Tuesday, 19 August 2014

Mtu chake...

Kwa kawaida mimi sina tabia ya kuangalia watu ninapokuwa natembea na hata kama nimekaa mahali nitakuangalia kama nimependa ulichovaa....na kuangalia kwenyewe ni kwa Sekunde chache tu.


Kuna watu wanajua kukodolea macho wenzao bila kupepesa! Yaani anakukazia macho mpaka unaona aibu kwa ajili yake!

Ukitaka ugomvi na watoto wa London wale wa Uswahilini bana wakazie Macho hivyo....anakufuata na kukuuliza "what you looking at?" huku kashikilia Kisu!

Kisu bit pale juu nimeongezea tu chumvi, ila kuna vipigo na vifo kadhaa vilitokea kutokana na mtu kumkodolea macho mwenzie.

Stori time: Sasa jana tupo mtaani tunatembea na watoto....nyie mnatoka Weekend sie twatoka J'tatu....kisa na sababu? Ili tusiwe sawa, hakuna lingine wacha kutuJAJI eeh!

Nasikia Asali wa Moyo analalamika "mijaume ya kiafrika sijui ikoje (yeye mwenye Muafrika) inamkodolea macho mke wa mtu wakati inaona kabisa yupo na Mtu wake"

Hee! Nkauliza kwani wewe umeonaje kama wananikodolea macho kama wee mwenyewe hujawakodolea?!!

Akanijibu kwa kifupi, "mtu chake"!....nkafurahi Moyoni kabla sijajiuliza maswali kadhaa kuhusiana na yeye kuwa Mwanaume wa Kiafrika!


Asali wa Moyo akampeleka Babuu kwenda kuangalia makorokocho(Toys), mie nkawa nimekaa sehemu na Kibibi(kabinti) nampatia Lishe.....Mara akaja Mkongo, akaomba direction, nkampatia kisha akasema "ningependa kukujua zaidi, nikupe namba yangu?" Nkasema akuu sina Simu mie.Babai.
Mapendo tele kwako...

No comments: