Skip to main content

Faida ya kumchukia mtu usiemjua....

Ni nini hasa?

Unajua kuna watu maisha yao ni ya huzuni sana bila wao kujijua. Anakaa kabisa na kutulia kisha anaanza kurusha maneno makali. Unawezaje kum-attack mtu kwa matusi wakati humjui?


Hupendi anachokiandika au kukisema fair enough....sasa kitu gani kinakupeleka kwenye Ukurasa wake wa FB au Twitter au Blog na Sites?


Binafsi kama sipendezwi na Blog fulani basi sitoitembelea tena.....muda wa kuendelea kufuatilia anachokiandika ambacho mimi sikipendi sina.


Heri nitumie muda huo kupeleka Wanangu Park wakacheze au nikoshe nywele zangu au kutengeneza Kucha au kwenda kufanya manunuzi at the end nifurahi moyoni......there are so much more in life than being a Troll.


Unakosa usingizi ukifikiria nini cha kwenda kumuambia mtu in an attack way kwenye Site au Page yake.....unapata faida gani?


Mimi Dinah kuacha kublog Dinahicious is nothing to do with January Makamba au mabadiliko ya Sheria Tz ni uamuzi binafsi.



Ngoja nikusaidie kuelewa: Google walipokuja na mabadiliko ya Sheria Mwezi wa Kwanza nikapata nguvu as in excuse ya kuachana na Blog bila lawama za Wapenzi wa Blog husika.



Google imeifanya Dunia kuwa Kijiji (biggest search engine)na inafanya kazi kwa karibu na Serikali zote Duniani ili ku-protect watoto dhidi ya Ngono (na masuala mengine ya Kiulinzi ofcoz)na hivyo kila Nchi kufanya iwezavyo kuzuia upatikanaji wa Ngono kirahisi via Mitandao.



Baada ya Bloggers wa Ngono wa Muda mrefu kulalamikia kuwa google wanakuwa unfair....Google waka-withdraw uamuzi wao kuzifanya Blogs za Ngono kuwa private  au kuzifuts na ndio maana bado unaweza kuiona Dinahicious na Blog nyingine za Ngono isipokuwa ni lazima uingie ukiwa na miaka 18.



I blog from the UK.....I don't follow Bongo's Politics for nearly 3 years  sasa hivyo I know nothing about Sheria zenu.


I thought  I should help you to know the above. I didnt really have to do that....but here we are.


Try to have peace in your heart and improve your life Mwana wa Tanzania. Remain blessed.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao