Skip to main content

Posts

Showing posts with the label 20s

Muendelezo wa Twiti yangu ya "if he is hot, don't let yourself go"...

Miaka mitatu iliyopita niliandika kuhusu Wanaume wapenda nachuro byuti, kama ilikupta isome hapa  kisha tuendelee. Kwanza habari za leo? mie nipo Likizo, aina ya Likizo ambapo unafanya yote uyafanyayo unapokuwa nyumbani isipokuwa haupo nyumbani. Achana na hili. Kuwa shabiki wa "natural beauty" wakati unavaa Nguo, unaoga maji Safi ya Bomba(yana Kemikali), unavuta hewa kila siku(imejaa toxic), unakula vyakula vinavyotunzwa kwa kutumia Kemikali ili kuepusha magonjwa/wadudu, Ukiugua unatumia Tiba ya Kisasa, Unatumia Simu kuwasiliana  n.k. sio rahisi. Hakuna tatizo la mtu kupenda Urembo wa Asili na hakuna tatizo kwa yeyote anaependa Urembo wa kununua/jiongezea ailimradi tu hambadilishi na kukufanya uonekane mtu mwingine. Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wanaume kusakama Wanawake wanaopenda kujiremba(usually wasio kuwa na pesa, maana makeups sio chee). Kutokana na maisha yalivyo  hivi sasa (Wanawake tunafanya yaliyokuwa yakifanywa na Wanaume pekee) na mabadiliko ya Hali

Jinsi ya kutojali.....au niseme jinsi ya kuto-give a damn?

....pengine how not to give a F*ck imekaa vizuri!! najua maana moja tu ya hilo neno F, nakumbuka Mwaka wa Kwanza Chuoni(when I was in London)....Jamaa mmoja alinambia "go f**k yourself" nkamwambia really?can you show me how?.....Darasa likawaka moto kwa kicheko. sasa sijui walikuwa wananicheka mimi(sijui Kiingereza) au jamaa. Achana na hili! Kujali kuhusu kila kitu au mambo ambayo watu wanajaribu kukufanyia na kwanini wanafanya hivyo husababisha maumivu ya Hisia.....unajua ile hisia unayoipata(ulipokuwa mdogo) pale unapomsalimia mtu Mzima halafu haitikii? Unaanza kujiuliza huku "umia" Baba/Mama nanilihu kwanini haitikii "shikamoo yangu"(labda alikuwa anakutaka) but kwa umri wako mdogo unahisi kama vile umenyang'anywa kitu cha thamani kinachoitwa "Heshima kwa wakubwa" ambacho Baba na Mama yako walikufunza. Mie binafsi nilikuwa nalalamika daily Watu Wazima wakinichunia, siku Marehemu Baba akanambia "kama hawaitikii Salam