Kwa mwaka mmoja na nusu (au tuseme miwili maana nilianza likizo ya Uzazi nikiwa na Mimba ya Miezi 5) nimekuwa Mama wa Nyumbani. Mie kuwa Mama wa nyumbani ilikuwa choice kutokana na moja ya Misimamo yangu ya kimaisha ambayo wengi hushindwa kunielewa....kwamba miaka 3 ya mwanzo ya wanangu ni lazima niifaidi (as in kuona wanavyobadilika kila siku, kuwafunza manners n.k kabla hawajaanza shule rasmi). Pia ile hali ya mimi kutoamini mtu mwingine kuangalia wanangu, nahisi kuwa hawatawapa huduma, upendo na attention inavyotakiwa, na wao hawataniambia kwani bado wadogo. Hiyo ilikuja baada ya kujifungua mtoto wa Pili, yule wa kwanza bado nilikuwa na ile "lazima nirudi kazini, am financially independent working Mum" hivyo Babuu akawa Day care akiwa bado mchanga. Back to Mama wa kunyumba! Heeeeeeee! Nawaheshimu wote, kazi yenu ni ngumu, Kuzaa is nothing compared to Mama wa Nyumbani na anashatili malipo ya juu ambayo ni zaidi ya Ā£60,000 kwa mwaka....well sio wote bali wale ambao haw...