Binafsi naamini kuwa sio sahihi kumuita mtu majina ambayo unauhakika ukiitwa wewe hutofurahia iwe ni kweli upo hivyo au la! Mfano unapomuita Mwenzio Malaya unapaswa kuwa na Uhakika kuwa Baba ni Baba yako kweli (una DNA bila rushwa).
Utamponda huyu hajitumi au Utaiponda Ofisi yake? |
Sasa kwa sababu tu wewe umezaliwa au kubahatika kuwa na shughuli ya kufanya huna haki ya kuwalaumu na kuwaita majina mabaya kama vile Tegemezi, wanapenda kuomba-omba Wavivu, Wazembe, Waoga, Masikini wa Fikra n.k.
Pia wewe wa Ughaibuni, kwavile tu wewe unaishi huko ulipo na kuona Maisha ya baadhi ya "wenye Nchi" mazuri na ukapendezwa na labda utaratibu wa Serikali na kudhani Utaratibu huo umewekwa na "wananchi" hao kwa sababu sio Wavivu/Wazembe au majina yeyote machafu unayowaita Watanzania wenzako basi tambua kuwa unakosea.
Kabla ya kuanza kumlaumu na kumshutumu Mtanzania mwenzio kuwa matizo yake yanasababishwa na yeye kuwa mvivu au kutopenda kujituma au kufanya kazi kwa bidii (wakati hakuna Kazi).....unahitaji kujua Chanzo kinachosababisha yeye kuwa hivyo unavyodhani alivyo.
Chanzo cha Matatizo ya Mtanzania au Umasikini wake na mengine yote unayomuita ni Utaratibu wa Serikali yake! sasa kama unataka kumsaidia Mtanzania huyu unapaswa kupigana ili "system" ibadilike na kusababisha mabadiliko ya "Kacha" ya Uvivu, Uzembe, Kuomba-omba n.k.
"Kacha" inatengenezwa na hivyo inaweza kubadilishwa.....kabla hujaanza kubisha unapaswa kujua Tofauti ya Utamaduni aka "Kacha" na Desturi. Desturi haibadiliki, lakini Utamaduni unaweza kubadilika kwa sababu ya Maendeleo au Mabadiliko.
Utamaduni hubadilishwa haraka kwenye Nchi husika kulazimisha Jamii kuishi kwa namna fulani, namna hiyo inaweza kuwa ya Kifukara, Kati au Juu. sasa ili Wananchi wabadilike nakuicha "kacha" ya kuomba-omba au Uvuvu ni wazi kuna Ulazima wa "system" kubadilika na kuweka sheria Mpya zinazotekerezeka.....kuondoa Mgawanyo mkubwa kati ya Masikini na tajiri.
Kwasababu Umeishi Ughaibuni na kuona kuwa Wazungu ni watu wenye Bidii na Kujituma which is kweli kabisa lakini sio wote. Unadhani kwanini wanabidii na kujituma? Kwasababu kisheria wanapaswa kulipa Bills zao kwa wakati na wakikosa wanalipishwa "riba" sio tu kwenye Wanavyomiliki bali pia Bank inawalipisha kwa kutokuwa na pesa kwa wakati husika ambao ulijua unapaswa kulipa Bills zako.
Kuna utaratibu wa kusaidia wasio na Kazi(Benefit), Utaratibu huu ulifanya wananchi hao unaoamini kuwa wanajituma na wana bidii ya kazi (Wazungu) kuwa Wavivu nakutegemea "kukinga mikono", hii ikawa "kacha" na hivyo watu wengi wakaamua kuacha kujituma na badala yake kukaa Home na kutukana wenzao via Sosho Midia, kuangalia Tv na kucheza Games kwenye PC.
"Kacha" hiyo ikaharibu Uchumi wa Nchi kwasababu Serikali ilikuwa inatumia Pesa zaidi kuliko kuingiza na Matokeo yake wakaamua kubadilisha utaratibu na hivyo kubana Kipato cha "Benefit" ili watu warudi Makazini.....umeona sasa?!!
Watanzania wanajituma sana tu (angalia Machinga na Mama Ntilie, Wauza Sokoni,Wlanguzi n.k), sema Utaratibu wa Serikali yao unawaangusha. Naamini Vijana wanauweza na nguvu ya kufanya kazi na wanania ya kujituma......lakini sasa utajituma kwenye nini wakati hakuna Kazi?
Serikali ikibuni Ajira na kuweka "thamani" ya ajira kwa kuwa na kiwango cha malipo na kisheria lazima wafanya kazi walipwe hivyo au zaidi na sio chini ya Kiwango husika. Pia kuondoa "kacha" ya kila kazi kuhitaji "Kiwango cha Elimu ya Digrii kwa kazi ya Uratibu Ofisi".....Karatasi pembeni waangalie nia ya mtu na Uwezo wake wa kufanya Kazi husika(kutokana na Mahojiano), kuwe na utaratibu wa kufundisha kazi with Malipo then "Kacha" ya kusubiri kusiaidiwa au kukinga mikono, Uvivu na Uzembe itaondoka/isha.
Kama huna uwezo wa kubadilisha chanzo cha Watanzania wenzako unaowaita Wavivu/Wazembe, hawajitumi au pengine huijui Siasa wala System ya Nchi yako hakika kaa pembeni na uwaachie wenyewe. Bora nisome Makala/Twiti kutoka kwa Muandishi(sio lazima awe Habari bali muandikaji mzuri na anaejua Siasa kwa mbali) kuliko kuambiwa na Celeb au Star kuwa Watanzania ni Wavivu/Hawajitumi, wanapenda kungojea wasaidiwe.
Wewe ni Celeb wa uhakika au Uchwara, una Mikataba na Projects zaidi ya tatu kwa Wiki moja, ni rahisi kwako kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwasababu kuna "kazi" na umesaini kuzifanya na usipozifanya hakika utakosa Kipato(na mialiko itakauka) na utashtakiwa/Daiwa....sijui naeleweka!
Kwa kawaida sifanyi Siasa(siku hizi) lakini here we are! Nathamini na kuheshimu Muda wako hapa, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments