Skip to main content

Reality Tv Shows....

Haiyaaaaa (Waswahili wa huku ndio wanasalimiana hivyo)....Wakishua wanasema how do yo do.....asa nani anamuda wa "hau-du-yu-du Maisha haya?!!



Unakumbuka enzi Reality shoo zinaanza kulikuwa na slogan ya "Movies are boring, Reality is exciting"....well not exactly ila ili-sound hivyo bana eh!




Basi bana si Ndio akina Kadarshian* wakaanza na mimi nikiwa mmoja wa watazamaji wa mwanzo kabisa nikiamini kuwa nilichokuwa nakiona ni uhalisia wa Maisha yao....kwa miaka miwili.....mai miaka Miwili naangalia scripted "reality" Tv shoo (nalia hapa kwa aibu).




Basi bwana, nikaacha kuangalia na kuchukia Reality Tv shoo zote ikiwemo Big Brother!




Sasa nilipomimbika 2012 nilianza Likizo ya Uzazi nikiwa na Mimba ya Miezi 5.....unataka kujua kwanini? Hehehehehe aiii nilikuwa "rough" sana na kazi yangu inahitaji u-smart bana, nkaona mmh ntakosa Maternity Leave hapa, mwanamke wacha nikimbie mapemaa(natania).




2012 ndio nikaanza tena kuangalia "Real House Wives" tena marathon ili nitosheke, hee nkawa addicted (blame it on Mimba, akyanani vile halikuwa kosa langu)....nikaanza kuhisi nazidi kuwa Mjinga lakini nikashindwa kuacha mapaka nilipojifungua 2013 phewww!!



Baada ya hapo nikaja gundua Mary Mary nao wana Reality Tv show, knowing wale ni Wajukuu wa Yesu nkajisemea hawawezi kukubali show yao iwe scripted(hawatokubali kucheza uongo ili kunogesha show) aiii Kitukuu cha Yesu nikaanza kuangalia.






Uzuri wa Mary-Mary ilikuwa kuimba-imba hapo wimbo wa "Go get it" ndio unazidi kunibamba....mwanamke nacheza nakuliachia tumbo langu la uzazi linarukaruka.





Mara booom! One of Mary-Mary hubby ka-cheat....sijui nini na nini...imagine hau lavi davi in jizasi nemu thei wea kwenye lishoo lao alafu sasa....mxsiii SCRIPTED!





Oh! Kijana wangu wa Miaka 3 anaimba ile wimbo ya Ali Kiba Ft Bonge la nyau "ukanifanya nilale njaa ili wewe usije kosa" mpaka nafurahi, Kiswahili kitamu.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao