Skip to main content

Muendelezo wa Twiti yangu ya "if he is hot, don't let yourself go"...


Miaka mitatu iliyopita niliandika kuhusu Wanaume wapenda nachuro byuti, kama ilikupta isome hapa kisha tuendelee. Kwanza habari za leo? mie nipo Likizo, aina ya Likizo ambapo unafanya yote uyafanyayo unapokuwa nyumbani isipokuwa haupo nyumbani. Achana na hili.


Kuwa shabiki wa "natural beauty" wakati unavaa Nguo, unaoga maji Safi ya Bomba(yana Kemikali), unavuta hewa kila siku(imejaa toxic), unakula vyakula vinavyotunzwa kwa kutumia Kemikali ili kuepusha magonjwa/wadudu, Ukiugua unatumia Tiba ya Kisasa, Unatumia Simu kuwasiliana  n.k. sio rahisi.



Hakuna tatizo la mtu kupenda Urembo wa Asili na hakuna tatizo kwa yeyote anaependa Urembo wa kununua/jiongezea ailimradi tu hambadilishi na kukufanya uonekane mtu mwingine. Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wanaume kusakama Wanawake wanaopenda kujiremba(usually wasio kuwa na pesa, maana makeups sio chee).


Kutokana na maisha yalivyo  hivi sasa (Wanawake tunafanya yaliyokuwa yakifanywa na Wanaume pekee) na mabadiliko ya Hali Nchi(are those words?) inakuwa  ngumu kwa Mwanamke kuonyesha "unamake wake" na hivyo wengi kujikuta wanakuwa kama Wanaume kima vazi, kimaongezi na wengine mpaka miondoko inabadilika hihihihi ili tu "kuheshimika" aka wasionekane wanavutia.
(Unajisemea ge to to the point Dinah hehehe nakusikia)


Wanawake tunapenda kuonyesha uanamke wetu kwa aina mbali mbali tofauti, nyingi huwa faraghani/nyumbani na chache kwenye kadamnasi mf, jinsi tunavyotembea, mavazi, kujiremba/pamba/jipenda,  jinsi tunavyo ongea, kula n.k.


Uanamke wetu huyumba tunapojifungua au tunapokuwa na Mwanaume ambae anadai kuwa anapenda nachuro byuti yako  huku yeye anajipendezesha na daily yupo "Hot" kimuonekano. na wewe unaonekana kama msaidizi wake na sio mwenza wake. lakini unajiachia tu na huoni sababu ya kujijali/penda/remba kwa sababu Mumeo anapenda Unachuro wako.


Mumeo ambae Hot sio anajipenda for nothing, huko endako anakutana na "hot" wenzie, anaona wanavyopata attention na pengine na yeye anazitoa na kuzipokea lakini hataki kabisa wewe uzipate na hivyo kumpa amani Moyoni kuwa Hakuna "hota" mwingine atakaevutiwa na wewe kwasababu sio "hot". Ana uhakika kabisa wewe huwezi kuvutiwa na "no so hot" kwasababu yeye ni "Hotter"...sijui umenielewa?


Kama mumeo anajipenda(ata asipojipenda) hakikisha unajipenda, unajijali....nyumba haihitaji wanaume wawili bali Mwanaume na Mwanamke, tumia uanamke wako kuweka tofauti hiyo wazi. Jirembe, Fanya  mazoezi(kwa afya sio kukonda), remba nyumba yako, usafi wa mazingira(sukuma mumeo na watoto wasaidie).

Marehemu Bibi yangu (mfundaji) alinambia "Ukiolewa sio ruhusa kwa wanaume wengine kuona Sura yako ikiwa Uchi, hiyo sura ni kwa ajili ya Mumeo tu hivyo jirembe"....mimi nakuambia ikiwa mumeo anavutia, mtanashati usijiachie Jirembe, pendeza,vutia.

Tambua nathamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Bai.

Comments

Unknown said…
Habari dada yangu, nataka kusoma ulichoandika miaka mitatu iliyopita inanigomea

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao