Skip to main content

Posts

Showing posts with the label muziki

"Sheria" ya wa Ughaibuni kuwaletea Zawadi/kuwalisha Bata...

....nani aliiweka? au ndio mambo ya Mgeni karibu wenyeji tupone? Nakubali upatikanaji wa vitu ni rahisi zaidi huku kuliko Tanzania, lakini hiyo haina maana kuwa ukusanyaji(ununuzi na utunzaji) wa  makorokocho(vitu) na kusafirisha ni Rahisi pia! Ukiachilia mbali hilo, pia badhi yetu tunapokuja Nyumbani ni kwa ajili ya mambo  mengine na sio kulishana Bata kwenye sehemu mbalimbali za Kisasa hapo Nchini. Tandika Sokoni Eti wanataka ujisikie kama "upo nyumbani" kwa kukupeleka/tembeza meneo ya "Kisasa" ambako wanauza mavyakula(sumu) na vinywaji kama vya huko utokakao. Ukweli hapa sio wewe, bali wao ndio wantaka kenda kufanya watakayo kwa kutumia Vihela vyako vya huko utokako. Stori time: Nimerudi zangu Bongo na Mwanangu wa kwanza, tena akiwa mchanga(miezi 8). Kiutamaduni ndugu na jamaa hakuna kumshika mtoto "mikono" mitupu si ndio? heeee! Mwanangu kashikwa na Mikoni Milioni na hakuna hata mmoja aliemshikisha "Senti"....well isipokuw

Siku ya kwanza Kidatoni...Miaka 20 tangu Secondary!

Mwaka huu November inatimia Miaka 20, sasa sio mbaya kama nikiweka kumbukumbu zangu za safari yangu ya Shule kuanzia Msingi mpaka Secondari(intro hiyo hihihihi). Siku ya kwanza naingia kama Mwanafunzi wa Kidato cha kwanza ili kuwa ngumu maana hakukuwa na mtu nilietoka nae Msingi. Wengi walikuwa wanajigawa kwa makundi kwasababu wanajuana kwa kutoka shule moja ya msingi ama shule zao zilikuwa jirani. Kulikuwa na Wanafunzi kibao kutoka Mlimani Shule ya Msingi, Olympio na Upanga(wajuajiii, mabishoo, Kiingereza kingii). Ikabidi nitafute namna ya kujiunga nao, maana kati yao watakuwa na mimi Darasa moja.....nikaanza kutumia Tiketi ya Kuiba (naongea Kiingereza kwa Nyimbo hihihihihi). Nilikuwa najua nyimbo nyingi ahsante  "Double Compact something Cassete Music system".....unaweka Compact yako halafu unasimamisha ili kuandika mstari wa Wimbo husika. Nilikuwa na "book" full of nyimbo za RnB. Baba(Mungu amrehemu) alikuwa anatununulia hizo eti tujifunze Kiinger

The Online Support....kwa Celebs!

Hata kwa sie ambao sio maCeleb is real.....unajua pale unapoungwa mkono na kupewa ushirikiano wa "kisaiba"(cyber) na kukufanya ujihisi umebebwa....unapendwa...unakubalika. Unahisi furaha na pengine kujiona Mashuhuri(mtu wa kawaida) au kuhisi Umashuhuri wako (kwako Celeb) umeongezeka na kupata Konfisensi ya ajabu ya kufanya lolote au chochote. Unajua ile umeweka Picha halafu unapata followers zaidi na wanakumwagia masifa.....wanaomba kuona zaidi na wewe unazimwaga picha za mapozi tafauti hihihihihi baada ya siku mbili wanakuja followers wapya(wale wale kwa account tofauti via device tofauti) na kuanza kukuponda.....unabaki kulia na kuita watu "fake friends". Inategemea ni nini hasa kimefanya upate support ya "Fanzi" aka followers wako Online.....kuna wakati unahisi kutaka kusema ukweli wako ulivyo na sio uongo wausikiao au ku-justfy na ku-share zaidi ya unachopaswa kusema/ku-share. Bila kuomba ushauri kutoka kwa "inner self" au bila kumsikili

The other woman kwa Kiswahili ni Kimada?

Jana nilikuwa masoma Magazine moja hivi nikakutana na stori ya mdada Mashuhuri kiasi cha kutosha Uingereza. Alikuwa akizungumzia suala la kuwa Kimada ukitumaini au kuomba kama sio kusubiri Mwanaume unaemuiba amuache mkewe na watoto wake ili mwanaume huyo awe na wewe full time. Akaongeza....Mume wa mtu alipomtokea kabla hajajua kuwa ni mume wa mtu alimkubali then Jamaa akamwambia ameachana na Mkewe na Talaka itachukua muda  kiasi hivyo sio mbaya kama wakilianzisha. Mkimama akagoma na kumwambia watatoka soon baada ya Talaka kukamilishwa kwasababu hataki kuwa sababu ya kuharibu Maisha ya Mkewe na Watoto wake. Akagusia kwa kusema....wanaume  Wazinzi huanza kukuvuta kingono via mitandao ya kijamii na kuomba uwaambie utawafanyia nini ikiwa utapata nafasi ya kuwa nao. Kisha huenda na kuponda maisha yao ya kingono na Wake zao kwako.....halafu wakiona upo interested wanaongeza "i wish my wife angekuwa open minded kama wewe"(wakati uliyomwambia ni masuala ya kawaida tu ambayo kila

Nakupa mapenzi alionipa Mama....

Unless hujui Elimu ya Viumbe Hai hasa kuhusu Mwanadamu utabisha na pengine kuwa offended. Unaeza kudhani kuwa Ali Kiba amemkosea adabu Mama yake na pengine ulajiiliza utampaje mpenzi wako Mapenzi aliyokupa mama obviously hayato tosh......halafu ukawaza ni mapenzi gani hasa mwenzetu alipewa eeeh! Well uhusiano wa kwanza wa mtouo yeyote ni ule wa yeye na Wazazi wake.....mtoto hajui kupenda mtu yeyote zaidi ya wazazi wake hivyo lolote analopata kuyoka kwa wazazi hao ni mapenzi. Linapokuja penzi la mama kwa mtoto wale wa Kiume au Baba kwa Binti yake kidogo kuna mkanganyiko na wengi hushindwa kuelewa lakini kama nilivyosema ikiwa kama unalijua vema Somo la Viumbe Hai baada ya High school(ambayo mie sikuipata hii ni another sitori ya siku ingine) utaelewa. Vitendo vya kimapenzi au upendo ambavyo Mama alitupatia baada ya Kuzaliwa na kipindi tunakua ndivyo ambavyo tunavifanya au tunapenda kufanyiwa na Wapenzi wetu tukiwa watu wazima kwa......mf kunyonyana Chuchu, kukumbatiana, kupeana mab