Nakumbuka miaka michache nyuma nilipokuwa Twita alijitokeza Binti mmoja nakuanza kuwaambia watu wa Ughaibuni(Nchi za Ulaya na Marekani) kuachana na Siasa za Tanzania na kufurahia maisha yako "mazuri" popote walipo Ulaya(popote nje ya Afrika)....natabua kua sio kila mtu Ulaya ana maisha mazuri(inategemea sababu yako ya kuishi huko) lakini nakubaliana nae.
Wabongo wengi walimkandya/ponda kwa kudai kuwa anataka attention ya Bongo Twita sababu hakuna mtu anamfahamu, binti alijitetea na kusimamia alichokisema ambacho hakika nakubaliana nae. Watu wa Ughaibuni ambao hawaishi Tanzania wanaguswa na Mabadiliko ya kisisa yanayoendelea Tz, hawa ni wachache sana ambao wana Biashara na pengine kumiliki ardhi(nyumba, mshamba n,k,) na wachache ambao hurudi nyumbani mara kwa mara, wengine wapo wapo tu na ndio huwa na kelele zaidi kuhusu Tanzania na Siasa zake. Unadhi utabadilisha nini Tz na Kodi hulipi? Mind your Ughaibuni business and enjoy your High tax, cost of living and free Heathcare while it last.
Ukiachana na suala la Siasa, kula suala la ndugu tegemezi(wavivu), yaani kwa vile tu wewe upo Ulaya basi unabeba zigo la kusaidia kila mtu kwenye Ukoo, kama wewe sio Narcsist hili zigo haliwezi kukupa furaha wala amani na ku-feed ego yako ya kuwa wewe ndio Tajiri wa familia. Unadhohofika na kukonda /nenepa na kupata maradhi kwa kufanya kazi Masaa mengi zaidi kuliko inavyoruhusiwa kwa usalama wa afya yako, ili tu ukamalizie Bonge la jumba Tz, usomeshe watoto wa kaka zako na wa bibamu na dada zako na vimada wao....ukiulizwa kwanini unajitesa kwa ajili ya familia nyingine wakati una mke na watoto, unasema ni "Utamaduni wenu wa Kitanzania na Damu haipotei bure". Kama ndio hivyo basi mie sio Mtanzania kwakweli.
Ukirudi home(tz) ndugu zako wanag'aa kuliko wewe utadhani wao ndio wametoka Ulaya, unashangaa nini wakati wewe ni Serikali yao na damu(undugu) wenu ndio mchango wao mkuu wa mapato ili uwape Huduma nzuri za Afya, Elimu na Miundo mbinu(gari, makazi).
Kukitokea tatizo huko kwenu kama wewe sio wa kwanza kutoa mchango na kuwapa maelekezo ya nini wanapaswa kufanya basi uta kuwa pekee ulietoa Sehemu kubwa ya mchango, ukishangaa, shangaa unapigwa vibomu na kila mtu kwa wakati wake kwa suala/tatizo hilo hilo moja(wanakuchuna)...huezi kujua hili na hawatokuambia ukweli.
Upo Ulaya lakini unaishi kwenye jamii ya Maskini wa Kizungu, sasa kwa vile ni wazungu unajiona upo safi wakati Elimu yako na background yako na kiwango cha maisha kabla hujaenda Ulaya ni u-Surbabian.
Ungeweza kabisa kuishi hivyo(ki-surbabian) na kufurahisha Mkeo na watoto wenu kama ungedharau Ego yako na kujiweka mstari wa mbele kutaka kutatua matatizo ya kila mmoja anaekujia na shida zake na wakati huo huo kuwekeza kwenye ardhi ambayo unajua kabisa haitokuwa na faida kwako wala wanao isipokuwa Ndugu zako ambao zaidi ya kuchangia damu, hawana umuhimu kama wanao unaoishi nao Ughaibuni.
Sisemi usiwajali ndugu zako isipokuwa nakukumbusha kuwa ndugu hao wanafamilia zao walizozianzisha wao na nijukumu lao kubeba mahitaji yote muhimu. Ikitokea wanahitaji msaada once in while, sio mbaya kusaidia lakini kujiweka mbele kama vile wewe ni Serikali, sio nzuri kwa afya yako ya akili, sio haki kwako kwa mkeo na kwa watoto wenu. Kumbuka ukiugua na hata ukijifia mapema kwasababu ya kuji-over work kwasababu ya Ndugu Tz...Mkeo na watoto ndio watakaohangaika. Piga kazi kwa kiwango cha kutosha bila kuathiri afya na ku-provide kwa ajili ya familia yako uliyoianzisha aka Legacy yako na acha kila mtu abebe familia (Msalaba) yake.
Hao ndugu unaowasaidia ndio huwa wanaweka kikao na kukujadili, jamaa kamaa Miaka 30 Ulaya lakini hana hata tofali la choo, Kiwanja. Wanasahau kuwa kipato chote kinaishia kwao na familia zao. Kuna faida gani ya kupata sifa na kuzikwa na watu wengi kwasababu ya wema wako lakini unaacha Legacy yako inataabika Duniani? Toa msaada inapohitajika na umeguswa, kisha mind your Ughaibuni business.
Nitakuona baade...
Comments