Skip to main content

Adui mpende.....mpende adui yako.

Hivi wewe una adui?

Kusema ukweli kabisa mie sina adui which means mie sio adui wa mtu yeyote.....oh hello!


Kuna wakati unazungumza na watu unaofahamiana nao(wewe unawaita marafiki) na unakutana na suala la maadui......kwamba wanawazungumzia "maadui zao" na jinsi gani wanawachukia halafu unajiuliza imekuaje mpaka hawa watu wanakuwa na maadui?



Adui yako anaweza kuwa mtu yeyote kuanzia nduguyo wa damu mpaka yule uliewahi kuchangia nae mwili lakini sasa ni HISTORIA iliyofutika .



Sababu za hawa majamaa kuwa maadui zinayofautiana lakini chanzo mara zote (nidhaniavyo mimi) ni ukaribu wao kwako.



Ndugu: Unajua Ndugu wa damu mnapokuwa watu wazima mnabadilika (mnakuwa) na ule ukaribu wenu hupungua kutokana na mmoja wenu kuishi maisha tofauti na  (mume au mke) wake.




Baadhi ya ndugu huwa bitter wakidhani kuwa huwajali tena na badala yale unajali zaidi mkeo/mumeo na "familia yake".....ni kweli halafu sio kweli kwa kisingizio cha  utahama kwenu na kumfuata mwenza wako.




Jamaa na marafiki: Huna muda tena wa kukesha nao au kufanya starehe kila mwisho wa Wiki AU kuongea kwa masaa na masaa Simuni....watadai umebadilishwa na mkeo/mumeo.



Unapokuwa mtu mzima(well in your 30s aka mimi) na unakafamilia kako kuna vitu vilivyokuwa muhimu enzi za 20s havina umuhimu tena so unaachana navyo.



Sasa kwasababu ulishawahi kuwa karibu na hayo makundi niliyoyataja hapo juu ni wazi kuwa hawatakuacha uendelee na maisha yako kwa amani. Wanakuwa kama wale Exes vinga'ang'anizi waishio in Past for life(move on darling life is passing you by).



Makundi hayo yatafanya yote ili kujua unaishi vipi ili wakuharibie so that urudi kwao. Wakishindwa kabisa wanatumia ule ukaribu wao waliokuwa nao kwako na wakijuacho ili kusambaza chuki (kumbuka kuna mambo nyeti waliyajua kuhusu wewe).


Halafu kuna wale ndugu ambao inatokea tu hawakupendi (kabla ya u-30s)mpaka unahisi kuwa "mama alitereza" nje nini? Kwanini kaka/dada yangu kutoka baba na mama mmoja ananichukia hivi!



Mie sina Adui japokuwa kuna watu (maadui wa mume wangu)wanalazimisha wawe maadui zangu hihihihi lakini sitoi nafasi.



Pia nikikorofishana na mtu Familiani huwa nawaua (in my head) so wanakuwa hawa exist....siwazungumzii wala kuwaulizia na sitomwambia mtu yeyote kwanini tulikorofishana.



Ukaribu wako kwao ni kuwa easy target kwa mengi mabaya ambayo ni chanzo cha Uadui. Shukurani kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao