Skip to main content

Posts

Showing posts from August 3, 2014

Reality Tv Shows....

Haiyaaaaa (Waswahili wa huku ndio wanasalimiana hivyo)....Wakishua wanasema how do yo do.....asa nani anamuda wa "hau-du-yu-du Maisha haya?!! Unakumbuka enzi Reality shoo zinaanza kulikuwa na slogan ya "Movies are boring, Reality is exciting"....well not exactly ila ili-sound hivyo bana eh! Basi bana si Ndio akina Kadarshian* wakaanza na mimi nikiwa mmoja wa watazamaji wa mwanzo kabisa nikiamini kuwa nilichokuwa nakiona ni uhalisia wa Maisha yao....kwa miaka miwili.....mai miaka Miwili naangalia scripted "reality" Tv shoo (nalia hapa kwa aibu). Basi bwana, nikaacha kuangalia na kuchukia Reality Tv shoo zote ikiwemo Big Brother! Sasa nilipomimbika 2012 nilianza Likizo ya Uzazi nikiwa na Mimba ya Miezi 5.....unataka kujua kwanini? Hehehehehe aiii nilikuwa "rough" sana na kazi yangu inahitaji u-smart bana, nkaona mmh ntakosa Maternity Leave hapa, mwanamke wacha nikimbie mapemaa(natania). 2012 ndio nikaanza tena

Kupenda kusifiwa....

Ah! Kama wewe ni mzuri wa jambo fulani hakika utakuwa unajijua hivyo sio mbaya kujisifia mwenyewe.....au subiri Mpaka urudishe namba (ufariki) ndio watu wakusifie kwa Mema na hata kwa yale mabaya yako. Mmh! Lamini ukifariki unakuwa umemaliza ya Duniani, sasa sifa za Walimwengu uliowaacha zitakusaidia nini? Kungekuwa na uhakika wa Sifa hizo kukupunguzia Madhambi uliyofanya au Ukali wa Moto siku ya Kihama, ingekuwa Poa! Sasa, kuna Watu wameumbwa kuzitafuta Sifa kwa nguvu.....yaani mtu anatengwa, anafanyiwa maovu na mabaya yote lakini yeye yumo tu kujionyesha Mwema kwa hao Walimwengu.....wacha kujipendekeza, fanya yako....hutakiwi na huna umuhimu kwao! Unawajua wale Jamaa wanafanyiwa mabaya, wanaharibiwa familia zao au Mradi ambao ulikuwa Tegemeo kiuchumi....Jamaa waharibifu wakirudi na kuomba Msamaha wanasamehewa na Ujamaa unarudi upya. Mie siwezi bana, ukinitenda ama nalipiza Kisasi kwa Jamii yako Nzima au nakufuta akilini (nachukulia kuwa

Kuwekana...

Heloooooooo there! Mie huwa sishangai mtu akimchomekeza Jamaa yake (binamu, mtoto wa ba' mdogo).....nilishakuambia Ndugu ni wale mnaochangia Damu kwa Baba na Mama vinginevyo nyie ni jamaa tu! Hii haina "Dinah kakaa sana Ulaya kabadilika"....tangu Mdogo mie huwa siwachukulii Jamaa kuwa Ndugu! Ndugu zangu ni wale tuliotoka Tumbo Moja au Baba na Mama Mmoja.....kama hutaki kukubali bana shauri yako! Mambo ya kulazimisha Undugu bana ni kumaskishana (kutiana umasikini) na kuongezeana ma-stress tu.....hii ndio huwakosesha watu "bahati" ya kufanikiwa. Bana mie ningekuwa sijui nani ni nani Serikalini halafu kuna nafasi za kazi zinapatikana unadhani nitakuajiri wewe wakati nina Mpwa wangu (Jamaa) anaelimu na ujuzi ka' wako nyumbani? Aiii nitampa nafasi yeye kwanza, akiikataa ndio wewe wa Nje utafikiriwa. Najua sheria za kazi na kadhalika BUT Mpwa wangu sio Ndugu yangu, hatu-shei damu wala Ubini sasa undugu unatoka w