Leo si Halloween bana, wacha nami niungane nao kwa kuzungumzia Wafu.
Jana tulikuwa (Mimi na Asali wa Moyo) tunaangalia Tv, mara Tangazo la Documentary ya Ebola (Ebola crisis) hilooo!
Nkasema mie sipendi kuona/onyeshwa miili ya wafu hata kama imefunikwa(hifadhiwa vizuri), kama wameenda wameenda tu hata mkituonyesha haifanyi Ebola kuwa Hatari zaidi ya ilivyo!
Mwenzangu akasema, "mie sielewi kwanini watu hupenda kwenda kutoa "Heshima" za mwisho wakitegemea kumuona Marehemu kwa mara ya Mwisho, marehemu ambae hawakuwa nae karibu kama Ndugu(wa Damu). Kwanini utake kumuona Mtu akiwa Maiti?
Nikakumbuka Msiba wa Marehemu Kanumba(Mungu akuongezee heri huko uliko, Ameen), ambao sasa umekuwa (in my head) kama "model" ya Misiba ya MaCeleb wa Bongo kwa Uwingi wa watu....*whispering* nasikia MaCeleb wa Kibongo wanaombea nao wajekuzikwa na watu wengi kama huyo nliyemtaja!
Walioshiriki walilalamika na wengine kukasirika kwanini hawakupewa nafasi ya "kumuona" Marehemu kwa mara ya mwisho!
Waingereza waliotuletea "utaratibu" wa Kuaga Marehemu kwa kuiangalia Maiti hawafanyi hivyo tena kwasababu wanakiuka Haki za Marehemu (Binaadamu) husika....unless alisema kwa maandishi kuwa anataka kuonwa akiwa hana uhai.
Sasa leo nilikuwa Duka la Madawa nasubiri Dawa(wanangu wanakohoa kwa Mashindano.....ahsanteB *nahisi umenipa pole*).
Pembeni alikuwa amekaa Mmama mmoja Mweupe(Mzungu), kachangamkaa, kama kawaida akaanza Stori...mara nikamaliza yangu (pata Dawa) nikamuaga.....akasema "am trying to be nice to everybody, because I don't know who'll look after me in a Nursing Home or Hospital".....mie nkatabasamu nkasema "aww how kind"....Do I look like a....never mind!
Point hapa ni kuwa, kwanini tunapenda kuhofia nani atanizika....nani atakuja kwenye Msiba wangu na kuishia kujenga urafiki na watu wengi ambao ni Maadui!
Hebu tujaribu kuwa nice/kind kwa kila mmoja wetu bila kurafikiana kwa kuegemea kwenye kuhofia nani atatusaidia Hospitalini au tutakapopata Udhuru mahali ambapo hakuna umjuae/akujuae.
Babai.
Mapendo tele kwako...
Comments