Kwa siee wa Ulayani huwa tunapenda sana zawadi kutoka Nyumbani, zawadi (Radha ya Nyumbani) kama vile Ubuyu, Mahindi Mabichi*, Matembele ya Kukausha, Dagaa wa Kigoma, Viuongo vizima vya Pilau, Maembe Dodo au Embe Tanga bila kusahau Embe Ngong'a(unazijua?!!), Maharage ya Mbeya au yale ya Njano, Njugu Mawe n.k.
Mimi binafsi huwa napata hizo mavitu moja kwa moja kutoka kwa Mama, lakini kwa wale wenye Wenza wanaopenda kwenda Bongo Mara kwa Mara huwa wanavipata moja kwa moja kutoka kwa Wenza wao.
Tatizo ni kuwa Mwenza anapokuletea zawadi wakati mwingine inakuwa imetoka kwa Mme/Mke mwenzio bila wewe kujua.
Inasemekana wenzetu walioungana na "rangi" tofauti huwa wana-miss sana "rangi" yao hivyo wanaporudi Nyumbani huwa rahisi kupata wanawake/wanaume ambao huwapatia kile wanachokikosa kutoka kwa wenza wao Weupe....Maisha yaha....namaanisha Haya!!!
Halafu kuna wale ambao wanapenda tu kulala hovyo(Malaya)....Ujue! Ili uendelee kuwa interested na Kimada wa Kiume/Kike kila unapotoka Ughaibuni ni vema kuonyesha unaipenda Familia yake (ili akuamini) na hapo ndipo suala la Zawadi linapokuja!
Mke/Mume anarudi kutoka Bongo na makilos ya kila kitu nilichokitaja hapo awali, hadi dawa za Miti shamba.....hihihihihi mambo ya "radha" ya nyumbani!
Mwenyewe unapokea kwa furaha ukidhani zatoka kwa mwenza kumbe ni kwa Mke/Mume mwenza! Mara unaanza kumchukia Mumeo/Mkeo bila kujua sababu.....hehehehehe.
Kabla hujanijaji! Mama amekuwa na tabia ya kuniandalia mavitu hayo akijua naenda au kuna mtu anaenda so nina uhakika havitoki kwa "mwenza" bali Mama yangu mpendwa.
Halafu anavyojua kuvifunga sasa, hehehehe nadhani ni kwasababu ya "security" Uwanjani.....amekuwa akifanya hivyo Tangu sijakutana na Mume wangu. Enzi nasoma!
Isitoshe hakuna mtu anakula "radha" ya Nyumbani bali mimi peke yangu.
THE POINT is........
Babai.
Mapendo tele kwako...

Comments