Halafu kuna yale ya Miaka ya 80-90 maeneo ya Tabata, Mbezi Beach.....tulia, nazungumzia Maghorofa ya NHC na ya Kampuni kubwa kama vile TTCL, PPF na kadhalika sio yake binafsi.
Ninayoyataka hapa ni yale ya 40s-70s, ambayo hayakujengwa katika mfumo mzuri wa Maji safi na Maji taka, Nyaya za umeme zimekaa kihatari-hatari na Juu ya Ghorofa ya Mwisho kuna uwazi kwa ajili ya eer "kupunga hewa" " kufurahia the view"?!!! in which kwa nchi yenye watu wenye ma-stress na ma-depression kama UK ingekuwa rahisi kujipoteza (kujirusha ili kufa).....mbona tungewa-sue NHC mpaka wangekoma.
Pamoja na hasi hizo bado majengo yale yana sifa ya kujengwa kwa kutumia Malighafi Imara ukilinganisha na Maghorofa yanayojengwa Karne hii.
Magorofa hayo yakikarabatiwa mmmh itakuwa gharama kuu na pengine kulipuliwa na yaanza kuanguka labda yapewe "cosmetic" tu....kubadili mfumo wa Maji safi na taka(choo incl) na umeme(yale manyaya bana khaaaa)!!
Majengo hayo ndio yanalifanya Jiji la Dar es Salam kupendeza na nadhani kuwa Jiji la kwanza lenye Majengo Marefu is it East Africa au Tz tu?(Hata sijui)!!....hupendeza sana mida ya Usiku (kama kuna Umeme).
Watu wanaokaa kwenye Maghorofa (Makabati hihihiihihi) hayo huwa na "status" tofauti na wale wanaokaa nyumba za Chini.....wanajidaaaaaai
Pale chini kuna Mitaro isiyorasmi inamwaga mimaji michafu na hapo pembeni kuna Mfumo wa Maji safi(what a mixture)....Karo zinafurika Vinyesi alafu watu hawana habari wala nini....full maringo! Nimekulia Maghorofani enzi zileeeeee hivyo najua ninachokizungumzia.
Kinachonisikitisha ni Maghorofa hayo kutelekezwa na ama watu Binafsi waliyoyanunua au Wamiliki kama vile NHC(kwa kisingizio wapangaji hawalipi Kodi kwa wakati).
Na pengine itafikia mahali watayabomoa na hivyo kupoteza Historia.
Kwanini nakuambia haya? Ni kutokana na uzoefu nilioupata Jijini Scotland. Kumbuka Scotigo ni wenye Majengo marefu Mengi kuliko Nchi nyingine ndani ya UK. Nitakuelezea sehemu ya pili. Very Interesting, usikose!
Babai.
Mapendo tele kwako...
Comments
Deeply niko kama wewe ila nimevurugwa tu maishani so sometimes vipaji, karama na endowment nilizo nazo zinashindwa kuwa manifested na kunifanya most of the time kuwa mtu niliyejaa huzuni.
Nikipata nguvu siku nyingine nita share nawe a brief or unbrief version of my life, utajua namna ya kuitumia either kwa kuitohoa kidogo ili kunipa veil ya identity au kuitoa tu kama ilivyo iwe mafunzo wa watu wengine.
Nimependa tu kukuambia kuwa ni mfuasi wako kwenye blog zote mbili na naipenda hii maana iko 'valuvalu' na haitabiriki kuwa leo topic itakuwaje though na ile ya kule ndio ilikuwa zinduzi ya mie kukufahamu na kujua umebarikiwa mno kiuandishi na udadavuzi na unajua namna ya ku communicate na hadhira yako.
Be blessed na salimia BI (Barack na Iman)
MwanaMalundi
Salamu zimefika, ahsante kwa kujali. Ubaki salama.