Hakika! wao kwanza kabla ya watu wengine baba yao included(hello Asali wa Moyo hihihihi). Hata mie nimewahi kusema/kuwaambia watu kuwa Wanangu kwanza halafu wengine na mengine ndio yanafuta.
Nakumbuka nilikuwa na mwambia Mama, "nikija kuwa na mtoto, sitoruhusu mtu amshike....hata baba yake" hapo nilikuwa sijui Uchungu wa Mtoto wala Emotional connection na Bond kati ya Mimba/Mtoto na Mama. Nilihisi kuwa mtoto yupo Salama zaidi akiwa na Mama(nadhani ni Nature tu).
Baada ya kuwa Mama hakika Wanangu waka wa kwanza kabla ya lolote kubwa au dogo. Maisha yangu yakazunguukwa na Wanangu na kila kitu kinachowahusu. Ikafikia mahali nikaanza kuhisi sifurahii hii "biashara" sijui "kazi" ya kuwa Mama. Ikawa too much mpaka nikasahau mimi ni nani.
Nikasoma mahali (ukinipa mtihani wa Mimba, Kuzaa na kukabiliana na shida/mabadiliko ya kuwa Mama early days baaya ya kuzaa nafaulu zaidi ya Kufaulu), maana sijawahi kusoma in my life kama nilivyosoma/ninavyosoma kabla ya Mimba ya Babuu mapaka leo.....bila shaka nitaendelea kusoma ili kujifunza zaidi kutokana na uzoefu wa watu wengine. Achana na hili.
Nilipomaliza kusoma nikajifunza kuwa Mama mwenye furaha anasababisha furaha ya Familia yake na hivyo watoto kukua Vema Kiakili, Kimwili, Kihisia na Ki-sosho. Sasa je utakuwaje Mama mwenye furaha?
Niliamini kuwa hakuna tatizo kwenye Uhusiano(ndoa yetu) so i was(still am) actually happy na kila kitu, isipokuwa hii "biashara" ya My kids first inaniondolea furaha kwa kuchoka Kimwili n a Kiakili, so wanangu ndio Tatizo? Hapana....Tatizo lilikuwa ni Mimi kuwaweka wao Mbele na kujisahau/kutokujua kuwa Mimi ndio Nguzo na hivyo napaswa kuwa Imara.
Mimi ndio nilitakiwa kuwa Mbele, Mimi ndio nilitakiwa kuwa wa Kwanza kabla yao ili niweze kuwaangalia na kuwatunza kwa Umakini bila kuwa na Mzigo wa Uchovu na Mawazo ya "nimepoteza Utambulisho" wangu!
Haya ndio yaliyonifanya nianze kufurahia tena Maisha kama Mama;-
1-Nalala na Kuamka Muda ule ule kila siku(kuepuka mwili kuwa comfused).
2-Naamka mapema....nusu saa kabla ya watoto na kujiandaa/pendezesha(huwa naoga Usiku tu so time saved),
3-Nafungua Madirisha
4-Watoto wanaamka Saa Moja na Nusu (sijui huwa wanaamshana hehehe)....nawaandaa wote kwa pamoja.
5-Tunafungua Kinywa Pamoja
6-By Saa 8:40am tunatoka kwenda Mdondosha Babuu Shule.
7-Narudi na kuendelea na Mipango Mingine ya Siku husika.
Nafanya Mzoezi Mara 3 kwa Wiki (Nyumbani sina pesa wala Muda wa Gym), nafanya Mazoezi Jioni kwasababu Naoga Usiku/Jioni tu. Kufanya yote hayo kwa Mpangilio huwa kunanifanya ni "look forward" kwa siku inayofuata.
Kuhitimisha: Wanangu wanakuja baada ya Mimi. Hivyo mimi kwanza, Watoto pili, Baba yao tatu, familia yangu(wadogo zangu na Mama).... halafu mengine na wengine hufuata.
Je wewe Mama mwenye watoto wadogo, huwa unafanya nini au unafuata mpangilio gani ili kufurahia Umama wako bila kuhisi kuwa "umepotea".....sio Dinah tena bali MamaBI au Mke wa DK(mie).
Naheshimu na Kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments