....pengine how not to give a F*ck imekaa vizuri!! najua maana moja tu ya hilo neno F, nakumbuka Mwaka wa Kwanza Chuoni(when I was in London)....Jamaa mmoja alinambia "go f**k yourself" nkamwambia really?can you show me how?.....Darasa likawaka moto kwa kicheko. sasa sijui walikuwa wananicheka mimi(sijui Kiingereza) au jamaa. Achana na hili!
Kujali kuhusu kila kitu au mambo ambayo watu wanajaribu kukufanyia na kwanini wanafanya hivyo husababisha maumivu ya Hisia.....unajua ile hisia unayoipata(ulipokuwa mdogo) pale unapomsalimia mtu Mzima halafu haitikii? Unaanza kujiuliza huku "umia" Baba/Mama nanilihu kwanini haitikii "shikamoo yangu"(labda alikuwa anakutaka) but kwa umri wako mdogo unahisi kama vile umenyang'anywa kitu cha thamani kinachoitwa "Heshima kwa wakubwa" ambacho Baba na Mama yako walikufunza.
Mie binafsi nilikuwa nalalamika daily Watu Wazima wakinichunia, siku Marehemu Baba akanambia "kama hawaitikii Salamu yako basi usiwasalimie, achana nao" nkahisi huyu Mzee vipi? Unatufunza daily tuwe na adabu na kusalimia wakubwa wetu, leo unaniambia nisiwasalimie.....tena?
Tangu siku hiyo nikawa "Mwanzilishi" wa kuuchuna, nikiamini kuwa huwzi kunichunia mimi wakati mie ndio CEO hihihihihi silly eeh! Ukinichunia kwasababu ya issue zako za Kimaisha na mie nakuchunia milele. Hii imenisaida sana kwenye kutojali kuhusu watu wengine watanifikiriaje.
Ni rahisi sana kumwambia mtu asijali watu wanasema nini juu yake na kwamba yeye aendelee na Maisha yake, hasa kama mhusika ni Mdogo(20s). Unaweza kudhani kuwa Era hii ya Sosho Midia ni rahisi kwasababu kuna Memes, Ushauri wa Jinsi(hows) na Quotes kila kona. Uwingi wa hizo "makitu" ni kithibitisho cha ongezeko la Ugumu wa "kutokujali" watu wengine wanasema/fikiria nini kuhusu wewe au chochote ufanyacho.
Kila mtu Duniani anamaoni yake kuhusu kila mtu na kila kitu....Wakosoaji, wafuatiliaji na kila aina ya watu wapo huru na karibu zaidi na wewe(japo hawakujui) kuliko ilivyokuwa Miaka ya nyuma(wakati mimi nakua miaka ya 90).
Pamoja na kuwa sehemu ya kukosolewa huko kunaweza kukusaidia kufanya mabadiliko na kuwa mtu bora/mwema zaidi bado kama binadamu una hisia na unaweza kuumia kwa kiasi fulani na ukashindwa kufanya kile ufanyacho au kuboresha kile kilichokosolewa9inategemea na Uimara wako sio).
Kama kawaida, mimi nimeishi maisha tofauti sana na "dada yako" mkubwa na kwa muda mrefu kukupita wewe hihihihihi hivyo nitakupa Hows zangu za kutokujali Walimwengu wanasema nini, Kwanini na wapi? Chagua unalodhani unaweza kulifuata na kisha changanya na ya kwako na ya watu wengine ili kufanikiwa kwenye hili. Ila ukifanya haya (bila mpangilio huu)yote na kuchanganya na uyajuayo utanufaika zaidi. Twende sasa:-
1-Uvumilivu- Unapitia hayo yote kama sehemu ya Ukuaji, unajifunza along the way na the moment unaingia 28 utaona mabadiliko Makuu ya jisni unavyopokea na kuchukulia vitu/mambo. Haya unayopitia sasa utakutana nayo tena baada ya Kuolewa/Oa, yatahusisha watu ambao ni Muhimu kwa Mkeo au Mumeo....usipojifunza kuchukulia watu kama walivyo au kutojali sasa, ni wazi utaiona Ndoa ni Chungu na kuhisi umeolewa/Oa Ukoo Mzima.
