Mwaka huu November inatimia Miaka 20, sasa sio mbaya kama nikiweka kumbukumbu zangu za safari yangu ya Shule kuanzia Msingi mpaka Secondari(intro hiyo hihihihi).
Siku ya kwanza naingia kama Mwanafunzi wa Kidato cha kwanza ili kuwa ngumu maana hakukuwa na mtu nilietoka nae Msingi. Wengi walikuwa wanajigawa kwa makundi kwasababu wanajuana kwa kutoka shule moja ya msingi ama shule zao zilikuwa jirani. Kulikuwa na Wanafunzi kibao kutoka Mlimani Shule ya Msingi, Olympio na Upanga(wajuajiii, mabishoo, Kiingereza kingii).
Ikabidi nitafute namna ya kujiunga nao, maana kati yao watakuwa na mimi Darasa moja.....nikaanza kutumia Tiketi ya Kuiba (naongea Kiingereza kwa Nyimbo hihihihihi). Nilikuwa najua nyimbo nyingi ahsante "Double Compact something Cassete Music system".....unaweka Compact yako halafu unasimamisha ili kuandika mstari wa Wimbo husika. Nilikuwa na "book" full of nyimbo za RnB.
Baba(Mungu amrehemu) alikuwa anatununulia hizo eti tujifunze Kiingereza(hahahahaha) wengine mpaka leo hatujui Kiingereza na tunaishi na kufanya kazi Uingereza daah! achana na hili.....Basi nikaaa pembeni na Miatu yangu Mieupe ambayo 2002 ni Wazee tu ndio walikuwa wanavaa.(imerudi kwenye fashion though) nikaanza kuwa busy kuimba TLC's baby baby baby.
Viatu vyangu vilikuwa exctly like this....nilikwa na Nyeusi na Nyeupe |
Mara Kengere ya Mstarini ikagongwa....zikaanza Risala za kutukaribisha nini na nini. halafu kupangwa Madarasani nakujitambulisha. Kwenye kujitambulisha nikatupia Tiketi nyingine ya " iaemu zionli pyupu to pass to zisi schooli fromu mai skuli" excactly like that.....nikapigiwa Makofi. Sasa kuimba na kuja Foronda peke yangu kati ya watoto Mia Sita waliofaulu Shuleni kwetu aii nikawa popular.
"Dinah unaweza kuimba wimbo huu.....Dinah nani ali-produce wimbo huu?".... zikawa nyingi hihihihihi. Nikaona hizi toto za "wakubwa" sio Level yangu....nikaanza kujichanganya na kila mtu. Kila siku nabadilisha Group....Darasa zima wakawa "marafiki" zangu. So hii sina "Best friend" imeanza kitambo sana bila mimi kujua.
Naheshimu na Kuthamini muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments