Skip to main content

Kuwa "affectionate" kwa Mwenza wako kunaweza haribu Ndoa/Uhusiano wenu...



Baadhi ya watu hasa Vijana wanapenda sana kuonyesha "hisia" zao kwa vitendo, katika umri mdogo ambao ndio kwanza unajifunza Ujinsia wako, "Affection" goes a long way. Katika hali halisi huitaji zaidi ya kuhisi unapendwa na  kupata uzoefu wa mwili wako unavyoibua Msisimko wa raha ambao hujawahi kuuhisi tangu Ubalehe/Vunje Ungo.


Wengi huamini wapenzi wanaofanya hivyo basi huwa na uhusiano/ndoa yenye Afya. Ukweli ni kuwa sio mara zote, sio tu kwamba kuna wakati mnajikuta hamna muda kutokana na mtindo wa maisha ya sasa bali inapoteza uzito/umuhimu(ni vema kuirudisha time to time).



Utajiuliza kwanini kuonyesha "hisia" zako kwa vitendo kuharibu uhusiano/ndoa wakati ukifanya hivyo unajisikia vizuri/raha na kuwa karibu zaidi na mwenza wako? Jibu ni rahisi tu, Kwenye Ndoa kuonyesha Hisia zako ni rahisi kuliko kukabiliana na "issues" kubwa au hata  kuchangia maoni yako au kumshauri mwenza wako labda kikazi, kifamilia(kule alikozaliwa), maendeleo n.k.



Pamoja na kuwa "affectionate" ni muhimu, kumbuka sio muhimu kila wakati kila siku, wakati mwingine Mume/Mke anahitaji zaidi kutoka kichwani kwako(Matumizi ya Akili) na sio kushikwa-shikwa(tomaswa), lambwa-lambwa(mabusu), nuswa-nuswa au kukumbatiwa na kunong'onezwa.


Stori time: Nimewahi kufanya kazi(ya kushauri) Pea moja kitambo hivi, Mke mtu alikuwa mzuri kweli kwenye kuonyesha "hisia" zake  kwa vitendo kwa mumewe wa Miaka 12. Lakini akawa anashangaa kwanini  siku hizi Mume wake haonyeshi furaha kama awali. Akawa anahisi labda mumewe kapata mtu mwingine nje ya Ndoa yao.


Mume mtu alikili kuwa anashukuru kuwa anaporudi kutoka Kazini Mkewe anampokea kwa furaha, kumkumbatia na kumpa mabusu kendekende, wakati mwingine kumuandalia "bath" maalum na kumkanda mwili ili kuondoa Uchovu. Lakini pamoja na yote hayo bado anahisi anahitaji zaidi kutoka kwa Mkewe, kwamba anahitaji Ushauri/changamoto na kuwekwa sawa zaidi ya kusikilizwa na kupozwa kwa "affection".


Natambua kuwa Wanawake wengi ambao ni "traditional" lakini tumetoa mavumbi machoni(mimi Mmoja wao) tunapenda kuwafanya waume wetu wajione "Wanaume" kwa kuonyesha nguvu yetu ya u-feminin. Tatizo baadhi hupitiliza au hawajui namna ya ku-balance the two. Kwamba kuwa wa Kizamani na wa Kisasa kwa wakati mmoja.


Ni muhimu kwenda na wakati lakini usisahau Asili ya Mwanadamu, Mwanaume anapenda kujiona/hisi  kuwa Uanaume wake unaheshimiwa na Mwanamke anapenda kuhisi Uanamke wake unathaminiwa. Lakini hapo hapo Ndoa/Uhusiano wa "ndio bwana" na too much affectionate hupelekea upande mmoja kuhisi haupati Changamoto na hivyo kwenda kuisaka kwingine au kuwa mkorofi(jinsi anavyo ongea na wewe) ili tu Usimame na kumuweka sawa.



Changamoto ninayoizungumzia hapa sio ya kuongeza Kimada, kama ambavyo baadhi ya wanaume Tanzania wanavyo amini kuwa ili Mkeo "achangamke" basi mtafutie mwenzie....hilo sio suluhisho bali unyanyasaji wa Kihisia, Kisaikolojia na Kakili kwa Mkeo na watoto wenu,


Changamoto ninayozungumzia hapa ni Mf: Mume kaleta  wazo la Mradi mpya na anakuelezea jinsi gani ataufanya n.k., wewe unaishia kumpongeza na kutoa maafeksheni yako, badala ya kuhoji na kutoa maoni yako kulingana na maelezo alioyokupa ili kumuongezea "ideas".


Au amekuwa akifanya Shughuli ile ile tangu mmekutana na haionyeshi kuboresha maisha yenu, badala ya kumpa changamoto  na kumsaidia/fanya awe "ambitious" wewe unaendelea tu kutoa mafeksheni yako na "ndio bwana" zako na kuishi kwa mazoea.


Wanaume hawafanani, kwasababu uliambiwa kwenu sijui kwenye Kitchen party au Imani yako ya Dini kuwa Mume habishiwi, mwanamke ni kukaa kimya haina maana Mume wako ni mmoja wa wale walio waoa hao watoa mafunzo.

Pamoja na yote, kumbuka Wanaume wengi wanapenda Changamoto.

Ahsante kwa kuchagua Blog hii. Nathamini muda wako hapa, mpaka wakti mwingine tena,


Bai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao