....nani aliiweka? au ndio mambo ya Mgeni karibu wenyeji tupone? Nakubali upatikanaji wa vitu ni rahisi zaidi huku kuliko Tanzania, lakini hiyo haina maana kuwa ukusanyaji(ununuzi na utunzaji) wa makorokocho(vitu) na kusafirisha ni Rahisi pia! Ukiachilia mbali hilo, pia badhi yetu tunapokuja Nyumbani ni kwa ajili ya mambo mengine na sio kulishana Bata kwenye sehemu mbalimbali za Kisasa hapo Nchini. Tandika Sokoni Eti wanataka ujisikie kama "upo nyumbani" kwa kukupeleka/tembeza meneo ya "Kisasa" ambako wanauza mavyakula(sumu) na vinywaji kama vya huko utokakao. Ukweli hapa sio wewe, bali wao ndio wantaka kenda kufanya watakayo kwa kutumia Vihela vyako vya huko utokako. Stori time: Nimerudi zangu Bongo na Mwanangu wa kwanza, tena akiwa mchanga(miezi 8). Kiutamaduni ndugu na jamaa hakuna kumshika mtoto "mikono" mitupu si ndio? heeee! Mwanangu kashikwa na Mikoni Milioni na hakuna hata mmoja aliemshikisha "Senti"....well isipokuw