Skip to main content

Nakupa mapenzi alionipa Mama....


Unless hujui Elimu ya Viumbe Hai hasa kuhusu Mwanadamu utabisha na pengine kuwa offended.


Unaeza kudhani kuwa Ali Kiba amemkosea adabu Mama yake na pengine ulajiiliza utampaje mpenzi wako Mapenzi aliyokupa mama obviously hayato tosh......halafu ukawaza ni mapenzi gani hasa mwenzetu alipewa eeeh!



Well uhusiano wa kwanza wa mtouo yeyote ni ule wa yeye na Wazazi wake.....mtoto hajui kupenda mtu yeyote zaidi ya wazazi wake hivyo lolote analopata kuyoka kwa wazazi hao ni mapenzi.


Linapokuja penzi la mama kwa mtoto wale wa Kiume au Baba kwa Binti yake kidogo kuna mkanganyiko na wengi hushindwa kuelewa lakini kama nilivyosema ikiwa kama unalijua vema Somo la Viumbe Hai baada ya High school(ambayo mie sikuipata hii ni another sitori ya siku ingine) utaelewa.


Vitendo vya kimapenzi au upendo ambavyo Mama alitupatia baada ya Kuzaliwa na kipindi tunakua ndivyo ambavyo tunavifanya au tunapenda kufanyiwa na Wapenzi wetu tukiwa watu wazima kwa......mf kunyonyana Chuchu, kukumbatiana, kupeana mabusu, kupapasana, hali ya kujali, kununuliana zawadi n.k.


Watoto nao hurudisha mapenzi hayo kwa wazazi wao.....well kwa mama tena zaidi kuliko Baba zao yaani mume husika. Hali hii hufanya baadho yetu kusahau kama kuna Mkibaba anauitaji affection pia.....sababu watoto wetu wanatupatia bila kusema kuomba yaani unamwagiwa  maafeksheni lundo daily kwa miaka ka 6 ya maisha ya mtoto bila "am not in mood" sababu ya stress za Kazi, ndugu, jamaa na marafiki.

Halafu mapenzi ya Mama hayaishi.....hayapungui wala kugubaa. Mapenzi ya mama ni ya milele hata kama mtakosana kibinaadamu (wakianza nataka mjukuu kabla sijafa .....simpendi mkeo).



I wonder kwanini watoto wa kike huwa hatupewi nafasi ya kupata uzoefu wa mapenzi ya Baba zaidi ya kupewa kidole  unyonye pale unapomsumbua hihihihihi usiende huko mxsii lione!



Anywaaaaaaay ukiachilia mbali kuwa napendezwa na Dogo (Ali Kiba) bado sioni kama amekosea kwenye Wimbo wa Chekecha.


Pamoja na kusema hivyo bado naelewa kwanini baadhi ya watu wanaeza kusema au kulalamika kuwa amekosea.



Hey you sogea hapa nikunong'oneze......you need to go out a bit more.....hihihihihi natania!....namaanisha you need to educate yourself sio unapoteza Muda na Data kusoma Udaku tu ambao haukusaidii.



Soma kuhusu Sayansi ya Viumbe na menhine ambayo unadhani kuwa huyajui au hukusoma ili kuepusha hali ya kuwa offended kichee.

Elimu kwenye Kiganja halafu hakuna Mtihani....how cool is that?

Babai

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao