Skip to main content

Posts

Showing posts with the label chuki

Hii ndio sababu ya mawifi/Mama wake kutuchukia?

Usinielewe vibaya, mie pia ni Wifi "mkubwa", lakini  tofauti ni...sio  kwamba nawachukia(hawajawahi kunikosea) au nawapenda(sijawahi kuishi nao).....nawachukulia kama walivyo na kuwaheshimu kama wanavyoniheshimu. Kamwe sijawahi/siwezi kujaji lolote kuhusu wao kwasababu siwajui kama ambavyo Kaka zangu wanawajua Wake zao. Sijawahi kuhoji kwenye  kufanana kwao na watoto wao. Huwa nasema tu mnawatoto wazuri, wapwa wangu wanapendeza n.k. Ikiwa Kaka zangu hawakuwa Makini na wanalea watoto wa wenzao, hiyo ni issue yao, sio yangu. Sasa, kuna siku nilikuwa nazungumza na Asali wa Moyo wangu kuhusu mambo ya Kijamii na tukagusia Chuki ya Wanawake kutoka Upande wa Mwanaume, akaniuliza hivi ni kwanini? Nkamwambia mie pia ni Wifi(mwanamke kutoka upande wa Kaka zangu) lakini sina Chuki na wala sifuatilii mambo yao na familia zao! Tukaenda ndani (deep)kidogo, nikagundua kuwa, chuki hii inaweza kusababishwa na moja9au yote) kati ya haya yafuatayo;- *Mwanamke anajua kuwa yeye ni

Mzazi kukupenda zaidi ya wenzio...

Habari ya sasa! Kwa kawaida Mtoto wa Kwanza na yule wa Mwisho kwenye Familia nyingi hutokea kupendwa zaidi na wazazi au Mzazi......wakati mwingine wadogo/wakubwa zake. Sababu ya kuwa "favourite" angalau kwa muda hapa ipo wazi. Mtoto wa kwanza ndio kifungua Familia na huwa peke yake kwa muda mrefu au ikitokea kuna mdogo wake kaja fasta basi ile "huruma" huwafanya Wazazi waongeze attention kwa yule wa kwanza. Mtoto wa mwisho ni mdogo kuliko wote hivyo Wazazi na dada/kaka huwa over protected. Pamoja ya kupendelewa au kupendwa zaidi bado Wazazi wengi huwa hawaonyeshi hilo kwa uwazi ili kuepusha ugomvi au kuwafanya watoto wengine kujiona hawapendwi kwa kiwango sawa. Lakini mnapofikia umri mkubwa unaweza kuona kabisa kuwa Baba na Mama wanampendelea fulani zaidi na hivyo kuanza kujenga chuki au ushindani dhidi ya mwenzenu ambae mnahisi kuwa anapendelewa. Hali hufikia pabaya, mpaka anaependelewa kuanza kujidai na kutumia kupendwa zaidi na Waza

Sababu Kuu ya Kumchukia Ex wake...

.....wengi hudhani kuwa ni Wivu au Hofu kwamba Mwanaume anaweza kurudi alikotoka au kukuacha kama alivyomuacha yule ila tofauti ni kuwa anakwenda kwa Ex wake sio Mwanamke mpya. Yote ni  sababu common lakini ile kuu ambayo wanawake wengi hutusumbua na hata kujenga dislike(nikisema hate inakuwa too strong) huenda ni hii hapa chini. Umewahi kutaka kumjua kama Mpenzi wako ana type? na pengine kwenda ndani na kutaka kumuona Ex wa Mpenzi wako kabla yako na hata kutaka kukutana nae? sio ili muwe marafiki bali ni kutaka kuona kama alikuwa Hot au Not....(hihihihihihi). Ikiwa Mpenzi wako ana type na aliempitia kabla yako alikuwa Hot basi unafurahi kuwa na wewe ni hot (pengine wala sio that hot) na kwabahati mbaya kama ex alikuwa Not basi hapo ndio hasira huja. Kila ukimfikiria/kumbuka yule Ex alivyo unamchukia vibaya sana hehehehehe huku unajisemea "am not that ugly" na kujiuliza "am I that ugly?". Yaani sio kwamba unachukia alivyo (kuwa ugly is okay but....) ba

Magaidi wa Kiislam...

Ahsante kwa kuichagua Blog hii.....natumaini umeanza Wiki yako vama. Post ya jana inaweza kukufanya udhanie kuwa naunga mkono Mauaji ya hao Waislamu(if you are that thick). Ukweli ni kuwa tangu 7/7 London Bombing sina Imani wala huruma na Waislam wa UK. Victoria line au Piccadilly ndio lines zangu then nateremkanpale KingX......siku hiyo ya Saba-saba niliamua kutega Kipindi cha asubuhi kilichokuwa kinaanza saa 9:30am.....ningetoka muda wangu wa kawaida labda leo nisingekuwa hapa. Nilipoona Waislamu nahofia kuwa wanaeza jilipua.....miezi michache ya 2005 baada ya 7/7 nilikuwa nahama behewa(kwenye Tube) su nasubiri the next one ikiwa kuna mkimama au mkibaba alievaa Kiislam au mwenye asili ya Waislam kama vile Wasomali, Wapakistan n.k. Mpaka leo karibu miaka 10 naishi masaa 8 driving kutoka London na Dakika 45 kwa ndege (Dar to Moshi....pata picha)bado naogopa kujimix na hao majamaa(wapo kila kona). Baada ya kilichotokea Tunisia hakika kinaongeza hofu na chuki inakua dhidi ya Waisla

Adui mpende.....mpende adui yako.

Hivi wewe una adui? Kusema ukweli kabisa mie sina adui which means mie sio adui wa mtu yeyote.....oh hello! Kuna wakati unazungumza na watu unaofahamiana nao(wewe unawaita marafiki) na unakutana na suala la maadui......kwamba wanawazungumzia "maadui zao" na jinsi gani wanawachukia halafu unajiuliza imekuaje mpaka hawa watu wanakuwa na maadui? Adui yako anaweza kuwa mtu yeyote kuanzia nduguyo wa damu mpaka yule uliewahi kuchangia nae mwili lakini sasa ni HISTORIA iliyofutika . Sababu za hawa majamaa kuwa maadui zinayofautiana lakini chanzo mara zote (nidhaniavyo mimi) ni ukaribu wao kwako. Ndugu: Unajua Ndugu wa damu mnapokuwa watu wazima mnabadilika (mnakuwa) na ule ukaribu wenu hupungua kutokana na mmoja wenu kuishi maisha tofauti na  (mume au mke) wake. Baadhi ya ndugu huwa bitter wakidhani kuwa huwajali tena na badala yale unajali zaidi mkeo/mumeo na "familia yake".....ni kweli halafu sio kweli kwa kisingizio cha  utahama kwenu na kumfuata mwenza wako. Jam

Faida ya kumchukia mtu usiemjua....

Ni nini hasa? Unajua kuna watu maisha yao ni ya huzuni sana bila wao kujijua. Anakaa kabisa na kutulia kisha anaanza kurusha maneno makali. Unawezaje kum-attack mtu kwa matusi wakati humjui? Hupendi anachokiandika au kukisema fair enough....sasa kitu gani kinakupeleka kwenye Ukurasa wake wa FB au Twitter au Blog na Sites? Binafsi kama sipendezwi na Blog fulani basi sitoitembelea tena.....muda wa kuendelea kufuatilia anachokiandika ambacho mimi sikipendi sina. Heri nitumie muda huo kupeleka Wanangu Park wakacheze au nikoshe nywele zangu au kutengeneza Kucha au kwenda kufanya manunuzi at the end nifurahi moyoni......there are so much more in life than being a Troll. Unakosa usingizi ukifikiria nini cha kwenda kumuambia mtu in an attack way kwenye Site au Page yake.....unapata faida gani? Mimi Dinah kuacha kublog Dinahicious is nothing to do with January Makamba au mabadiliko ya Sheria Tz ni uamuzi binafsi. Ngoja nikusaidie kuelewa: Google walipokuja na mabadiliko ya Sheria Mwezi w