Skip to main content

The other woman kwa Kiswahili ni Kimada?

Jana nilikuwa masoma Magazine moja hivi nikakutana na stori ya mdada Mashuhuri kiasi cha kutosha Uingereza.


Alikuwa akizungumzia suala la kuwa Kimada ukitumaini au kuomba kama sio kusubiri Mwanaume unaemuiba amuache mkewe na watoto wake ili mwanaume huyo awe na wewe full time.



Akaongeza....Mume wa mtu alipomtokea kabla hajajua kuwa ni mume wa mtu alimkubali then Jamaa akamwambia ameachana na Mkewe na Talaka itachukua muda  kiasi hivyo sio mbaya kama wakilianzisha.



Mkimama akagoma na kumwambia watatoka soon baada ya Talaka kukamilishwa kwasababu hataki kuwa sababu ya kuharibu Maisha ya Mkewe na Watoto wake.



Akagusia kwa kusema....wanaume  Wazinzi huanza kukuvuta kingono via mitandao ya kijamii na kuomba uwaambie utawafanyia nini ikiwa utapata nafasi ya kuwa nao.



Kisha huenda na kuponda maisha yao ya kingono na Wake zao kwako.....halafu wakiona upo interested wanaongeza "i wish my wife angekuwa open minded kama wewe"(wakati uliyomwambia ni masuala ya kawaida tu ambayo kila mwanamke anayafanya.).



Umeingia mtegoni ukidhani mjamaa kafika kwako kwani utampa mambo ADIMUUU. Siku ya siku inafika anakuambia "hatuhitaji Condom....nitatolea nje"....unakubali mara kabuumu Mwanaharamu katunga hihihihi samahani Kiswahili kitamu bana na hakina huruma....love child? No ya wazungu waachie Wazungu thank you....ni MWANAHARAMU.


Miaka mitatu imepita yule Jamaa bado yupo na Mkewe na wameongeza Mtoto wa tatu kwenye familia yao.



Nikamkumbuka Binti mmoja aliomba ushauri kwangu ili nimsaidie arudiane na Mpenzi wake ambae ni Mume wa mtu kwani anampenda sana Mume huyo wa mwenzie na hajawahi kumtenda wala kuingilia Ndoa yake.


Got it? Mpenzi wake ni Mume wa mtu lakini hajawahi kuingilia Ndoa yake.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao