Skip to main content

Posts

Showing posts from September 17, 2023

Endelea mtongoza Wife...

Ni kawaida kwako Mume (na jamii kwa ujumla) kutegemea mkeo afanye kila awezalo kuifanya ndoa kusimama utasema kajioa mwenyewe. Kuna siku nikaamua kugugo matatizo ya Ndoani, kila maelezo niliyoyapata kwa Kiswahili na Kiingereza, mzigo wa kuweka mambo sawa wenye Muungano huo alibebeshwa mke.   Hakukua na maelezo ya kutosha ambayo yanamsaidia Mume kutatatua matatizo ya ndoa zaidi ya nini afanye akishindwa kusimamisha, Mke na Mama nani nimpende? au nini cha kufanya ikiwa anamaliza haraka? Vipi kuhusu nini cha kufanya ikiwa umemuudhi mkeo? Nini mbadala wa kumnunia/fokea/ignore mke wangu, kitu gani nifanye kukabiliana na mzunguuko wa hedhi wa mke wangu baada ya kupevusha pale anapokaribia Siku zake(sio za kufa bali Hedhi) n.k.? Kuna mengi kwenye ndoa zaidi ya Ego, Mama yako na Uume wako.     Kwenye blog hii tutakumbushana mengi tu ambayo hayahitaji uekisipati wa jinsia bali ni uelewa wa kawaida tu wa kusomana kwa pande zote mbili. Nakumbuka enzi nilipokuwa Twitter kuna wakaka wawili nawahesh