Udini unatutenga, Udini unasababisha watu wasifanye mambo kwa uhuru, Udini hukosesha watu wake/waume wema n.k.
Hivi unajua kuwa Dini zililetwa na Wageni ambao sasa ama hawazifuati au wameamua kubadilisha waliotuaminisha kuwa "yaliandikwa" na nani sijui nani.
Halafu Waafrika tunaanza kuwaona namna gani vipi hawa jamaa wanatubadilishia Maneno ya kwenye Vitabu vyetu vitakatifu ili kuendana na "maisha" ya sasa! Ama kweli Dunia imefikia mwisho.
Tunajipa Moyo na kushikilia Imani zetu tukiamini kuwa ni za kweli na kuponda hao Wageni (Wamagharibi na Waarabu waliotuletea hizo Dini) kuwa ni Wafuasi wa Shetwani.
Baada ya wao kuchoshwa na Imani mbili tangu Miaka 2000 iliyopita wengi wao wakaamua ama kuachana nazo au kuanzisha nyingine ili ku-suit maisha yao ya Nyakati hizi.
Sasa wewe unapoteza Muda wako wote kujaribu kuwalisha wenzako Maneno yasio na ukweli (nani mwenye Uhakika kama yaliyomo kwenye Vitabu Vitakatifu yalisemwa na Allah/Mungu au Yesu?....thibitisha basi kama ulishuhudia....hihihihi).
Mie sifuati maneno ya kwenye Vitabu vitakatifu, lakini namuamini Mungu....naamini kuwa yupo mahali na hunisikiliza bila kuuliza Maswali katikati ya maelezo yangu pale ninapomshukuru, hutekeleza kwa wakati wake pale ninapomuomba....(mmh ila siku naumwa Uchungu wa kuzaa bana my 1st born Mungu alinichunia, nilimuomba nisisikie Maumivu hata kiduchu).....liache hili!
Wageni (Wamagharibi na Waarabu) wakija na Dini zao mpya, Jinsia Mpya sijui Haki mpya mie walaaa sina habari kwasababu najua Mungu wangu ni Mmoja na ananisikiliza.
Nilikuambia napenda kusikiliza Mawaidha....sasa kuna Mazuri na ya kufunza/ongoza, Mabaya, yakerayo na kupotosha jamii.
Kuwa makini na ma-information uyapatayo via Mitandao, Simu na ndugu zake....kumbuka kuchuja.....chukua yenye maana kwako mengine yaache yapite.
Imani ni choice ya life style (in my head) tusilazimishane bana eeh!
Babai.
Mapendo tele kwako...
Comments