2-Focus-Weka Focus yako kwenye mambo muhimu zaidi kwako kuliko mtu/watu wengine ambao sio muhimu. Unacotengeneza sasa ndio kitakachokusimamisha huko mbele kimaisha, iwe ni Elimu, Biashara, Mafunzo n.k. Pia Focus yako kwenye ufanyalo itasaidia usiwe na Muda wa "kujali" yasioyo na Muhimu.
3-Toa time out-Kwa Ndugu/Jamaa/Marafiki ambao ni wabaya/wasio na umuhimu kila baada ya muda(mie nilikuwa nafanya kila mwaka).....usisubiri mpaka wakukosee. Angalia tu ni nani anaumuhimu kwa sasa na ubaki nae karibu, wale ambao hawana umuhimu wachunie kwa muda. Hii huokoa muda na kupunguza Lawama.
Wazuri sio wale anaokuja kwako/kwenu kila siku au kukupigia simu kila siku na kuchat/catch up(kila siku?). Wazuri ni wale wanaoheshimu Muda na Nafasi yako....lakini ukipatwa na Shida watakuwa karibu na kusaidia kwa namna yeyote awezayo.
4-Jione/Tambua kisha Jisifie- Ukingojea kusifiwa, utangoja sana na ukitegemea Likes, RTweets tambua tu kuwa wasifiaji wa Online sio wakweli hihihihi (most of them). Sasa ni lazima utakuwa na moja (au yote)kati ya haya mf. Elimika(kishule au kidunia), mrembo/mtanashati, Imara, unamahali pa kulala(hata kama ni kwa mama/baba), unajilipia/changia bills, unafanya mambo na kufanikiwa bila mchango wao. Lolote zuri au unalojivunia wewe kama wewe.....Jipe sifa!

5-Jitolee Muda-Kusaidia wengine. Kumsaidia Mtu sio lazima umpatie pesa. Muda wako ni Mali tosha, na huitaji kujitolea Siku nzima.....somea watoto kitabu mara moja kwa mwezi/wiki, saidia wengine kujifunza somo ambalo ni gumu kwao lakini kwako ni jepesi. Fanya jambo kwa ajili ya mtu mwingine ambae hakuhusu(toa msada/saidia).
6-Jisomee...iweni Koran(Koroani), Biblia, Makala, Vitabu, itakusaidia kujifunza zaidi na kupata Amani.
-7-Usiogope kujitoa "mhanga".....Kama kuna issue inajadiliwa popote ulipo (kwa mfano)na unahisi kuwa unataka kuongezea, Uliza au kupinga with facts/points au kuunga mkono. Ingia kati na chukua sehemu yako na simamia usemacho lakini pia kubali kujifunza/elewa points kutoka kwa washiriki wengine.
-8-Usiogope kukosea..... lakini usikosee makusudi(makosa yatakusaidia kujifunza zaidi)
9-Jipe time off Sosho Midia, au kama unaweza chagua Platform Moja na usiwe kwenye kila Sosho midia "outlet". Kumbuka Dunia imekuwa Kijiji(Ahsante Teknolojia na urahisi wa kuifikia Internet), kwenye kila Sosho Midia utakutana na watu walewale na tofauti itakuwa majina labda, lakini mitazamo yao inaweza isibadilike. Sasa kama hawakupendezwa na wewe Insta hawawezi kupendezwa na wewe Snapchat etc.
-10-Kuwa Mbinafsi....ulikuja Duniani(ulizaliwa) peke yako na utaondoka(kufa) peke yako! So yeahaa don't give a fuck of what-who-where or why. Post hii nimelenga wadogo zangu, lakini kama wee umekua mwili tu na akili bado imebaki in your early 20s.....hongera kwa kuibamba Post hii.
Ahsante kwa kuichagua Blog hii na tafadhali share, tambua kuwa nathamini muda wako hapa.
Babai.
Comments