Skip to main content

Posts

Showing posts with the label damu

Mind your Ughaibuni business...

 Nakumbuka miaka michache nyuma nilipokuwa Twita alijitokeza Binti mmoja nakuanza kuwaambia watu wa Ughaibuni(Nchi za Ulaya na Marekani) kuachana na Siasa za Tanzania na kufurahia maisha yako "mazuri" popote walipo Ulaya(popote nje ya Afrika)....natabua kua sio kila mtu Ulaya ana maisha mazuri(inategemea sababu yako ya kuishi huko) lakini nakubaliana nae. Wabongo wengi walimkandya/ponda kwa kudai kuwa anataka attention ya Bongo Twita sababu hakuna mtu anamfahamu, binti alijitetea na kusimamia alichokisema ambacho hakika nakubaliana nae. Watu wa Ughaibuni ambao hawaishi Tanzania  wanaguswa na Mabadiliko ya kisisa yanayoendelea Tz, hawa ni wachache sana ambao wana Biashara na pengine kumiliki ardhi(nyumba, mshamba n,k,) na wachache ambao hurudi nyumbani mara kwa mara, wengine wapo wapo tu na ndio huwa na kelele zaidi kuhusu Tanzania na Siasa zake. Unadhi utabadilisha nini  Tz na Kodi hulipi? Mind your Ughaibuni business and enjoy your High tax, cost of living and free Heathcare

Adui mpende.....mpende adui yako.

Hivi wewe una adui? Kusema ukweli kabisa mie sina adui which means mie sio adui wa mtu yeyote.....oh hello! Kuna wakati unazungumza na watu unaofahamiana nao(wewe unawaita marafiki) na unakutana na suala la maadui......kwamba wanawazungumzia "maadui zao" na jinsi gani wanawachukia halafu unajiuliza imekuaje mpaka hawa watu wanakuwa na maadui? Adui yako anaweza kuwa mtu yeyote kuanzia nduguyo wa damu mpaka yule uliewahi kuchangia nae mwili lakini sasa ni HISTORIA iliyofutika . Sababu za hawa majamaa kuwa maadui zinayofautiana lakini chanzo mara zote (nidhaniavyo mimi) ni ukaribu wao kwako. Ndugu: Unajua Ndugu wa damu mnapokuwa watu wazima mnabadilika (mnakuwa) na ule ukaribu wenu hupungua kutokana na mmoja wenu kuishi maisha tofauti na  (mume au mke) wake. Baadhi ya ndugu huwa bitter wakidhani kuwa huwajali tena na badala yale unajali zaidi mkeo/mumeo na "familia yake".....ni kweli halafu sio kweli kwa kisingizio cha  utahama kwenu na kumfuata mwenza wako. Jam