Skip to main content

"Sheria" ya wa Ughaibuni kuwaletea Zawadi/kuwalisha Bata...

....nani aliiweka? au ndio mambo ya Mgeni karibu wenyeji tupone?


Nakubali upatikanaji wa vitu ni rahisi zaidi huku kuliko Tanzania, lakini hiyo haina maana kuwa ukusanyaji(ununuzi na utunzaji) wa  makorokocho(vitu) na kusafirisha ni Rahisi pia! Ukiachilia mbali hilo, pia badhi yetu tunapokuja Nyumbani ni kwa ajili ya mambo  mengine na sio kulishana Bata kwenye sehemu mbalimbali za Kisasa hapo Nchini.


Tandika Sokoni



Eti wanataka ujisikie kama "upo nyumbani" kwa kukupeleka/tembeza meneo ya "Kisasa" ambako wanauza mavyakula(sumu) na vinywaji kama vya huko utokakao. Ukweli hapa sio wewe, bali wao ndio wantaka kenda kufanya watakayo kwa kutumia Vihela vyako vya huko utokako.





Stori time: Nimerudi zangu Bongo na Mwanangu wa kwanza, tena akiwa mchanga(miezi 8). Kiutamaduni ndugu na jamaa hakuna kumshika mtoto "mikono" mitupu si ndio? heeee! Mwanangu kashikwa na Mikoni Milioni na hakuna hata mmoja aliemshikisha "Senti"....well isipokuwa Mama yangu.




Baada ya muda wetu kuisha tukajikusanya na kurudi kwetu Ughaibuni, huku  nyuma watu wakaanza kulalamika kwamba tumekuja Tanzania Mikono mitupu....."Mwanamke hata zawadi looo!"."kutwa kutembea kwenye Masoko na Vichochoro badala ya kwenda Mjini...wajameni si nimewaletea Mpwa, Mjukuu, Kitukuu, Binamu, mwana kama Zawadi au? hihihihihi. Halafu ni hivi! ninachokuja kukiona ni kile mabacho sikioni Ughaibuni.....nafurahi kula vile ambavyo sili Ughaibuni, tatizo ni nini?



Inawezekana ni sisi wenyewe wa Ughabuni ndio tumewazoesha baadhi ya watu, kwamba tunaporudi tunatumia pesa ili "tupate heshima" au "wasitusahau".... Mimi binafsi nabeba zawadi kwa Wadogo zangu(nilichukua sehemu ya Urithi wao kuja Huku) so automatikali wana kwalifai au wanaamini kuwa ni Haki yao na ni Jukumu langu(Ukubwa shughuli).



Sasa, tangu nimezaliwa sijawahi kufika Mlimani City sijui ndio mnaiita Mall. Mie zangu Tandika Sokoni, Mwenge Sokoni, Kariakoo, Soko la Samaki Ferry, Kunduchi Sokoni na sehemu nyingine zote ambazo ni za kawaida.


Natumai Post hii imekupa tabasamu, kicheko, mshangao......vyovyote vile nashukuru kwa kuichagua Blog hii. Tambua nathamini muda wako.


Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao