Skip to main content

Mtoto wa Kiume vs Wa Kike....

....wanatofautiana kwenye kila kitu, kuanzia utungwaji wa Mimba zao mpaka wepesi wa malezi, Ulaji wao na bila kusahau Ughali na Urahisi wa Mavazi. Kwa uzoefu wangu so far Mtoto wa Kiume ni rahisi ku-deal nae kuliko wa Kike(labda ni Homono).....Lakini Mtoto wa Kiume ni Ghali kuliko wa Kike linapokuja suala la Toys na Mvazi.




Tukiacha tofauti hizo na nyingine ambazo wewe unauzoefu nazo, bado wote ni Watoto na wanahitaji Upendo, Mafunzo, Elimu, Ulizi etc sawa sawa. Natambua kwa Wazazi wetu ilikuwa tofauti, kwamba Msichana alikuwa akilindwa zaidi kuliko Mvulana. Baadhi ya Wazazi wa sasa bado wanaendelea na "Kasumba" hiyo ambayo mie nahisi kuwa imepitwa na wakati(inaharibu upande mmoja).




Ni imani iliyojengwa miongoni mwetu kuwa Mtoto wa Kike ni "dhaifu" na hivyo ni rahisi kushawishika na kufanyiwa mabaya/kuharibiwa kuliko Mtoto wa Kiume.  Hii inafanya kuongeza "ulinzi" na Elimu juu ya "Watu wabaya" dhidi yao. Inasahaulika  kuwa huyu Mvulana(mtoto wa Kiume) nae ni Mtoto, hakuzaliwa Mwanaume na kujua kujilinda, hakuzaliwa tu na kuwa Imara,Kujiamini n.k. Huyu Mtoto wa Kiume anajifunza haya mambo kutokanana mazingira yanayomzunguuka lakini zaidi ni jinsi Wazazi wake mnavyomfunza  (kama mfanyavyo kwa mtoto wa kike).





Waharifu/Watu wabaya/Waovu siku zote hutafuta mbinu mpya ili kufanya Ushetani wao, sasa tangu Wazazi tume-relax kwenye Ulinzi kwa Watoto wa Kiume dhidi ya Watu waovu, tumefanya watoto wetu wa Kiume kuwa "easy target"! Kwa maana nyingine tunakuwa Sexit kwa watoto wetu. Umesikia mara ngapi Vijana wa Kiume wa miaka 8-16 wanajiua au wanauwawa kutokana na Unyanywasaji wa "Wavulana" wenzao(wengi ni Wanaume watu wazima aka Pedo).




Kutokana na Era ya "Smart kilakitu", unaweza kusema Malezi yamekuwa rahisi, lakini mimi binafsi naona kuwa Malezi kwa Watoto wa leo ni Magumu kwasababu, ili kuenda sambamba  na Wanao nilazma ujifunze masuala ya "code" na kwenda nao sambamba na Technology....kwa maana hivyo tunarudi "shule" kila siku ili ku-keep up.....juu ya Kazi zako, wajibu wako kama Mzazi kwao, Bills, Majukumu ya Nyumbani  kama Mke/Mume n.k.





Sasa hii "Smart kilakitu" inapendwa zaidi na Watoto wa Kiume, kwasababu naturally wao ni "fixers"  na "Technical" sio (weka Ufeminist kando),  wengi wao wanapenda Games na ku-code, kutengeneza Apps, kujenga TV au PC n.k. wenyewe katika Umri mdogo.




Mara nyingi  yote hayo hupatika kwa urahisi ikiwa Mtoto atakuwa connect Online na huko ndiko hujenga urafiki na "watoto wengine" ambao actually sio wa Umri wake bali ni watu Wazima wanaopenda watoto wadogo wa Kiume(Pedos). Nia yao ni ku-Groom watoto hao na kuwa-abuse na pengine kuwaua au kuwasukuma  wajiue kwa kuwa-troll ili majamaa waendelee kufanya Uhalifu wao.kama ambavyo baadhi ya Wanaume hufanya kwa watoto wa kike ambao luckly tunawalinda zaidi ya wenzao wa Kiume.




Watoto wa Kiume wanahitaji Ulinzi sawia kama wale wa Kike, Watoto wa Kiume wanakuwa Groomed pia. Nimechoka ku-type, naamini umepata Mwanga wa nini hasa nilitaka kusema. Ahsante kwa kuichagua Blog hii.


Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao