Skip to main content

Posts

Showing posts with the label wajinga

Wale wasema "Watanzania" Wavivu/Wazembe/Waoga...

Binafsi naamini kuwa sio sahihi kumuita mtu majina ambayo unauhakika ukiitwa wewe hutofurahia iwe ni kweli upo hivyo au la! Mfano unapomuita Mwenzio Malaya unapaswa kuwa na Uhakika kuwa  Baba ni Baba yako kweli (una DNA bila rushwa). Utamponda huyu hajitumi au Utaiponda Ofisi yake? Sasa kwa sababu tu wewe umezaliwa au kubahatika kuwa na shughuli ya kufanya huna haki ya kuwalaumu na kuwaita majina mabaya kama vile Tegemezi, wanapenda kuomba-omba Wavivu, Wazembe, Waoga, Masikini wa Fikra n.k. Pia wewe wa Ughaibuni, kwavile tu wewe unaishi huko ulipo na kuona Maisha ya baadhi ya "wenye Nchi" mazuri na ukapendezwa na labda utaratibu wa Serikali na kudhani Utaratibu huo umewekwa na "wananchi" hao kwa sababu sio Wavivu/Wazembe au majina yeyote machafu unayowaita Watanzania wenzako basi tambua kuwa unakosea. Kabla ya kuanza kumlaumu na kumshutumu Mtanzania  mwenzio kuwa matizo yake yanasababishwa na yeye kuwa mvivu au kutopenda kujituma au kufanya kazi k