugomvi na watoto wa London wale wa Uswahilini bana wakazie Macho hivyo....anakufuata na kukuuliza "what you looking at?" huku kashikilia Kisu!

Kisu bit pale juu nimeongezea tu chumvi, ila kuna vipigo na vifo kadhaa vilitokea kutokana na mtu kumkodolea macho mwenzie.

Stori time: Sasa jana tupo mtaani tunatembea na watoto....nyie mnatoka Weekend sie twatoka J'tatu....kisa na sababu? Ili tusiwe sawa, hakuna lingine wacha kutuJAJI eeh!

Nasikia Asali wa Moyo analalamika "mijaume ya kiafrika sijui ikoje (yeye mwenye Muafrika) inamkodolea macho mke wa mtu wakati inaona kabisa yupo na Mtu wake"

Hee! Nkauliza kwani wewe umeonaje kama wananikodolea macho kama wee mwenyewe hujawakodolea?!!

Akanijibu kwa kifupi, "mtu chake"!....nkafurahi Moyoni kabla sijajiuliza maswali kadhaa kuhusiana na yeye kuwa Mwanaume wa Kiafrika!


Asali wa Moyo akampeleka Babuu kwenda kuangalia makorokocho(Toys), mie nkawa nimekaa sehemu na Kibibi(kabinti) nampatia Lishe.....Mara akaja Mkongo, akaomba direction, nkampatia kisha akasema "ningependa kukujua zaidi, nikupe namba yangu?" Nkasema akuu sina Simu mie.Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 18 August 2014

The why's!

Nilijua siku nikizaa mmoja kati ya wanangu (au wote) watakuwa waongeaji sana kama errr Mimi?!!

Well, najua kuwa napenda kuongea (labda kwa vile sinywi pombe au sina nguvu ya kupigana) lakini sio muongeaji kihiiivyo.

Nakumbuka Marehemu Baba alikuwa anawaambia watu "aah kuwa makini, binti yangu huyu anamaneno sana".

Kiukweli kabisa na admit mimi ni Mbishi sana....nope! wala sina asili na watu wa Kibondo, Kigoma! Labda kwa vile sina Nguvu za kupigana lakini wakati huohuo sipendi kuonewa, sipendi kudanganywa na siamni katika "kubali yaishe" BS na wala sio "ndio bwana"....sasa nikiwa na uhakika na ninachokisema nitakubishia mpaka kesho muda kama huu.


Turudi kwenye uongeaji ambapo ndipo Babuu(my 1st born) anapokuja sasa....Laaaa! Mwanangu anaongea jamaniiiii....akianza stori zake....halafu ana "why's" za kutosha.

Maana nilikuwa nahofia Hisabati akianza shule, sasa nina shughuli ya kujibu why's.....wakati mwingine mtu hujui hata jibu halafu huwezi kumdanganya, basi unabaki bikozi izi eh...I will google, I mean tell you when we get home!!!
Mbaya zaidi why's zake wakati mwingine ni ngumu(halafu mbele za watu)....hivi hapo ulipo bila kufikiria unaweza niambia kwanini tunapata Kwikwi (....toa jibu la Kibaiolojia kwa Kiinglishi)!

Ujue swali Why kwa Kiswahili ni gumu hivyo watoto wengi huwa waongeaji lakini huchelewa kuuliza ze "kwaniniZi"!
Mtoto anaweza kumlilia baba yake anapokwenda kazini halafu ukamwambia tu...baba kaenda kazini na atarudi jioni kesi ikaisha sio!
Huyu wangu bana lazma upate "why dad has to go to work everyday?".....na usipojibu swali litaimbwa mpaka utoe jibu lenye because....Hata sijui kwanini Asali wa Moyo anaenda kazi kila siku....eer in English that is!


Na ukitoa jibu fupi kama "dad has to work so that we can pay bills"....unapewa "why do we have to pay bills" aiiii kazi ya Ualimu nayo ni £24,000+ kwa mwaka.Nikuache kwa sasa!
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 13 August 2014

Mama wa Nyumbani...

Kwa mwaka mmoja na nusu (au tuseme miwili maana nilianza likizo ya Uzazi nikiwa na Mimba ya Miezi 5) nimekuwa Mama wa Nyumbani.


Mie kuwa Mama wa nyumbani ilikuwa choice kutokana na moja ya Misimamo yangu ya kimaisha ambayo wengi hushindwa kunielewa....kwamba miaka 3 ya mwanzo ya wanangu ni lazima niifaidi (as in kuona wanavyobadilika kila siku, kuwafunza manners n.k kabla hawajaanza shule rasmi).


Pia ile hali ya mimi kutoamini mtu mwingine kuangalia wanangu, nahisi kuwa hawatawapa huduma, upendo na attention inavyotakiwa, na wao hawataniambia kwani bado wadogo.


Hiyo ilikuja baada ya kujifungua mtoto wa Pili, yule wa kwanza bado nilikuwa na ile "lazima nirudi kazini, am financially independent working Mum" hivyo Babuu akawa Day care akiwa bado mchanga.


Back to Mama wa kunyumba! Heeeeeeee! Nawaheshimu wote, kazi yenu ni ngumu, Kuzaa is nothing compared to Mama wa Nyumbani na anashatili malipo ya juu ambayo ni zaidi ya £60,000 kwa mwaka....well sio wote bali wale ambao hawana wasaidizi (house girl/boy) na wanafanya kila kitu wao wakati Waume zao wapo Kazini.

Maana mwanamke unafanya kazi ya "domestic assistant" ambayo ni £12,000 kwa mwaka.....unafanya kazi ya Mpishi £20,0000+ kwa mwaka....unafanya kazi Dobi(laundry assistant) £15,000+ kwa mwaka.....unafanya kazi ya Nursery assistant £18,000 kwa mwaka, unafanya kazi ya Nursery Nurse 22,000+ kwa mwaka na mwisho kabisa unafanya kazi ya Muuza Ngono tena High class naa exclusive hihihihihihi nikuwekee mahesabu yake hapa?!!.


Mama wa nyumbani ni kazi ngumu kuliko kwenda Kazini (nje ya nyumbani) kila siku.....huko kazini kwako unafanya kazi ya mtu mmoja tu, Mama wa nyumbani anafanya kazi za zaidi ya watu 4 kila siku na hakuna Likizo!

Haya huyo ni Mimi Mama wa nyumbani mwenye mapenzi na Familia yangu....watoto wangu na Mume wangu, nafanya yote hayo kwa moyo mkunjufu na wenye furaha!

Vipi kuhusu wale wasaidizi ambao unawaita "mahausi gero"? Unawadharau, Unawanyanyasa kwa njia zote possible.....Unasahau au hujui thamani yao kubwa kwa wanachokifanya kwenye maisha yako na ya watoto wako kila siku!


"Am financially independent working Mum" story itakujia soon....nikikumbuka that is...hihihihi


Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 12 August 2014

Maghorofa-2

Siku nimekatiza mahali nkasikia sauti ya Kike kwa Lafudhi ya Kipemba "Bwana Dullah wee panda basi mwenzio nipo hoi".....nkajisemea eh watu na shughuli zao asubuhi-asubuhi.

Wacha mawazo machafu! Bwana Dulla alikuwa Chini ya Ghorofa akitaka Bibie amfuate kwani aogopa panda Lift-ini peke yake!

Sasa Glasgow-Scotigo kama nilivyogusia jana ni Jiji (lililozubaa) lakini linamajengo Marefu mengi kuliko Majiji mengine ndani ya UK.

Pamoja na sifa hiyo wataalam wanadai hayakujengwa vema na mbaya zaidi yana reputation mbaya ya "Komando Yoso" Vijana wakorofi na familia mbazo ni masikini(wanaotegemea Benefit).


Wananchi wakaanza kuzikimbia nyumba za Maghorofani na kukimbia maeneo ambayo kuna majengo hayo Marefu kwa kuhofia "status" zao na kuibiwa au kuuwawa.

Baada ya Muda Serikali(almashauri ya Jiji husika) wakaamua kuyabomoa yale ambayo waliona ni ghali sana kuyatengeneza na Mengine kuyagawa(kuyauza) kwa Mashirika Binafsi ya Nyumba kwa miadi kuwa watayakarabati na kufanya yavutie.


Hakika baadhi yamependeza (mie sikuwepo kabla so sijui)....kwa yale ambayo kulikuwa na Yobs(Komando Yoso) sugu, yalibomolewa na Familia zao zote kuhamishwa miji ya mbali-mbali ili kumaliza Uyoso wao.

Sasa Majengo hayo Marefu yanaanza kurudisha Hadhi yake japokuwa bado wananchi wanasita kwenda kukaa.

Jamii ya wana Architectures...wanasifia sana Mpangilio wa Majengo Marefu uliopo sasa Jijini Glasgow baada ya Baadhi kubomolewa na yaliyobaki kupewa "Cosmetic".

Baadhi ya wananchi waliokulia kwenye Majengo hayo miaka ya 50-70s wanajivunia Historia yake.Nakubaliana nao! Historia yenye vielelezo asilia na vinavyoshikika ni muhimu kwa Vizazi hata Vizazi.....na Giza likianza kuingia Skyline ya Glasgow inapendeza sana....kukicha unakutana na the Boring Glasgow hihihihihi!

Nimejifunza Mengi kuanzia u-nationality wao(wanaotaka kujitenga), Ukabila, Ubaguzi, Uvivu (eeh bana kuna wavivu kule acha)....ila la Majengo ndilo lililonivutia zaidi ndio maana nime-share na wewe.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 11 August 2014

Majengo marefu(Maghorofa)!

Kuna yale yaliyojengwa kati ya Miaka ya 40s na 70s ( I guess) Ilala, na yale pale kati ya Mnazi Mmoja na Stesheni, Posta, Kariakoo, Tandika, Keko, Upanga, Ostabei.


Halafu kuna yale ya Miaka ya 80-90 maeneo ya Tabata, Mbezi Beach.....tulia, nazungumzia Maghorofa ya NHC na ya Kampuni kubwa kama vile TTCL, PPF na kadhalika sio yake binafsi.

Ninayoyataka hapa ni yale ya 40s-70s, ambayo hayakujengwa katika mfumo mzuri wa Maji safi na Maji taka, Nyaya za umeme zimekaa kihatari-hatari na Juu ya Ghorofa ya Mwisho kuna uwazi kwa ajili ya eer "kupunga hewa" " kufurahia the view"?!!! in which kwa nchi yenye watu wenye ma-stress na ma-depression kama UK ingekuwa rahisi kujipoteza (kujirusha ili kufa).....mbona tungewa-sue NHC mpaka wangekoma.


Pamoja na hasi hizo bado majengo yale yana sifa ya kujengwa kwa kutumia Malighafi Imara ukilinganisha na Maghorofa yanayojengwa Karne hii.


Magorofa hayo yakikarabatiwa mmmh itakuwa gharama kuu na pengine kulipuliwa na yaanza kuanguka labda yapewe "cosmetic" tu....kubadili mfumo wa Maji safi na taka(choo incl) na umeme(yale manyaya bana khaaaa)!!

Majengo hayo ndio yanalifanya Jiji la Dar es Salam kupendeza na nadhani kuwa Jiji la kwanza lenye Majengo Marefu is it East Africa au Tz tu?(Hata sijui)!!....hupendeza sana mida ya Usiku (kama kuna Umeme).


Watu wanaokaa kwenye Maghorofa (Makabati hihihiihihi) hayo huwa na "status" tofauti na wale wanaokaa nyumba za Chini.....wanajidaaaaaai

Pale chini kuna Mitaro isiyorasmi inamwaga mimaji michafu na hapo pembeni kuna Mfumo wa Maji safi(what a mixture)....Karo zinafurika Vinyesi alafu watu hawana habari wala nini....full maringo! Nimekulia Maghorofani enzi zileeeeee hivyo najua ninachokizungumzia.

Kinachonisikitisha ni Maghorofa hayo kutelekezwa na ama watu Binafsi waliyoyanunua au Wamiliki kama vile NHC(kwa kisingizio wapangaji hawalipi Kodi kwa wakati).

Na pengine itafikia mahali watayabomoa na hivyo kupoteza Historia.

Kwanini nakuambia haya? Ni kutokana na uzoefu nilioupata Jijini Scotland. Kumbuka Scotigo ni wenye Majengo marefu Mengi kuliko Nchi nyingine ndani ya UK. Nitakuelezea sehemu ya pili. Very Interesting, usikose!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 7 August 2014

Reality Tv Shows....

Haiyaaaaa (Waswahili wa huku ndio wanasalimiana hivyo)....Wakishua wanasema how do yo do.....asa nani anamuda wa "hau-du-yu-du Maisha haya?!!Unakumbuka enzi Reality shoo zinaanza kulikuwa na slogan ya "Movies are boring, Reality is exciting"....well not exactly ila ili-sound hivyo bana eh!
Basi bana si Ndio akina Kadarshian* wakaanza na mimi nikiwa mmoja wa watazamaji wa mwanzo kabisa nikiamini kuwa nilichokuwa nakiona ni uhalisia wa Maisha yao....kwa miaka miwili.....mai miaka Miwili naangalia scripted "reality" Tv shoo (nalia hapa kwa aibu).
Basi bwana, nikaacha kuangalia na kuchukia Reality Tv shoo zote ikiwemo Big Brother!
Sasa nilipomimbika 2012 nilianza Likizo ya Uzazi nikiwa na Mimba ya Miezi 5.....unataka kujua kwanini? Hehehehehe aiii nilikuwa "rough" sana na kazi yangu inahitaji u-smart bana, nkaona mmh ntakosa Maternity Leave hapa, mwanamke wacha nikimbie mapemaa(natania).
2012 ndio nikaanza tena kuangalia "Real House Wives" tena marathon ili nitosheke, hee nkawa addicted (blame it on Mimba, akyanani vile halikuwa kosa langu)....nikaanza kuhisi nazidi kuwa Mjinga lakini nikashindwa kuacha mapaka nilipojifungua 2013 phewww!!Baada ya hapo nikaja gundua Mary Mary nao wana Reality Tv show, knowing wale ni Wajukuu wa Yesu nkajisemea hawawezi kukubali show yao iwe scripted(hawatokubali kucheza uongo ili kunogesha show) aiii Kitukuu cha Yesu nikaanza kuangalia.


Uzuri wa Mary-Mary ilikuwa kuimba-imba hapo wimbo wa "Go get it" ndio unazidi kunibamba....mwanamke nacheza nakuliachia tumbo langu la uzazi linarukaruka.

Mara booom! One of Mary-Mary hubby ka-cheat....sijui nini na nini...imagine hau lavi davi in jizasi nemu thei wea kwenye lishoo lao alafu sasa....mxsiii SCRIPTED!

Oh! Kijana wangu wa Miaka 3 anaimba ile wimbo ya Ali Kiba Ft Bonge la nyau "ukanifanya nilale njaa ili wewe usije kosa" mpaka nafurahi, Kiswahili kitamu.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 6 August 2014

Kupenda kusifiwa....

Ah! Kama wewe ni mzuri wa jambo fulani hakika utakuwa unajijua hivyo sio mbaya kujisifia mwenyewe.....au subiri Mpaka urudishe namba (ufariki) ndio watu wakusifie kwa Mema na hata kwa yale mabaya yako.

Mmh! Lamini ukifariki unakuwa umemaliza ya Duniani, sasa sifa za Walimwengu uliowaacha zitakusaidia nini? Kungekuwa na uhakika wa Sifa hizo kukupunguzia Madhambi uliyofanya au Ukali wa Moto siku ya Kihama, ingekuwa Poa!


Sasa, kuna Watu wameumbwa kuzitafuta Sifa kwa nguvu.....yaani mtu anatengwa, anafanyiwa maovu na mabaya yote lakini yeye yumo tu kujionyesha Mwema kwa hao Walimwengu.....wacha kujipendekeza, fanya yako....hutakiwi na huna umuhimu kwao!


Unawajua wale Jamaa wanafanyiwa mabaya, wanaharibiwa familia zao au Mradi ambao ulikuwa Tegemeo kiuchumi....Jamaa waharibifu wakirudi na kuomba Msamaha wanasamehewa na Ujamaa unarudi upya.

Mie siwezi bana, ukinitenda ama nalipiza Kisasi kwa Jamii yako Nzima au nakufuta akilini (nachukulia kuwa hau-exist) nasonga mbele.....hizi sio NYAKATI za Yesu na siamini katika "Mungu atanilipia" Bwanshee (sijui hata maana yake).


Naishi maisha mbayo hayana stress zinazosababishwa na Marafiki (ambao sina) au Jamaa (ndugu wa kuunganisha) kwasababu nimejiwekea utaratibu wa "kuengua" watu as I go....nitajaribu "kujipendekeza" mara 2....usipo-respond namie nakuwa nimemaliza!


Ukirudi baadae nitakusikiliza.....oh siku hizi nina watoto hivyo sina muda wa kusikiliza.

Nimepoteza track!.....nachojaribu kusema hapa ni kwamba usifanye mambo ukitegemea kusifiwa au kuzungumziwa vizuri kwa Watu.Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 4 August 2014

Kuwekana...

Heloooooooo there!


Mie huwa sishangai mtu akimchomekeza Jamaa yake (binamu, mtoto wa ba' mdogo).....nilishakuambia Ndugu ni wale mnaochangia Damu kwa Baba na Mama vinginevyo nyie ni jamaa tu!

Hii haina "Dinah kakaa sana Ulaya kabadilika"....tangu Mdogo mie huwa siwachukulii Jamaa kuwa Ndugu! Ndugu zangu ni wale tuliotoka Tumbo Moja au Baba na Mama Mmoja.....kama hutaki kukubali bana shauri yako!

Mambo ya kulazimisha Undugu bana ni kumaskishana (kutiana umasikini) na kuongezeana ma-stress tu.....hii ndio huwakosesha watu "bahati" ya kufanikiwa.


Bana mie ningekuwa sijui nani ni nani Serikalini halafu kuna nafasi za kazi zinapatikana unadhani nitakuajiri wewe wakati nina Mpwa wangu (Jamaa) anaelimu na ujuzi ka' wako nyumbani? Aiii nitampa nafasi yeye kwanza, akiikataa ndio wewe wa Nje utafikiriwa.


Najua sheria za kazi na kadhalika BUT Mpwa wangu sio Ndugu yangu, hatu-shei damu wala Ubini sasa undugu unatoka wapi hapo?!!!
Kuwa mkweli! Hata wewe ungefanya hivyo....kila mtu anafanya hivyo.....kama hufanyi hivyo basi wewe unaroho mbaya sana.


Nakuona hapo unataka kusema "ndio maana wenzetu Wazungu wanaendelea kwasababu hawawekani"......umeishi nao? Umewahi kufanya nao kazi Nchini mwao?


Wazungu wanawekana like nothing else, tofauti ni kama nilivyosema Binamu sio Ndugu yake.....Mtoto wa Dada yako sio Ndugu yake so hata akiwaweka kwenye "Office" hakuna anaejua "connection" ya Ujamaa.
Kumuweka Mdogo wako, Mkeo au Mwanao sasa hilo ndio Kosa!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 31 July 2014

Umewahi ombwa Mchango wa Birthday?

Huu ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa heshima wa Vipato vya watu....hii kwa Michango yote isipokuwa Ada ya Shule.

Kama humudu kulisha watu kwenye sherehe ya kuadhimisha siku yako ya kuzaliwa si uachane na issue nzima ya Sherehe!!

Kujitegemea Kiuchumi kumegawanyika katika makundi mbali mbali ujue...(sina uhakika, najaribu kulazimisha tu hapa hihihihihi).....!

Kuna baadhi ya watu ambao huishi kutegemea wenzao ili kufanikisha mambo au jambo kwa faida zao Binafsi......wandugu jitegemeeni kiuchumi EBO!!!

Mchango wa Harusi: Wakati harusi(Bikira) yenyewe wewe na mtarajiwa wako hamna hiyo HARUSI. Kama hamuwezi kulisha wageni wenu kwa kutumia vipato venu basi fungeni Ndoa mkiwa peke yenu wawili na mashahidi....eti? Siiiiiiimple + no stress.
Birthday Party: hii sinimeisha isema kule juu? Eeeh kuna hii hapa chini:


Michango ya Baby Shower: Kwa kawaida ukialikwa unaenda na Zawadi inayomhusu Mtoto mtarajiwa si ndio? Sasa hii biashara ya kulazimishana kuchanga senti au kununua Zawadi nani kairuhusu kwanza na je inalipiwa KODI (mmh usikute ile walioniandalia walichangisha wageni so yeah hihihihihi)....?!


Michango ya Misiba: Siku hizi Mtu kufa imekuwa Social event na kwa baadhi ni Mashindao ya "Misiba wa akina nani umefana"......waombolezaji wanatumbuizwa na Wanakwaya (live Band).

Aiiii I prefer Misiba ya Kiislam no fuss....jiombee kabla hujaombewa Shimoni you go!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 29 July 2014

Religious vs Believe in God

Nilikuambia nipo Michezoni Glasgow-Scotigo, basi bwana si nkakutana na jamaa wakaniuliza kama mimi ni Religious, nkasema hapana ila naamini Mungu.....acha washtuke!!!


Udini unatutenga, Udini unasababisha watu wasifanye mambo kwa uhuru, Udini hukosesha watu wake/waume wema n.k.


Hivi unajua kuwa Dini zililetwa na Wageni ambao sasa ama hawazifuati au wameamua kubadilisha waliotuaminisha kuwa "yaliandikwa" na nani sijui nani.


Halafu Waafrika tunaanza kuwaona namna gani vipi hawa jamaa wanatubadilishia Maneno ya kwenye Vitabu vyetu vitakatifu ili kuendana na "maisha" ya sasa! Ama kweli Dunia imefikia mwisho.


Tunajipa Moyo na kushikilia Imani zetu tukiamini kuwa ni za kweli na kuponda hao Wageni (Wamagharibi na Waarabu waliotuletea hizo Dini) kuwa ni Wafuasi wa Shetwani.

Baada ya wao kuchoshwa na Imani mbili tangu Miaka 2000 iliyopita wengi wao wakaamua ama kuachana nazo au kuanzisha nyingine ili ku-suit maisha yao ya Nyakati hizi.


Sasa wewe unapoteza Muda wako wote kujaribu kuwalisha wenzako Maneno yasio na ukweli (nani mwenye Uhakika kama yaliyomo kwenye Vitabu Vitakatifu yalisemwa na Allah/Mungu au Yesu?....thibitisha basi kama ulishuhudia....hihihihi).

Mie sifuati maneno ya kwenye Vitabu vitakatifu, lakini namuamini Mungu....naamini kuwa yupo mahali na hunisikiliza bila kuuliza Maswali katikati ya maelezo yangu pale ninapomshukuru, hutekeleza kwa wakati wake pale ninapomuomba....(mmh ila siku naumwa Uchungu wa kuzaa bana my 1st born Mungu alinichunia, nilimuomba nisisikie Maumivu hata kiduchu).....liache hili!


Wageni (Wamagharibi na Waarabu) wakija na Dini zao mpya, Jinsia Mpya sijui Haki mpya mie walaaa sina habari kwasababu najua Mungu wangu ni Mmoja na ananisikiliza.


Nilikuambia napenda kusikiliza Mawaidha....sasa kuna Mazuri na ya kufunza/ongoza, Mabaya, yakerayo na kupotosha jamii.

Kuwa makini na ma-information uyapatayo via Mitandao, Simu na ndugu zake....kumbuka kuchuja.....chukua yenye maana kwako mengine yaache yapite.

Imani ni choice ya life style (in my head) tusilazimishane bana eeh!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 28 July 2014

Review Undugu wako...

Familia/koo nyingi huwa kuna mtu ambae karibu wote wanaMshuku....wanamuona hatari....kutokana na mambo yake Kiuchumi kuwa safi na kila anachosema basi ni "sheria" au hupewa "umuhimu" au "umakini" hata kama alichosema ni upuuzi!


Yaani watu kwenye Familia\Ukoo husika hawaishi kwenda kwa huyo mtu, watoto wake, Mke/Mume wake wote wanapewa attention tofauti na akina nyie Hohehahe.


Mtu huyu na Familia yake hufurahia yote hayo na huwa on the look out kuona nani anakuja speed ili kuwa kama yeye au kumpita Kiuchumi....basi akigundua atafanya kila alijualo kuzuia Ndugu (tumbo moja) au Jamaa(ndugu wa mbali wale wa kuunganisha mjomba, binamu etc) asifanikiwe.


Umewahi kumpa Ndugu yako wa hivyo idea ya Biashara au Mradi halafu akakukatisha tamaa kisha yeye anaifanya hiyo Biashara au ule mradi ambao alikuambia kuwa huwezi kufanikiwa ukiufanya, kwamba utapoteza pesa tu??.....hihihiihi sasa amka na review Undugu wenu!


Mtu huyu huwa hasaidii wenzake ambao ni masikini kuweza kujikomboa, siku zote atakupa senti ili uendelee kumuona Muhimu maishani mwako na hivyo kurudi kwake kuomba tena na tena.


Yaani anafurahia kukusaidia kidogo mara kwa mara....badala ya kukusaidia mara moja lakini msaada huo uwe ni wa muda mrefu.


Mf: kukupa Mtaji ili ukajiajiri kuliko kukulipia Ada ya shule na senti za Matumizi ya watoto, zikiisha urudie tena...hiyo ni furaha yake kwani unatendelea kumuona au kumchukulia kama Mkombozi wako hehehehehe!


Wahenga walisema "ukitaka msaidia mtu, usimpe Samaki....mpe Nyavu na umfunze kuvua ili awe anavua mwenyewe"!

Actually sio Wahenga waliosema(sijui aliesema), nilisoma huo Msemo Twita enzi zile....


Babai.
Mapendo tele kwako...

Friday, 25 July 2014

Glasgow 2014....

Siku ya Pili ya Mashindano ya Jumuiya ya Madola, nipo eneo la Tukio kwa Wiki 2....interested?....me neither!Kama umewahi kufanya kazi au kutembelea Jiji la London au NY au hata Dar(City Centres sio Keko sijui Masaki huko, nazungumzia "kiini")....ukija Glasgow bana.....ka' sio Jiji, yaani hakujachamgamka kiviiiiiile(ka' Jiji).....
Ila kuna kama "fun fair" kwa kids(sijui wanaitaje bana), nadhani hiki ndicho kitakachonileta huku mara kwa mara.
Michezo imeingiliwa na watu kutoka "Makabatini" bwana, wamefanya watu tushindwe ku-concentrate na Mashindano.....yaani "ukorosho" wao una distract kimtindo....maana wengine tulikuwa tunapenda Mbio na Kuogelea....kuangalia "zile maumbile" za Wakaka pale kati na Miguu (au ni mimi tu nakua pervert wa Kike....hihihihi).

Siku hizi bana mtu unajisikia vibaya hata kuangalia mchezaji, akili kama inahamia kwenye akifanyacho private! Kwani lazima watuambie wao wanalalwa na wanaume/wanawake wenzao?....Mbona sie "tulionyooka" hatuhangaiki kutaarifu Dunia? SOOOOOOO annoying.

Wakianza tu kutoka kwenye Mpira wa Miguu (which nadhani hawatatoka for biz reasons japo kuwa wapo) akyanani vile siangalii tena Kabumbu(si mshabiki, I just penda Mchezo).

Mtuache tubaki tukijiuliza hivi yule ni Mkorosho?....mmh lazima atakuwa Mkorosho, ujue kutokujua jambo na kukufanya ujiulize(kama unao muda huo) kunaongeza mwendo wa siku yako....mara boom saa moja Usiku, watoto wanatakiwa kwenda kulala na siku imeisha!
Speculation is fun.....hujui nini kinaendelea unabaki kuspekyuleti mwishowe unajiona Jinga unaachana na issue nzima.Nikutakie Mwanzo Mzuri wa Mwisho wa Wiki.Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 24 July 2014

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case.


Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo!

Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie!


Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*.


Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi Mazoezi, Haipati Hewa wala Mwanga wa Jua + unapenda sana kukaa chini*.


Sasa mwanamke(na mwanaume) fanya yote ambayo ni kinyume ya nilichosema hapo juu. Najua unajiuliza utapataje Jua makalioni eti?!!


Sio lazima ukayaanike makalio yako Juani kila mtu ayaone bali vaa Khanga bila Chupi(mwanamke) na Msuli/Pensi nyepesi bila kitu ndani (mwanaume) kisha simama Juani kwa muda kiasi.


Rangi tofauti Kwapani: Inasemekana Weusi huo hutokana na "kinga" ya Ngozi ya sehemu hiyo ku-over work ili kuzuia. Madhara ya Mionzi ya Jua....ndio maana hata ukiichubua inaendelea kuwa Nyeusi mpaka "kinga" ya Ngozi yote iishe ndio Kwapa litatakata.....so unfair and expensive kwa wapaka Mkorogo khaa!

Kwa baadhi yetu hata tukipaka "Sun cream" ili "kinga" "isiOve weki" bado Kwapa linabaki jeusi kuliko sehemu nyingine ya Mwili....so annoying!


Sasa ukitaka kuikomesha "kinga" inakupasa uiachie Kwapa yako nje ili ipate mwanga wa jua wa mara kwa mara ili "kinga" isi-react kwa hasira dhidi ya Mionzi ya jua mahali hapo!


Wengine Kwapa lawa juesi kwasababu ya kutokumalizika kwa Nywele baada ya kunyoa, Maambukizi ya ngozi na wengine ni kuinyoa sehemu hiyo kwa hasira....ni kwapa tu jamani, kwanini utumie nguvu na hasira kulisugua au kulinyoa?


Nguvu zako ndio zinasababisha "majeraha" usiyoyaona na hivyo kushambuliwa na Bacteria na kuweka "rangi" tofauti hapo kwapani.

Stori time: Jana Usiku nimeamua kunyoa Kwapa (you are welcome hihihihihi I mean sorry for TMI)....bila kutumia Cream....yaani nimeenda "chukuchuku" na Wembe baada ya Miaka zaidi ya 15.

Heee!Mwanamke najiangalia kwapa jeupee na laini halina hata baki la nywele.....Hair removal cream day time bai bai....umeni-cheat for nearly 15yrs....bai bai sikutaki tena!

Sasa ni hivi! Ngozi ni Mkao makuu ya Bacteria (Wanasayansi hawajui kwanini)....sasa unaponyoa Asubuhi ni wazi kuwa umewapa Bacteria Makao masafi ya kushambulia....ndio maana unapata mapele kwapani sometimes!


Hivyo ni vema kufanya "tretment" yeyote ya ngozi kama vile scrub, kutumbua/kamua chunusi, nini na nini...(kunyoa nayo ni treatment na Kwapa ni Ngozi bana wacha ubishi eeh)...mida ya Usiku ili kuipa ngozi nafasi ya kujijenga upya bila muingiliano wa wadudu wa huko Nje.

Kidokezo: Usichukue maelezo haya ukayatumia ukijifanya Mtaalam au umefanya Utafiti, maana Wambongo nanyie nao mmeendelea kweli.....mnaweka na Picha kabisa ili ionekane kuwa wewe ndio Umeandika wakati maelezo ni yangu kwa Uzoefu wangu Binafsi, Ulaaniwe wewe na jamii yako....HUH!!...(Calm down Dinah...Calm down).

Hii imefidia siku 2 ambazo siku-Blog! Ile "kupenda kukaa chini" haina ukweli ndio maana nimeweka *.

Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 21 July 2014

Chuki....

Ni sehemu ya Ubinaadamu si eti! Kama unaweza kupenda basi ujue unaweza kuchukia pia....zote ni hisia!


Mie bana ukiniudhi kwa kiwango cha kutosha na ukijaribu kuingilia Maisha yangu binafsi nakuchukia wewe, Familia yako, Ukoo wako, Jamii yako, Kabila lako na Nchi yako kwa Ujumla.

Yaani watu wanaotoka huko unakotoka wewe wote wanakuwa Maadui, yaani siwaPENDIIIIII mf ni Wanajeria.....Mungu anisamehe ila daa! Nawachukia balaa.....wengine ni wale Majirani zetu waliozima ka' umeme wa Tanesco (what does it mean) ambao hatutaniani na Kiswahili kwao ni sawa na kuwa Malaya the Nigerian of East Africa....BOY I HATE THEM.

Alafu kuna Wazimb hihihihihihi nikupe stori? Ni washenzi.....hapa hapatoshi kwa stori, maana ninazo nyingi.

Huyo mimi, halafu kuna wewe (sio wewe bali yule)....ambae unamchukia tu mtu wakati wala humjui, hujawahi kukutana nae na wala hajawahi kujihusisha na lolote linalokuhusu!

Unaanza Vita!.....aah! Kuna jamaa namkumbuka alikuwa namuandama mwenzie kwa chuki ya wazi kabisa halafu wala hawajuani.....yaani ikawa kama ndio Ajira yake kurushia Makombora ya Kashfa, Matusi, Mafumbo na mengineno.....sasa wenye Chiki ya namna hii hijikinga kwenye "kukosoa".....eh! Kuna tofauti ya kumkosoa mtu na kumchukia.... Chuki ya namna hii haina tofauti na MCHAWI!


Usinijaji, Mimi sio Mchwi bana eeh!....nina sababu KUU zinagusa maisha yangu binafsi tena kwa karibu, mmoja alitaka kunitoa Roho!.....Sasa hao niliowataja hapo juu nina Uzoefu MBAYA nao (usiniige) na ndio maana nawachukia wao na Nchi zao.

Sina kawaida ya kumchukia tu mtu bila sababu mpaka uguse maisha yangu, maisha ya Familia yangu au uniguse mimi mwenyewe.

Oh! Nawachukia Wayahudi pia.....Stori time:


Mwaka 2005 kwenye Uchaguzi Mkuu(UK) maeneo ya NW-London (wapo kibawo).....nimemaliza kupiga Kura, mmoja akaniambia "we don't want you here, go back to where you came from"....

Nikamjibu kwa kiingilishi changu cha KissWay "at least I have where I came from, you've got non....you were put in Jerusalem by Americans which is belong to Palestine"(hata sijui kama ni kweli)....akaishia kusema "am so sorry maam".....so yeah nawachukia hao na Vizazi vyao pia.

Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 17 July 2014

Nipo mtaani kwako, upo home?...

Sipendi hii tabia kwa Moyo Mkunjufu kabisa!!!


Nilikuwa namkimbia rafiki yangu Mghana kwa tabia hii....niambie basi siku moja kabla hujaja kuwa unapanga kuja kwangu....sio unafika Mtaani kwangu au pengine Mlangoni halafu ndio unaniambia kwa Simu!
Sio peke yake, hata ndugu (wa mbali) na jamaa wanatabia hiyo....kuna siku (nikiwa bado Nyumbani) nilimrudisha mtu kwao on next flight....the next Bus bana, hela ya next flight mie ninayo?!!....nikaambiwa nina Roho Mbaya.

Katoka huko Mwanza sijui wapi eti kaja kutafuta Kazi, asa kwanini usituambie mapema tujiandae na Bajeti!....anyway achana na hilo.
Mie huwa sifanyi jambo ambalo najua sipendi kufanyiwa, tatizo linakuja pale Mwenza wako sasa anatabia hiyo....hehehehe Baba Babuu Asali wa Moyo wangu bana anaudhi kweli!!!

Mnaweza mkawa safarini mara akakumbuka fulani anakaa karibu na hapo mnapopumzika labda....ananyanyua simu "eh bwana fulani! Upo nyumbani?....tupo hapa karibu kama vipi tuje kuwasalimia"....aiii! Naudhikaga*(huwa naudhika) sana sababu najua adha yake na siipendi.

Hata nikimwambia ni tabia mbaya wala hana habari, wenyewe wamemzoea. Ila wakitaka kuja kwangu bi Shalilah(hata sijui maana yake), sharti wanambie mapema.....Mwanamke nyumba na Sheria zake nazitunga/weka mie!

Ujue kuna siku mtu hujisikii kukutana na mijitu, alafu boom "nipo hapa, upo home?"


Tabia hizo za kuibuka kwa watu kwa kutoa notisi ya muda mfupi zikanifanya ni-redirect simu zote za ndani to a mobile so hata nikiwa home nasema tu sipo, "mbona umepokea simu ya ndani" nasema nime-redirect simu zote kwenye Simu ya mkononi.Ustaarabu waja kwa namna nyingi, kutoa taarifa mapema nao ni ustaarabu(unless ni immediate relative then njoo wakati wowote).


Babai.
Mapendo tele kwako...