....wanatofautiana kwenye kila kitu, kuanzia utungwaji wa Mimba zao mpaka wepesi wa malezi, Ulaji wao na bila kusahau Ughali na Urahisi wa Mavazi. Kwa uzoefu wangu so far Mtoto wa Kiume ni rahisi ku-deal nae kuliko wa Kike(labda ni Homono).....Lakini Mtoto wa Kiume ni Ghali kuliko wa Kike linapokuja suala la Toys na Mvazi. Tukiacha tofauti hizo na nyingine ambazo wewe unauzoefu nazo, bado wote ni Watoto na wanahitaji Upendo, Mafunzo, Elimu, Ulizi etc sawa sawa. Natambua kwa Wazazi wetu ilikuwa tofauti, kwamba Msichana alikuwa akilindwa zaidi kuliko Mvulana. Baadhi ya Wazazi wa sasa bado wanaendelea na "Kasumba" hiyo ambayo mie nahisi kuwa imepitwa na wakati(inaharibu upande mmoja). Ni imani iliyojengwa miongoni mwetu kuwa Mtoto wa Kike ni "dhaifu" na hivyo ni rahisi kushawishika na kufanyiwa mabaya/kuharibiwa kuliko Mtoto wa Kiume. Hii inafanya kuongeza "ulinzi" na Elimu juu ya "Watu wabaya" dhidi yao. Inasahaulika kuwa huyu